Yajue usiyoyafahamu kuhusu Vita ya Kagera

Yajue usiyoyafahamu kuhusu Vita ya Kagera

ila kutegemea Silaha na vipuri toka nchi zingine ni hatari sana na utumwa. Pia inaonekana hii vita imeelezwa vizuri zaidi na mabeberu kuliko hata waliopigana, kwanini?
 
Its a good story, but Im worried it is one sided. Ugandan may have a different story
 
Wakuu hapa nitawaletea matukio yote muhimu wakati wa vita hii ya Kagera. Sio kama mimi ndiye niliyeandika la hasha! Ninachokifanya mie ni kuwaletea hapa kutoka Gazeti la Mwananchi. Kaa nami upate uhondo huu.

Vita kati ya Tanzania na Uganda, au Vita ya Kagera ilidumu kwa miezi sita kuanzia Novemba 1978 hadi Aprili 1979. Vita hiyo ndiyo iliyouangusha utawala wa Idi Amin Dada uliodumu kwa muda wa miaka minane.

Idd Amin aliingia madarakani Jumatatu ya Januari 25, 1971 alipoiangusha serikali ya Dk Milton Obote na aliondoka Jumatano ya Aprili 11, 1979 wakati majeshi ya Tanzania na ya Uganda yaliposhirikiana kumuondoa.

Mgogoro wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Uganda ulianza Jumatatu ya Januari 25, 1971 baada ya Amin kuipindua Serikali ya Dk Obote. Muda mfupi baada ya hapo, Rais wa Tanzania alimpa Dk Obote hifadhi ya kisiasa. Akiwa Tanzania Dk Obote alianza mipango ya kurejea Uganda akitumia ardhi ya Tanzania.

Mambo mengi ambayo yangeweza kusababisha Vita ya Kagera yalikuwa yametendeka tangu Januari 1971 hadi Oktoba 1978, lakini kwa kipindi chote hicho hakuna vita iliyozuka.

Vita hiyo ilianza rasmi siku ileile ya maadhimisho ya Uhuru wa Uganda, yaani Jumatatu ya Oktoba 9, 1978 baada ya mwanajeshi mmoja wa Uganda kuvuka mpaka na kuingia Tanzania kupata kinywaji na kukutana na mpenzi wake ambaye alikuwa raia wa Tanzania.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la Uganda la Jumanne ya Oktoba 9, 2017, wakati mwanajeshi huyo akiwa mpakani upande wa Tanzania kwa starehe zake, alijikuta akipambana na wanausalama wa Tanzania.

Mwanajeshi huyo alikamatwa na kuwekwa rumande. Mapema asubuhi ya siku iliyofuata, aliachiwa aondoke. Kwa kudhani amedhalilishwa na wanausalama wa Tanzania, alikimbilia kambini kwake upande wa Uganda, akachukua bunduki na kurejea upande wa Tanzania kulipiza kisasi.

Alipofika umbali fulani kutoka kituo alichokuwa ameshikiliwa, alifyatua risasi kwa mbali. Askari wa zamu wa kituo hicho walilazimika kukimbia. Hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa.

Alipojisikia vizuri kwa kitendo hicho, aliamua kurejea kambini kwake upande wa Uganda na kumdanganya kamanda wa kikosi chake aliyejulikana kwa jina la Luteni Byansi kwamba alitekwa na askari wa Tanzania, lakini akapambana nao.

Bila kutafakari sana, Luteni Byansi alimpigia simu Kamanda wa Kikosi cha Malire (MMRR) kilichoko Lubiri mjini Kampala, Kanali Juma Ali Oka (alikuwa maarufu kama Juma Butabika).

Bila kuwajulisha maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Uganda (UPDF), Kanali Butabika aliviamuru vikosi vya jeshi vilivyokuwa Ziwa Victoria kwenda kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Luteni Byansi kuishambulia Tanzania.

“Nilikuwa kamanda wa kwanza wa vifaru kuingia Tanzania. Tuliamriwa kushambulia. Tulikaa Tanzania kwa wiki mbili kabla ya kuamriwa kuondoka na kurejea Uganda,” Luteni Muzamir Amule wa UPDF alimwambia mwandishi Faustine Mugabe wa Daily Monitor katika mahojiano aliyofanyiwa mwaka 2015 nchini Uganda.

Kwa maoni yake, Kanali Butabika aliingiza Uganda vita isiyo na ulazima wowote.

“Unawapelekaje vitani wanajeshi kutoka Malire (Kampala) hadi Mutukula (Tanzania) bila kumtaarifu Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama au hata kamanda yeyote wa juu wa jeshi?” anahoji Luteni Amule katika habari hiyo.

