Ndiyo, alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. Lakini ili dhambi zetu ziondolewe ni lazima tukiri kwamba sisi ni wenye dhambi, tutubu na kumpokea Yesu atawale maisha yetu. Wanaokataa kufanya hayo ndio watakaohukumiwa kwenda motoni siku ya hukumu.swali gumu :kama yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zenu siku ya hukumu ya nini?
1. Atashukia wapi ili kila mmoja aweze kumuona kwa wakati mmoja, ikiwa jua tu huwa halionekani kwa wakati mmoja kwa watu wa Dunia yote.Heshima zenu wakuu.
Leo nawaletea mpangilio(timeline) au mtiririko wa mambo mazito sana yatakayotokea Yesu atakapokuja. Maandalizi yanayofanyika nchini Israeli, ya kujenga hekalu la tatu, ni ushahidi wa wazi kuwa Yesu amekaribia kuja.
![]()
Rais Trump ashuhudia maandalizi makubwa ya kumpokea Masihi, nchini Israeli !!
Ndugu zangu, habari ya mjini ndio hii. Kiongozi mwenye mamlaka makubwa ya kidini nchini Israeli ametamka wazi mbele ya Rais Trump kuwa Waisraeli wanajiandaa kujenga hekalu la tatu, kubwa, mjini Yerusalemu. Ujenzi wa hekalu la tatu ni hatua muhimu sana kwa Waisraeli katika maandalizi ya kumpokea...www.jamiiforums.com
Nakusihi usome kwa makini uzi huu usije ukasema hukujua au hukuambiwa, mambo haya yatakapoanza kutokea:
1. Kunyakuliwa kwa Kanisa
Tukio hili litafanyika wakati Yesu atakapokuja mawinguni kulichukua Kanisa, yaani wote wanaomwamini (1 Thes 4:16-17). Waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza na kuungana na watakatifu walio hai duniani – kisha Yesu atawanyakua na kuwapeleka mbinguni na kukaa nao kwa miaka 7.
2. Kiti cha Hukumu cha Kristo na Arusi ya Mwanakondoo
Baada ya kunyakuliwa, waaminio watasimama mbele ya Kristo kupokea thawabu ya kazi waliyoitenda duniani. (2 Korns 5:10) – Kazi ya kila mtu itapimwa (1 Kor 3:12-15). Baada ya hapo Watakatifu watasherehekea pamoja na Kristo arusi ya Mwanakondoo. Hii ndiyo arusi(wedding banquet) niliyoizungumzia katika Mwaliko niliowapa members wote wa JF!
![]()
MWALIKO: Karibuni wote kwenye harusi kubwa na ya kifahari kuliko zote!
Ndugu wapendwa wote wa JF, Ninayo furaha tele kuwaalika kwenye sherehe ya harusi itakayokuwa kubwa sana kuliko zote zilizowahi kufanyika duniani! Ni wedding banquet la nguvu. Mnaopenda nyama choma, pilau, kuku, chips mayai, uyoga, karanga, kisamvu, mlenda, juice - mtakunywa na kula vyakula...www.jamiiforums.com
3. Miaka 7 ya Dhiki Kuu
Wakati Wateule wakisherehekea Arusi ya Mwanakondoo mbinguni, watakaobaki duniani watapata dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Wanaomlalamikia sasa Mungu eti kama ana upendo kwanini anaruhusu vita, njaa na mateso, kipindi hiki cha dhiki kuu ndio watatoa maneno ya kufuru kabisa kutokana na mateso mazito watakayopata chini ya utawala wa Mpinga Kristo(Mt 24:21; Dan 9:27; Ufu 13:16-17 Mpinga Kristo atamlazimisha kila mtu apokee chapa ya mnyama(666). Atakayekataa kuipokea hataweza kuuza wala kununua chochote.
4. Yesu Atarudi Tena Duniani na Kutawala Miaka 1000
Baada ya miaka hiyo 7 ya Dhiki Kuu, Yesu atakuja duniani kwa utukufu mwingi na kila jicho litamuona (Ufu 19:11-16; Zek 14:4; Mt 24:30). Yesu atamshinda Mpinga Kristo na Nabii wa uongo na kuwatupa katika ziwa la moto na shetani atafungwa kwa miaka 1000 (Ufu 19:19-20; Ufu 20:1-3) ndipo Yesu Kristo atakapoanza kutawala kwa miaka 1000. Miaka hii itakuwa ya haki na amani kabisa duniani (Ufu 20:4-6). Kipindi hiki hata wanyama wa mwituni hawatakuwa na madhara(Isa 11:6-9). Mwishoni mwa kipindi hiki shetani ataachiliwa kwa muda mfupi, atawadanganya watu lakini Mungu atamshinda na kumtupa katika ziwa la moto milele(Ufu 20:7-10).
5. Kiti Kikubwa Cheupe cha Hukumu
Waliokufa katika dhambi watafufuliwa na kuhukumiwa kwenda katika ziwa liwakalo moto.
(Ufu 20:11-15)
6. Mbingu Mpya na Nchi Mpya
Mungu ataumba mbingu mpya na nchi mpya. Watakatifu wataishi milele pamoja na Bwana(Ufu 21:1-4; 2 Pet 3:13)
7. Ni nini kitakachotokea kwa Waisraeli?
- Wakati wa Dhiki Kuu (Juma la 70 la Danieli) Waisraeli watateseka sana.
