Yajue Mapinduzi ya Niger kwa upana zaidi

Refinery unazijua vizuri au una adithiwa? Unajua bei ya lita moja ya mafuta Nigeria?
 
Naipenda ntarudi kuusoma vema
 
Mzuri
 
"The Enemy of your Enemy is your Friend". Kanuni hii kwa Master plan - Putin, yeye anaitumia kinyume chake. Anachofanya ni kuvuruga urafiki na kukubalika kwa Marekani ndani ya Afrika.

Sijui unanielewa?!

Kwa miaka mingi Urusi amekuwa akikutana na vigingi vya Marekani hasa pale anapotaka kufanya biashara na nchi za Afrika na hata upande wa "Geopolitics". Sasa ili kuondoa hivyo vigingi, Putin anataka kuitenganisha Afrika na Marekani kwa kuwaambia Waafrika kwamba mnaweza kujitegemea, mnaweza kuishi bila Marekani, na kwa kuanza mimi (Urusi) nitawasaidia katika hiki, kile na hiki.

Kwanza mkutano wenyewe Rais Putin aliupa jina la NEW WORLD MULTIPOLAR STRUCTURE. Kwa wasiofahamu "Multpolar" ni mifumo tofauti tofauti ya kiungozi isiyotegemea mfumo mmoja. Na hapa Rais Putin analenga kuondoa ukiritimba wa Marekani katika kuitawala Dunia nzima na sio Afrika peke yake.

Kuhusu silaha: Kuna mtu humu anasema kwamba Putin amesema atatupatia silaha, hivyo ni jambo la hatari kwa Afrika. Huu ni ujinga mwingine tena wa hali ya juu sana. Marekani ndio muuzaji kinara wa silaha, na nyingi anauza kwenye nchi za Afrika. Na ndio sinazotumika katika mapinduzi haramu na uasi. Sasa Urusi akitupatia silaha na mafunzo ili tuwe na uwezo wa kujilinda dhidi ya hayo mapinduzi haramu, shida ipo wapi?!

Mkutano wa Putin na viongozi wa nchi za Afrika.

Mkutano wa Rais Putin na viongozi wa nchi za Afrika ulikuwa na lengo moja tu, nalo ni;- Kuifungua dunia mpya ya kibiashara na ushirikiano ambayo haitoitegemea nchi za Magharibi. Hayo mengine ni kufanya "lobbying" ili kuvuruga ajenda.

Katika mkutano huo, Rais Putin aliiahidi kusaidia Afrika kwenye sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na ku-train majeshi ya nchi za Afrika ziwe na uwezo wa kujilinda dhidi ya mapinduzi haramu. Mapinduzi haramu ni yale ambayo mara nyingi nchi za Magharibi huya-engeneer ambapo hupindua serikali na kuweka vibaraka wao. Kumbuka mapinduzi ya Niger yamepewa baraka na wananchi wa Niger. Ni kama ilivyokuwa kwa "Arabian Spring" ikiwemo ile iliyomuondoa madarakani Hosni Mubarak ambapo wananchi waliunga mkono mapinduzi na upande wa Magharibi ukaunga mkono wananchi.

Kingine Rais Putin amesema;- Afrika inastahili nafasi kwenye UNSC (United Nations Security Council). Kwa wasiofahamu, UNSC ni Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na lina "council" mbili. Moja ni PERMANENT MEMBERS yenye members 5 tu (China, Marekani, France, UK na Urusi) alafu kuna GENERAL ambapo kuna wakati nchi za Afrika huingia. Sasa Putin anataka na nchi mojawapo kutoka Afrika iingie kwenye PERMANENT MEMBERS.