Ijumaa ya Oktoba 27, 1978, mara baada ya uamuzi wa Kanali Juma Butabika, zilitumwa ndege tatu za kivita aina ya ‘MiG-21’ (Mikoyan-Gurevich) za Kirusi. Marubani bora zaidi wa ndege hizo nchini Uganda, Luteni David Omita, Luteni Atiku na Luteni Abusala walichaguliwa kwa kazi hiyo maalumu.

Kumbukumbu nyingine zinaonyesha kulikuwa na rubani mwingine aliyeitwa Walugembe. Mwaka mmoja kabla, marubani hao watatu—Luteni Omita, Luteni Atiku na Luteni Abusala—walikuwa wamerejea kutoka mafunzoni nchini Urusi.

Uganda ilinunua ndege 20 za aina hiyo mwaka 1977 kuziba pengo la zile aina ya MiG-15 zilizoharibiwa Jumapili ya Julai 4, 1976, wakati makomandoo wa Israel walipoivamia Uganda katika shambulio linalojulikana kama Operation Entebbe.

Ndege hizo zilipaa kutoka Entebbe kwenda kuishambulia Tanzania. Ndani ya muda mfupi zikawa zimeshambulia na kurejea Uganda.

Zilipogeuka, ndege ya Luteni Omita ilipigwa kombora na wanajeshi wa Tanzania. Kombora hilo liliharibu bawa lake la kushoto na ikashika moto. Lakini kati ya sekundi chache kabla ya kushika moto, Luteni Omita alifanikiwa kuruka kwa parachuti.

Hadi wanajeshi wa Tanzania wanafika yalipokuwa mabaki ya ndege hiyo, rubani huyo alikuwa ameshatoweka.

Nchini Uganda, wanajeshi wenzake wakiamini kuwa Luteni Omita ameuawa na majeshi ya Tanzania, walimwona akirejea kambini kwa mguu. Baadaye alipelekwa Entebbe kukutana na Idi Amin ambaye alimpongeza kwa ujasiri wake.

Jumapili ya Oktoba 29, 1978, kwa mujibu wa matangazo ya kituo cha redio cha Voice of Uganda ya Oktoba 30, 1978, Idi Amin aliwapandisha vyeo Omita, Atiku, Abusala na Walugembe kuwa makanali na kuwafanyia tafrija.

Tafrija ya kuwapandisha vyeo ilifanyika mjini Entebbe kwenye Uwanja wa Ndege wa Jeshi.

Wakati Idi Amin akiwa katika sherehe hiyo, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilifanya shambulio lake la kwanza kabisa eneo la Kikagati ndani ya Uganda na kuingia kilometa kadhaa bila ya upinzani wowote.

Itaendelea kesho
Source Mwananchi la leo 10 Dec 2018
Wakorea vitu kama hivi wanavifanyia historical drama[emoji91] [emoji91] [emoji91] [emoji91] [emoji91]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo pia ni kuwa huyu mkuu ametoa kwenye gazeti la Mwananchi tu,lakini kwa mfumo m'baya wa uongozi aliokuwa nao Amin,sishangai kila mtu kujifanyia mambo alivyopenda,hasa wanajeshi wake wakiwa wanajua kuwa,tayari kulishakuwa na uhasama kati ya nchi yao na Tanzania.

Yasemekana kuwa,wasaidizi wake kadhaa Amin walijifanyia mambo ya kinyama na kiholela hata bila yeye kujua pia (au hata nae hakujali kabisa);Mfano Malyamungu,makamu wake Idris,mwanae Taban Amin.Hawa hawakuwa na subira kujifanyia watakayo.Hivyo sishangai kama kuna hao wengine pia walifanya waliyoona yafaa kwao binafsi hadi wakawa chanzo cha vita vya Kagera.

Amin,hasa kwa udogo wake wa akili,kukosa umakini na kupenda kusikiliza anayofurahia kusikia,angeweza kulishwa ujinga wowote na akaamini,ilimradi upo ndani ya mtizamo wa chuki na Tanzania.Hivyo,kamwe sishangai.Hiyo,ni licha ya kuwa kumbe hata yeye Amin alishatamka shari ya kushambulia Taznzania hata kabla ya hayo.

Na hata kama chanzo cha vita ilikuwa mtu au watu wengine ndani ya Uganda,bado yeye Amin kama kiongozi,hangeweza kukwepa wajibu wa vita kama kiongozi.Ni sawa na mzee Mwinyi alivyojiuzulu alipokuwa Waziri wa mambo ya ndani kama sikosei,yalipotokea mambo ndivyo sivyo kwa watu wa chini yake katika wizara aliyokuwa akiiongoza.

Ukisema "wanaopinga kukamatwa madini ni wasaliti vitani, na wasaliti vitani hupigwa risasi" halafu kweli watu wakapigwa risasi, machafuko yakatokea, huwezi kukwepa lawama kwamba wewe ndio mwanzilishi wa vita, wewe ndio umefanya dog whistling, umewapigia mbwa miruzi wafanye mashambulizi, watu wamefikwa maafa kwa vile wewe kiongozi ulishaonyesha nia na madhumuni ya kutaka watu wafikwe maafa. Hukwepi lawama.

