Yajue masharti ya kufuga njiwa: Hawapendi Umbea na Ulevi

nashawishika kuwafuga ila kamba zimezidi kwa thread
 
Hahaha ulijuaje mkuu? Mimi kaka yangu alikua anafungua kale kadirisha wanachopitia na anchotumia kuwapa chakula bas mara mnaona njiwa mgeni juu ya paa mara kaingia akishaingia anafunga hicho kidirisha anafungua mlango mkubwa anamnyonyoa mabawa anakua tayar kishamteka nilikua nainjoi sana the way wanafuga ilifikia point akiwafungulia wanamrukia mkononi hivi anawaita ana mluzi anapiga hata kama wako mbali watakuja na hadleo wanafuga walinifundisha pia jinsi ya kumjua jike na dume na njiwa ni waoga sana
umenikumbusha mbali...mateka. Alaf kuna mafundi wa kuteka. Ni kukaa karib na kaka zako ama?kwenye jamii yetu nayoishi haya ya njiwa ni michezo ya vijana wa kiume
 
Mengi uliyoandika ni uongo,nimefunga njiwa kwa zaidi ya miaka mitano(ni miaka 16 leo lakini kumbukumbu zao ninazo,baada ya kwenda shule mbali nje na nyumbani wakaisha maana walikoswa msimamizi.
 
14. Njiwa ukitaka kuwashika kwajili yakuuza , kuchinja, unatakiwa uwashike usiku sababu usiku huwa hawaoni...ukimshika mmoja mchana wanaobaki wakiona huondoka wote
 
asante kwa darsa. nachokupendea bibi si mchoyo wa ilimu adhimu kama hizi.
 
unawapaje taarifa
 
Kuna ya ukweli na ya uwongo mengi pia umejaza. Mimi njiwa nimefuga.
 
Huyu hajafuga mama. Amesimuliwa tu uongo mwingi nae kauleta hapa.
 
Mi naombeni njia za kuwatimua tuu,wamehamia kwangu na wamezaliana mnoo,kila siku wanadondosha ceilling board za kuzunguka nyumba,nawatwanga manati ila ndio kama nimewaongezea kasi ya kuzaliana...

Upo wap Mkuu nije kuwachukua.
 
Mi naombeni njia za kuwatimua tuu,wamehamia kwangu na wamezaliana mnoo,kila siku wanadondosha ceilling board za kuzunguka nyumba,nawatwanga manati ila ndio kama nimewaongezea kasi ya kuzaliana...
[emoji3][emoji3][emoji3] kamata mmoja chinja mchana mbele yao watasepa
 
1:Kwanza kabisa Njiwa ukiwanunua kwa mtu,sharti wawe wawili pair (dume na jike).

2:Kama muuzaji aliwafuga kwa banda la juu,hakikisha unakowapeleka uwaandalie banda la juu,ukiwaweka banda la chini wanaondoka.

3:Kama banda lako la chini,tafuta muuzaji mwenye banda la chini ndipo ununue vinginevyo unashauliwa uwanyonyoe manyoya na kuwafungia siku 40 kabla ya kuwafungulia.

4:Njiwa wakiwa mbele yako usipende kuwajadili,hawapendi masimango wataondoka!.

5:Ukifuga Njiwa nao hufatilia nyendo zako,ukiwa mlevi hawakai wanaondoka.Vurugu na kelele hawapendi.

6:Njiwa wana nguvu kiimani,hawapendi mfugaji awe Mmbea,kugombana na majirani.Kwa sababu wakatika wa ugomvi Njiwa hukaa juu ya Paa wakisikiliza halafu huondoka na hawarudi tena.

7:Njiwa hawapendi kuona umechinja Njiwa mwenzao mbele yao,wakiona wanahama wote kwa sababu wanahisi utawachinja.

8:Njiwa hawapendi makelele ya kushtukiza kama honi kali,kuwarushia jiwe na miziki mikubwa.Ukifanya hayo wanahama.

9:Njiwa akifa mmoja,huomboleza.Unashauliwa umtafute mwenza haraka kwa Njiwa anaebaki la sivyo wanaondoka/kuondoka.

10:Hakikisha Njiwa huwachanganyi na kuku mwenye vifaranga,wakiparuliwa huondoka mazima.

11:Njiwa wanaofugwa banda la Uani/nyuma/
jikoni huzaliana haraka zaidi kwa sababu ya mazingira tulivu.

12:Hakikisha Pakashume hawazoei kufika nyumbani kwako!.Njiwa hawapatani na Paka pori la sivyo wanahama wote!

13:Inasemekana Njiwa ni wa pili kwa wivu baada ya Nyegere..



Nakumbuka mbali sana nimuonapo njiwa,aliimbwa wakati huo nafaidi muziki,aliimbwa wakati uleee katika igizo la kidedea,kina tabia na jengua.....

Ewe njiwa,ewe njiwa peleka salaaamu.....

Way too far,i waa able to hear.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…