Kingine Rais Putin anaunga mkono Afrika kuwa "Permanent Member" wa G20. Wakuu hili sio swala dogo na huwezi kusikia vyombo vya habari vya Magharibi vikiandika. Rais Putin ameahidi kusaidia Afrika katika sekta mbalimbali ikiwemo teknolojia, kilimo, jeshi, mawasiliano, pamoja na kuzikwamua katika ukoloni (decolonization). Haya ni miongoni mwa mambo ambayo vyombo vya habari upande wa Magharibi havitaki kuyaandika.

Rais Putin amesamehe nchi za Afrika deni lenye thamani ya dollar B23. Umewahi kusikia UN, IMF, World Bank, US, EU au mashirika mengine ya nchi za Magharibi yakisamehe deni kubwa kiasi hiki?! Na kwa upana wa aina hii?! Unaambiwa hao wenyewe huwa hawasameheani. Juzi tu, Ulaya wamemaliza kuilipa Marekani kwaajili ya msaada wa World War 2. Wakati German wanadaiwa zaidi dollar 230B. Ukipata muda ingia mtandaoni, soma utaona ninachokueleza.

Ndugu zangu, kwa sasa upande wa Magharibi wamemeza mfupa na umewakwama kooni. Wanatakiwa wafanye maamuzi ili kujiokoa, aidha wauteme au ikibidi waumeze.

Uamuzi upo chini yao.
 
Ila hiyo ya kusema, US anatoa siraha kwa waasi na wakati huohuo kwa serikali ili waendelee kupigana mbona kama haimake sence??

Hata kama serikali za kiafrika sio makini ila sio kwa kiasi hicho mkuu, yaani uone mtu anakupa siraha wewe na anampa adui yako na bado uendelee kumuamini.
Au ni kua hiyo ni siri mnayoijua wachache huko hizo serikali nufaika hazijui hiyo sir??
 
Mkuu ni Crude oil,barrel ni drum ''Pipa''
 
Kwa akili za kawaida kwa inteligency waliyokuwa nayo WEST na dunia nzima wanashindwa kumaliza ugaidi Duniani? Mfano ni wale ISIS wanapata wapi silaha na magari mapya ya TOYOTA kila mwaka wanabadilisha wanavyotaka tena sehemu wanazokaa zinajulikana kabisa? Unaamini kuwa wanashindwa kukomesha ili janga apo NIGER tayari Alqaeda wameshapewa green light kuakikisha WAGNER wanafeli kusimamia ulinzi wa iyo nchi ..Ugaidi umeletwa ili wapate gia za kuingilia kwa kigezo cha kupambana na Ugaidi uku wanachukua raslimali zako na wewe ukiachwa maskini wakutupwa.
 
Bila shaka uwezo wa akili yako ni mdogo ktk mambo kama haya yaache tu yakupite, maana jibu umepewa kabisa usa ananufaikaje lakin hujaelewa.
 
Toa ushahidi kuwa mashariki ya kati ndo inatengeneza hayo makundi
 
Bila shaka uwezo wa akili yako ni mdogo ktk mambo kama haya yaache tu yakupite, maana jibu umepewa kabisa usa ananufaikaje lakin hujaelewa.
Sawa,achana uwezo mdogo wa akili,na Hilo usilifanye kuwa hoja kwasasa.
Narudia tena,huyu Rabi ni Muongo.
Kadanganya kuhusu Refineries.
Anasena Nigeria hakuna Refinery wakati Dangote mwenyewe tu anazo kwa ajili ya viwanda vyake achilia mbali na Serikali.
Anasema US inategemea Mafuta ya Nigeria wakati graph inaonyesha mtumiaji wa mafuta ya Nigeria ni India na Spain.
Then tukisema huyu Rabi/Mwalimu ni muongo wapenda porojo kama nyie mnatuita tuna matatizo ya akili,shauri yako.
 
30% ya Uranium ya Ufaransa inatoka Kazakhstan, Uranium kutoka Niger kwenda Ufaransa ni 20% sasa sijui wewe hiyo 60% ya umeme wa Ufaransa inatokana na Uranium ya Niger umeipata wapi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…