Kaka napita na haraka.
WEewe kichwa.
Hii biashara ukikomaa inalipa ile mbaya.Ninaposema kulipa ile mbaya kulingana na nature yake.
Nakushari kama upo Dar nenda pale Kariakoo,viu vyote hivyo vipo.
Maana hapa hata ukishauriwa ni kwamba aina zote ulizotaja hapo juu zina Size kulingana na ujazo wake.
Kwa kujazia hapo,nakushauri
-Tafuta mashine ya Juice ila ya Port mbili hadi tatu,ili iwe rahisi kuuza juice za aina zaidi ya moja.
-Najua hapo utahitaji Freezers
-Ongezea kwa kuuza Fresh fruites,usiuze zile za kiswahili sana za papai telee,matangao ya kutupia halafu unakoroga,huo ni uji sio Fruite. Uza ile ya vipande kwa mfumo wa packing na mfumo wa kula hapo hapo.Hii inalipa sana mkuu,Dar matunda mengi sana ila ndio mkoa wa watu wanoongoza kwa uvivu wa kujimenyea matunda wao wenyewe.
-Nakushauri katika biashara hii usiweke Juice za viwandani,kwanza ni kujaza Banda bila sababu,pili faida yake inaweza kuathiri mapato ya upande wa pili. Tambua kwamba kitu chochote unachoweka kwenye freezer au fridge lazima kupata baridi kitumie moto,na fridge au freezer hufanyakazi kulingana na idadi ya vitu vilivyomo ndani yake ili compressor iweze kuvuta umeme.Sasa biashara za faida ya shilingi 50 na zinahitaji umeme katika mfumo unaotaka kuanza wewe zitakugharimu bila kujua.
-Hakiisha fremu yako ya biashara isiwe kijiwe,watu wengie wenye kupenda kutumia kwenye mabanda hayo,huwa wanapenda kuona banda ni rafiki wa mteja na sio banda kama kijiwe cha kumnyima uhuru mteja.
-La zaidi,ukipata Mashine ya Ice cream na ukawa umepeta mafunzo ya utengenezaji wake basi hapo miguu juu.
Ila hesabu ya mashine hii ni ndefu sana,3.5 - 5m size ya kawaida outlets mbili
Nikumbuka lingine nitakuja