Porojo tupu. Mie nafuga njiwa tena wengi sana, hawa wa kawaida, wana rangi na patterns mbali mbali na wengine ni weupe kabisa. Nilianza na wanne tu baada ya mwaka wakawa zaidi ya 30, sasa hivi wanazidi 300, siwezi kuwahesabu.
Wanaishi juu ya banda kubwa la kuku, walivyo kuwa wanazidi nikawawekea dari za mbao za marine ambazo nimeziongezea coat ya waterproof hardner.
Kitoweo kitamu sana. Siku nikitamani huwa nachinja 20 mpaka 30, Na nimegawa wengi sana na nimeuza wengi sana.
Wao mradi chakula kwa wingi (Mtama, choroko, kundi) na maji safi ya kutosha kwenye mabeseni, wanapenda sana kuoga kwenye maji.
Hakikisha wanapoishi hakuna access ya paka, panya na nyoka.
Mengine yote ni myths.