Ndio ya Iddi Amini.

Ndio ya watawala wetu wengi Afrika.
 
Katika toleo lililopita tulisimulia namna majeshi ya Idi Amin yalivyoivamia Tanzania Jumatatu ya Oktoba 30, 1978 kupitia Kukunga, Masanya, Mutukula na Minziro na kuua raia na hatimaye kuteka eneo la kilomita za mraba 1,800 na kutangaza kuwa mpaka halali wa Tanzania ni Mto Kagera.

Habari za kutekwa kwa Kagera zilimfikia Rais wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere ambaye siku hiyo hiyo aliwaita makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) nyumbani kwake na kukubaliana kuwa kazi ya kumng’oa Idi Amin ianze mara moja.

Siku mbili baada ya kukutana na makamanda wa Jeshi la Wananchi Novemba mosi, 1978, Mwalimu Nyerere alilitangazia Taifa kuhusu “uvamizi wa Idi Amin na uamuzi wa Tanzania wa kumpiga”. Akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Mwalimu Nyerere alieleza uvamizi huo na jinsi Tanzania ilivyoamua kupambana na majeshi ya Idd Amin.

“Nimewaombeni mkusanyike tena hapa niwaelezeni jambo ambalo kwa sasa wote mnalijua. Lakini naona si vibaya nikieleza. Nitajaribu kueleza kwa ufupi.

“Wakati nilipokuwa ziarani Songea kuanzia juma la pili la mwezi uliopita (Oktoba), zilitangazwa habari kutoka Uganda kwamba jeshi la Tanzania limeingia Uganda na limechukua sehemu kubwa na kuua watu ovyo.

“Siku zilipotangazwa habari hizo nilikuwa nimekaribishwa chakula cha jioni na vijana wetu wa jeshi pale Songea, na nikakanusha. Na kwa kweli nikachukua nafasi hiyo kuvishutumu vyombo vya habari vya nje ambavyo vinapenda kutangazatangaza uongo wa Amin,” alisema Nyerere.

“Kila anapotangaza uongo, wao huurukia na kutangaza kama kwamba ni kweli. Huo ndio uliokuwa uongo wake wa kwanza, na aliendelea endelea.

“Baadaye akabadili sura, akaongeza uongo wa pili katika shabaha hiyohiyo kuwa Watanzania wanaua watu ovyo na kwamba wanasaidiwa na majeshi kutoka Cuba. Uongo huo nao tukaukanusha.

“Kwa hivyo, alivyozidi kusema habari hizo za uongo tuliendelea kuzikanusha na kuzipuuza. Lakini Alhamisi akatuma ndege za kivita Bukoba. Vijana wetu walizitupia risasi zikakimbia. Siku hiyohiyo ikarudi tena moja, ikaangushwa.

“Ijumaa zikaja ndege eneo la Kyaka. Zikatupa mabomu. Vijana wetu walizitupia risasi, na mbili zikaangushwa.”

Nyerere pia alizungumzia ndege za Tanzania zilizopotea uwanjani wakati zikitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza ambazo kutokana na kasi yake zilihisiwa kuwa ni za adui na kutunguliwa. Nyerere alisema Tanzania imechoshwa na uongo huo wa Idi Amin na hivyo wameamua zikionekana ndege za kivita, zitunguliwe.

“Kwa hiyo vijana wetu wamekwishaambiwa kuwa ndege za kivita zikionekana, zipigwe. Kama vile zile za Bukoba na Kyaka zilipigwa, basi na hizi zikapigwa zilipofika Musoma. Walidhani ni za adui. Tukapoteza ndege tatu,” alisema Nyerere.

“Lakini katika mambo ya vita ajali hutokea. Na vijana hawa walishaambiwa ndege zikionekana zipigwe. Wangeziacha? Wanajuaje ni za adui? Kwa hiyo ikatokea bahati hiyo mbaya.

“Matukio haya hatukuyatangaza. Hata kule kupigwa kwa ndege za Amin hatukutangaza. Hatukutangaza kwa sababu hatukutaka jambo lenyewe kulipa uzito mno. Tulisema akiendeleaendelea kuleta ndege zake, tutaendelea kuziangusha kila zinapokuja.

“Uwezo wa kuziangusha upo, na mwenyewe alijua uwezo upo. Ni vizuri akijua yeye. Tulijaribu. Tulikuwa tunaepuka kulipa uzito jambo lenyewe ambalo mwanzo wake ni uongo kabisa wa kuzua.”

