Yajue masharti ya kufuga njiwa: Hawapendi Umbea na Ulevi

Yajue masharti ya kufuga njiwa: Hawapendi Umbea na Ulevi

Porojo tupu. Mie nafuga njiwa tena wengi sana, hawa wa kawaida, wana rangi na patterns mbali mbali na wengine ni weupe kabisa. Nilianza na wanne tu baada ya mwaka wakawa zaidi ya 30, sasa hivi wanazidi 300, siwezi kuwahesabu.

Wanaishi juu ya banda kubwa la kuku, walivyo kuwa wanazidi nikawawekea dari za mbao za marine ambazo nimeziongezea coat ya waterproof hardner.

Kitoweo kitamu sana. Siku nikitamani huwa nachinja 20 mpaka 30, Na nimegawa wengi sana na nimeuza wengi sana.

Wao mradi chakula kwa wingi (Mtama, choroko, kundi) na maji safi ya kutosha kwenye mabeseni, wanapenda sana kuoga kwenye maji.

Hakikisha wanapoishi hakuna access ya paka, panya na nyoka.

Mengine yote ni myths.
Una raha sana Dada Faiza

Hivi kumbe ni watamu? Naona mdogo wangu anawauza tu hatujawahi waonja
 
Mi naomba kuuliza kwanini njiwa manga wanapenda sana nyumba za kishua? Yaani nyumba ikiwa ya hovyo hovyo huwezi kumkuta katua hta kwa bahati mbaya.....ila nyumba za kishua utawakuta wamejazana mpaka basi
wanapenda kula baga na soseji! huko uswazi utawalisha ukoko
 
Ukiachana tofauti ya bei ya njiwa huanzia elfu 10 pair moja ya njiwa Wa kawaida, elfu 60 kwa wale weupe, na wengine wapo wanauzwa hadi laki 8 kwa pair moja!

(Kazi moja ya njiwa ni urembo,burudani,kitowewo na baraka)

Kabla ya kufuga njiwa hao ni vyema sasa kutambua masharti yao;
  1. Kwanza kabisa njiwa ukiwanunua kutoka kwa mtu, sharti wawe wawili pair (dume na jike)
  2. Kama muuzaji aliwafuga kwa banda la juu, hakikisha unakowapeleka uwaandalia banda la juu, ukiwaweka banda la chini wanaondoka
  3. Kama banda lako la chini, tafta muuzaji mwenye banda chini ndipo ununue vinginevyo unashauliwa uwanyonyoe manyoya na kuwafungia siku 40 kabla ya kuwafungulia.
  4. Njiwa wakiwa mbele yako usipende kuwajadili, hawapendi masimango wataondoka!
  5. Ukifuga njiwa nao hufatilia nyendo zako, ukiwa mlevi hawakai wanaondoka kwasababu wanaamini mlevi anaweza sahau kuwafungulia bandani siku moja
  6. Njiwa wana nguvu kiimani, hawapendi mfugaji awe mmbeya kugombana na majilani, kwasababu wakati Wa ugomvi njiwa hukaa juu ya paa wakisikiliza halafu huondoka na hawarudi tena
  7. Njiwa hawapendi kuona Umechinja njiwa mwenzao mbele yao, wakiona wanahama wote kwasababu wanahisi utawachinja.
  8. Njiwa hawapendi Makelele ya kushtukiza kama honi Kali, kuwarushia jiwe na miziki mikubwa, ukifanya hivyo wanahama
  9. Njiwa akifa mmoja, huomboleza, unashauliwa umtaftie mwenza haraka kwa njiwa anaebaki la sivyo wanaondoka
  10. Hakikisha njiwa huwachanganyi na kuku mwenye vifaranga, wakipararuliwa huondoka mazima.
  11. Njiwa wanaofugwa banda la uani/nyuma/jikoni huzaliana haraka zaidi kwasababu ya mazingira tulivu
  12. Hakikisha pakashume hawazoei kufika nyumbani kwako! njiwa hawapatani na paka pori la sivyo wanahama wote!
  13. Inasemekana njiwa ni Wa pili kwa wivu baada ya nyegele! Hakikisha unafuga wawiliwawili.
Hayo ni machache tu kati ya masharti ya njiwa!!!
View attachment 1101970

HAKUNA chochote cha ukweli ulichoandika hapa juu. Yote uliyoyasema mimi baadhi nimeyafanya kam kuwasema njiwa yupi tukamkamate na kumchinja na hakun njiwa hata mmoja aliyetoroka. Tuache kudanganyana na kuaminishana uwongo.
 
chinja mmoja mbele yao utapata majibu;
,
 
Njiwa ukimchungulia wakati anataka kutaga hata kama yao lilisha anza kutoka analirudisha ndani hadi njiwa dume awepo[emoji1787]
hii hata kuku, au paka wakikutanisha vikojoleo vyao, huwa cha mwenzake kinajaa vumbi na kuwa kikavu .. show inasimama
 
Porojo tupu. Mie nafuga njiwa tena wengi sana, hawa wa kawaida, wana rangi na patterns mbali mbali na wengine ni weupe kabisa. Nilianza na wanne tu baada ya mwaka wakawa zaidi ya 30, sasa hivi wanazidi 300, siwezi kuwahesabu.

Wanaishi juu ya banda kubwa la kuku, walivyo kuwa wanazidi nikawawekea dari za mbao za marine ambazo nimeziongezea coat ya waterproof hardner.

Kitoweo kitamu sana. Siku nikitamani huwa nachinja 20 mpaka 30, Na nimegawa wengi sana na nimeuza wengi sana.

Wao mradi chakula kwa wingi (Mtama, choroko, kundi) na maji safi ya kutosha kwenye mabeseni, wanapenda sana kuoga kwenye maji.

Hakikisha wanapoishi hakuna access ya paka, panya na nyoka.

Mengine yote ni myths.
na kuhusu kuhisiwa na mambo ya kina Mshana Jr , ( samahani brother!!!)???
 
Back
Top Bottom