- Mpinga Kristo atafanya na Waisraeli mkataba wa uongo wa kuleta amani mwanzoni mwa miaka saba ya dhiki kuu(Dan 9:27). Katikati ya miaka hiyo (yaani baada ya miaka 3 na nusu), Mpinga Kristo atawasaliti Waisraeli, ataingia hekaluni na kudai yeye ndiye Mungu. Hapa unaweza ukaelewa sasa kwanini Waisraeli wanaandaa hekalu la tatu. Mpinga Kristo ndiye chukizo la uharibifu linalotajwa katika Mt 24:15-16 litakalosimama patakatifu.
- Waisraeli watatubu na kuokolewa mwishoni mwa miaka 7 ya Dhiki Kuu na kumtambua Yesu kuwa ndiye Masihi wao (Zek 12:10; Rum 11:26). Hii itatokea kabla Yesu hajaja mara ya pili kutawala dunia kwa miaka 1000.
mnatubu vipi wakati hamna dhambi?Ndiyo, alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. Lakini ili dhambi zetu ziondolewe ni lazima tukiri kwamba sisi ni wenye dhambi, tutubu na kumpokea Yesu atawale maisha yetu. Wanaokataa kufanya hayo ndio watakaohukumiwa kwenda motoni siku ya hukumu.
kwa hyo dhana kuwa yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zenu ni uongo?Ingekuwa hamna dhambi magereza yasingekuwepo, mkuu
Wokovu na maisha safi ndani ya wokovu ndio unaenda ,Arusi hii ni Arusi ya Mwanakondoo, Bwana wetu Yesu Kristo. Ameiandaa kwa ajili ya Bibi arusi wake—Kanisa lake takatifu!
Ufunuo 19:7
"Tufurahi na kushangilia; tumtukuze, kwani wakati wa arusi ya Mwanakondoo umefika, na bibi arusi yuko tayari."
Bibi-arusi ni wale wote waliotubu dhambi zao na kumwamini Yesu Kristo. Ni wale wanaoendelea kujiweka tayari kwa ujio wake kwa kuishi maisha matakatifu (Ebr 12:14).
Sherehe ya arusi itafanyika mbinguni baada ya Yesu kuja kulinyakua kanisa.
Siku na saa hatuijui, lakini dalili zinaonyesha Yesu yuaja upesi(Ufu 22:12)
Kiingilio ni WOKOVU tu.
Kama hujaokoka, sali(omba) sala hii ya toba, utapata tiketi ya kuingia mbinguni kusherehekea Arusi hiyo:
Omba(fuatisha) sala hii kwa moyo wako wa dhati:
“Mungu Baba, natambua mimi ni mwenye dhambi. Sina tiketi ya kuingia mbinguni. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu hadi siku utakayokuja kutunyakua na kutupeleka mbinguni. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, naomba na kushukuru. Amen.”
Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Umepata tiketi ya kuingia mbinguni kwenye sherehe ya Arusi ya Mwanakondoo. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuendelea vizuri kiroho. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu ujiunge nalo; ujifunze mambo mengine yakupasayo kufanya wakati huu tunapoendelea kumgojea Bwana Arusi Yesu Kristo. Ubarikiwe sana!
Tit for tati, inabidi wamfie kristo, howHio miaka saba ya dhiki kuu wale walioachwa na wanahitaji kuokoka wanafanyaje?
Kumfia kivipi ndio nataka nijue, maana hakuna tena huduma ya kiroho, kama mchungaji au Askofu amebaki maana yake wote hao sio wa Yesu tena.kwahio hapo inamaana tunakataa chapa ya 666 mpaka tufe kwa kukosa huduma?Tit for tati, inabidi wamfie kristo, how
Huduma unazopata hapo sasaiv huta kuwa na access, hakutakuwa na kuuza wala kununua bila kuwa na chapa ya666
Kumfia kivipi ndio nataka nijue, maana hakuna tena huduma ya kiroho, kama mchungaji au Askofu amebaki maana yake wote hao sio wa Yesu tena.kwahio hapo inamaana tunakataa chapa ya 666 mpaka tufe kwa kukosa huduma?
Aise hii sio ya kuombea ikukute ukiwa haiKiuchumi utazuiwa (huwezi kununua wala kuuza).
Kisheria utaonekana adui wa mfumo.
Ndiyo maana wengi watateswa au kuuawa.
Issue hapa ni kutotii mfumo itaambatana na mateso makali, hapa ndipo kumfia yesu kwa atakaye vumilia hadi mwisho, Ila Mungu atafupisha kipindi cha mateso hayo, akiacha hakuna atayechomoka aisee😂😂😂
yeah means njia ni mbili kuiokoa rohoAise hii sio ya kuombea ikukute ukiwa hai
Kuchagua njia sasahivi ni ngumu, ni kuombea kunyakuliwa tu ila ikitokea ukabaki ndio utaamua hapo hapo dhiki kuu ikikufika😀yeah means njia ni mbili kuiokoa roho
1. Upitie treni ya unyakuo , kitu ambacho kwa kweli ki kigumu, yani kuwa mtakatifu mda wote , unaweza kuwa mtakatifu then ukatenda dhambi moja tu, ile unawaza kutubu mara unyakuo huo, umeachwa😂
2. Treni ya mateso, na umeshaambiwa mateso yatakayokuwepo toka dunia kuumbwa hayajawahi tokea, emfikiria hii itakuaje?, unashuhudia ndugu marafiki , wakikamatwa na kukatwa vichwa, 😂😂
Kwakweli lazima utajiunga na chama tu na kutii mfumo.
SASA CHAGUA WEWE MKUU NJIA IPI