Yajue masuala mbalimbali kuhusu Biashara ya kuuza Juisi ya matunda ya aina mbalimbali

Chuck j

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2011
Posts
2,366
Reaction score
828

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
Nataka kufanya biashara ya juice,hii ya kutengeneza,matunda ya embe na nanasi,nawapa wadada wanaenda kuuza maeneo kama masokoni na kwenye mkusanyiko wa watu wengi,msaada wa kuboresha na kuifanya kwa anaejua.
---
---
---
Wadau,

Nina mtaji wa kuweza kufanya biashara ya juisi. Lakini tatizo bado sijapata mahali pazuri pa kufanyia biashara wala sijapata mfanyakazi wa kufanya naye hiyo biashara. Niko Dar es Salaam.

Mwenye uzoefu au anayejua chochote tuwasiliane hasa PM


BAADHI YA MAONI NA UFAFANUZI ULIOTOLEWA NA WADAU WA JF
---
---
---
===
CHANGAMOTO YA BIASHARA KUUZA JUISI NA NAMNA YA KUIKABILI
Kuharibika
Kutokana Na kuwa juisi unayotengeneza haina kemikali yeyote iliyoongezwa ili kuitunza hivyo huweza kuharibika pindi ikikaa kwa mda wa zaidi ya saa 24.

Kumbuka Juisi atakayopeleka mteja aliyesambaziwa ataiweka kwenye jokofu lake Na kawaida ya wafanyabiashara hawezi kuwasha jokofu mda wote hivyo uhakika wa Juisi kukaa kwa mda mrefu unakuwa mdogo.

Nini kifanyike?
1. Usitengeneze Juisi nyingi wakati unaanza
tengeneza Juisi kidogo huku ukizidi kupanua masoko yako. Hii itakusaidia kuzijua changamoto zinazokupata zikiwa kidogo Na kuzitatua bila ya kupata hasara kubwa sana.\

2. Weka Juisi kidogo kwa mfanyabiashara
wakati mnaanza biashara usizidi pakiti tano kwa sehemu inayochangamka Na pakiti tatu kwa duka linadolola.

3. Fungasha Juisi za bei ya chini
kuanzia miatatu Na miambili ikiwezekana Na za Mia Mia usifungashe za miatano maana makampuni makubwa yanatengeneza Juisi za bei hiyo hivyo hutaweza ushindani utakuwa mkubwa.

4. Kila siku hakikisha Unafanya ukaguzi kwa wafanyabiashara uliowasambazia Juisi zako
ili kuangalia kama kuna Juisi zilizokaa zaidi Na zinaweza kuwa zimehatibika uzibadirishe. Kubali kuingia hasara hii maana itakufanya uimarishe soko lako Na kulilinda.

Kama hutabadirisha mfanyabiashara mwingine anaweza kuwapatia Juisi kama zilivyo Na kujikuta wateja wanahama kutumia juice zako. Sio hasara kwa mfanyabiashara kuona Juisi hazina wateja tena akaacha kuziuza tena Na wewe kupunguza soko. Biashara ikipanuka kazi hii unaweza kumpa mtu mwingine ili kupunguza majukumu Na kumudu usimamizi

5. Usipende faida kubwa
Hii huangusha sana wafanyabiashara wengi sana, ukiwaza kupata faida kubwa sana sio mbali biashara yako itakufa.
Waza kupata wateja wengi sana Na kama unavyojua Tanzania yetu watu wengi hupenda vitu vya bei ya chini ndo maana utaona watu wengi wananunua maji ya Mia yaliyofungwa Na kuacha ya miatano

6. Mazingira safi
Tengeneza Juisi yako katika mazingira ya wazi ukiimarisha usafi Na umakini mkubwa. Nunua sare nyeupe pea kama sita Na vikofia Na grovuzi za kuvaa wakati wa kutengeneza Juisi, Osha vifaa vyako vikae vikiwa safi hadi Juisi ionekane ilivyokaa kwenye kifaa mazingira yasafishwe Na kuwa mbali Na vitu hatarishi kama:
- choo
-Mshimo la taka
Usijifiche watu wakaanza kukutilia mashaka
Zalisha Juisi yako mapema sana kuanzia saa kumi hadi saa kumi Na mbili uwe umemaliza Na kupaki katika kipindi cha awali ili kuwezesha wasambazaji kupeleka Juisi kwenye masoko kwa wakati, yaani kufikia saa tatu masoko yote yamesambaziwa juisi.

7. Malipo mazuri kwa wasambazaji na wafanyabiashara
Wape faida kubwa wasambazaji Na wafanyabiashara ili kupata molali ya kuendelea kuuza Juisi yako Na uzidi kuliteka soko.

8. Simamia mwenyewe
Nakwambia hivi simamia biashara yako kwa asilimia Mia. Simaanishi ufanye kazi zote peke yako usije ukanielewa tofauti nasema simamia biashara yako mwenyewe usimpe kazi mtu mwingine halafu wewe ukajiweka kama bosi mkusanya pesa utalia mda sio mrefu.

Hakikisha kila unachokiwaza kinatekelezwa Na uliyemuagiza usicheke Na mtu kazini hapa pesa Mzee umewekeza, usijiondoe
 
Nataka kufanya biashara ya juice,hii ya kutengeneza,matunda ya embe na nanasi,nawapa wadada wanaenda kuuza maeneo kama masokoni na kwenye mkusanyiko wa watu wengi,msaada wa kuboresha na kuifanya kwa anaejua.

Si mbaya, ila may be uwe makini na package yaani uweke katika chupa/sijui container safi, za kuvutia nk, Suala la usafi pia nk, mie ni hayo tu..ila wauza juice ni kama vile wengi so yako inabidi iwe tofauti kidogo in terms ya hiyo packaging, na mambo kadha wa kadha, bila kusahau matangazo na hudumu bora kwa wateja...ngoja waje winging
 
Ndugu wanajamii forum, Kwanza natoa pongezi kwa jukwaa hili la wajasiliamali. Mimi ni mdada mwajiliwa tayari ila ninapenda sana kujiajili ama kuwa na kibiashara changu pembeni kinachoniingizia hela kwa matumizi mengine madomadogo ya familia.

Ninawaza kuanza kutengeneza juice original ya embe, parachichi, ndizi na mengineyo na kuweka kwenye kijiwe changu, je inalipa kwa wale wazoefu? au ushauri jamani. Nimejaribu kuingia mtandaoni nikaona machine za kusagia juice ila sina uzoefu nazo mwenye uzoefu na bei na wapi zinapatikana anijuze jamani. Asanteni sana.
 
Machine nilizoziona kwenye mtandao za kutengenezea juice ni hizi attached here. Kwa wale wazoefu, nisaideni ubora wake, matumizi, bei
na wapi nawezazipata. Natanguliza shukrani ndugu



 
Juice ina faida nzuri sana, kama utapata sehemu nzuri ya biashara na usafi wa hali ya juu,chemsha maji ya juice au nunua yale madumu makubwa ya Uhai.

kama upo Dar unaweza pata used maeneo ya Ilala karibia na club ya wazee kuna maduka ya vyombo used au magomeni mapipa.

Kama unataka mpya kuna duka lipo maeneo ya Gold star maeneo ya gerezani (utaona wameweka sanamu ya chef nje) wanauza vifaa vya hoteli na bakery zipo hapo mi nilinunua yangu hapo.
 
zavi unaweza kunifahamisha bei ya hizo mashine za juisi? Je Blender haiwezi kufaa?
 
Last edited by a moderator:

kuhusu soko hilo si la kuuliza, hata wanaotembeza mtaani watu wanakunywa bila kujua usalama wa maji yaliyotumika na processing nzima. kikubwa hapo mkuu ni location, uwe na sehem ambayo ni strategic...yenye mzunguko mzuri wa watu na mazingira safi.

Pia kuwa mbunifu sana, usiuze juisi pekee, uza pia na fruit salad, yoghurt, matunda fresh nk...kama mimi mpenzi wa papai nikiingia kwako nachagua papai unaliandaa natafuna kisha naenda zangu! ubunifu tu mkuu, fanya kitu tofauti kidogo na wengi.
 
Machine nilizoziona kwenye mtandao za kutengenezea juice ni hizi attached here. Kwa wale wazoefu, nisaideni ubora wake, matumizi, bei na wapi nawezazipata. Natanguliza shukrani ndugu

hiyo ni dispenser utahitaji blender nzuri na vyombo vinginbe kama glass na visevio vingine!
 

Asante sana ndugu yangu kwa mchanganuo huo, mie sipo Dar, nipo Shinyanga mjini. Ndo nataka nifanye hichi kitu. Usafi ni jambo muhimu sana katika uandaaji wa juice, ila ningefurahi kupata hizo machine. Nashukuru sana
 

Asante sana mkuu, nimependa ushauri wako. Tupo pamoja, ngoja nipambane
 
Asante sana ndugu yangu kwa mchanganuo huo, mie sipo Dar, nipo Shinyanga mjini. Ndo nataka nifanye hichi kitu. Usafi ni jambo muhimu sana katika uandaaji wa juice, ila ningefurahi kupata hizo machine. Nashukuru sana
Na mi nataka nifungue biashara ya hivyo hivyo hapa Shinyanga mjini... Upo sehemu gani?? Mi nipo Mwasele
 
Machine nilizoziona kwenye mtandao za kutengenezea juice ni hizi attached here. Kwa wale wazoefu, nisaideni ubora wake, matumizi, bei na wapi nawezazipata. Natanguliza shukrani ndugu

Hizo hazitengenezi juice, ni ka dispenser tu.

Ukishatengeneza juice ndo unaweka humo kwa ajili ya kumvutia mteja, pia kuhifadhia.
 
zavi unaweza kunifahamisha bei ya hizo mashine za juisi? Je Blender haiwezi kufaa?

Blender lazima uwe nayo kwaajili ya kusagia matunda, na hiyo uliyoionyesha kwenye picture ni dispenser kwaajili ya kuifadhia juice . na bei zake kuanzia laki 6 mpk 1....m inategemea na container zipo ngapi. lakini ukitembea unaweza pata chini ya hapo .
 
Last edited by a moderator:
Hizo hazitengenezi juice, ni ka dispenser tu.

Ukishatengeneza juice ndo unaweka humo kwa ajili ya kumvutia mteja, pia kuhifadhia.

OK. Nimekuelewa mkuu, asante sana kwa hiyo hata nikinunua hizo ni lazima ninunue na blender siyo? asante sana kwa ushauri ndugu
 

Acha kumtisha bhana, Wise Sister, unaweza kuzipata hizi na ile yenye ubora kabisa inayoweza kusaga/kukamua machungwa, matango, apple, mapeasi n.k ni kama shilingi 200,000 na ile ya kukamua machungwa, nanasi n.k ni shilingi 50,000.

Hii ya elfu 50 haihitaji umeme na unaweza kuitumia mahali popote. Hizo zote unatengeneza juice bila kuchanganya na maji. Mimi ninazo nyumbani kwa matumizi binafsi lakini pia zinafaa kwa biashara.

Ili kuepuka kuharibika kwa juice pale umeme unapokatika mara kwa mara, ni vyema ukahifadhi matunda kwenye friji kwani mteja akija unaweza kumkamulia juice ndani ya dakika 2 akapata kiasi anachohitaji.

Karibu.
 
Last edited by a moderator:
Asante sana ndugu yangu kwa ushauri na mawazo mazuri, ngoja nipambane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…