Nyerere alisema jinsi Idd Amin alivyoendelea kuidanganya dunia na jinsi Tanzania ilivyomjibu hadi alipoamua kuvamia.

“Sasa Jumatatu ndiyo akaivamia nchi yetu. Akaingiza majeshi yake kwa nguvu, nguvu kubwa. Yakachukua sehemu kubwa. Yakaingia ndani mpaka Kyaka. Hii tukatangaza kwa sababu lilikuwa ni jambo la kweli na yeye kama kawaida yake akakana akasema haikutokea hivyo,” alisema Nyerere.

“Akaendelea kusema kwamba Watanzania ndio wako Uganda, ndio wamechukua sehemu ya Uganda. Akakana ukweli huo. Lakini tukawaeleza jamaa na mabalozi walioko Dar es Salaam kuwa huo ndio ukweli.

“Huyu mtu ameivamia nchi yetu. Sasa jana ametangaza mwenyewe kwamba ni kweli majeshi yake yameivamia nchi yetu na yamechukua sehemu hiyo ya Tanzania iliyoko kaskazini mwa Mto Kagera na kwamba tangu sasa, eti sehemu hiyo ni ya Uganda na itatawaliwa kijeshi kama Uganda inavyotawaliwa.”

Alisema kauli hiyo ya Idi Amin iliisaidia Tanzania kutangaza kutokea kwa uvamizi huo.

“Sasa hiyo ndiyo hali. Tufanye nini! Tunayo kazi moja tu. Watanzania sasa tunayo kazi moja tu—ni kumpiga,” alisema Mwalimu Nyerere.

“Uwezo wa kumpiga tunao. Sababu ya kumpiga tunayo, na nia ya kumpiga tunayo. Tunataka dunia ituelewe hivyo. Kwamba hatuna kazi nyingine.

“Na tunaomba marafiki zetu wanaotuomba maneno ya suluhu, waache maneno hayo. Kuchukua nchi ya watu wengine siyo kwamba majeshi yamekosea njia na kusema kuwa sasa sehemu hiyo umeichukua na kutangaza vita kwa nchi ile nyingine. Si sisi tuliofanya hivyo. Amefanya hivyo mwendawazimu.

“Na amefanya hivyo kwa jambo ambalo aliwahi kutangaza zamani. Aliwahi kusema zamani kidogo kuwa mpaka wa haki wa Uganda na Tanzania ni Mto Kagera, na kuwa siku moja atachukua sehemu hiyo. Ametimiza hivyo.”

Nyerere aliwaomba marafiki wa Tanzania kuielewa hali hiyo na kuisaidia katika kuyaondoa majeshi ya Uganda na kwamba wale waliokuwa wakitaka suluhu haitawezekana.

“Hatukupenda kufanya hivyo. Maadui zetu ni mabeberu, na kwa hivi sasa wako Kusini. Serikali ya Afrika, hata kama hatupendi matendo ya viongozi wao, hatuwahesabu kama adui wetu,” alisema Nyerere.

“Na kama Amin angekuwa amesema tu kwamba Tanzania ni adui wetu, sisi tungeendelea kumpuuza kama ni maneno hayo. Lakini kafanya kitendo cha uadui, hatuwezi.

“Ameingia Tanzania mwenyewe. Na mtu huyu ni mshenzi. Ameua watu wengi sana. Kwa hiyo nasema tuna kazi moja tu. Tutampiga. Vijana wetu wako mpakani sasa hivi. Wako kule. Wako kule na mapambano yanaendelea.

“Sasa hayo si mapambano ya TPDF peke yake, ni yetu wote. Kwa hiyo ninachowaombeni wananchi, hiyo kazi iliyoko mbele yetu muielewe.

“Pili, tuwasaidie vijana wetu. Kila mtu kwa mahali alipo. Tutaendelea na kila mapambano yanavyoendelea kueleza nini la kufanya na nani afanye nini.

“Tutaelezana wakati wote huo mpaka tumemuondoa huyu nyoka katika nyumba yetu. Na tunawaomba mtulie. Katika mambo haya ya vita, na hasa kama watu mlikuwa mmezoea amani mnaweza kubabaika sana.

“Msibabaike, tulieni. Fanyeni kazi kama kawaida. Lakini mjue vitendo hivyo kazi yake ni hiyo moja; kumpiga mshenzi huyu aliyekuja katika nchi yetu.”

Itaendelea kesho

Source Gazeti la Mwananchi la leo.

hizo ndege zilizotunguliwa ndo mijawapo
ilikuwa na mtoto wa nyerere ama??
 
Wakuu hapa nitawaletea matukio yote muhimu wakati wa vita hii ya Kagera. Sio kama mimi ndiye niliyeandika la hasha! Ninachokifanya mie ni kuwaletea hapa kutoka Gazeti la Mwananchi. Kaa nami upate uhondo huu.

Vita kati ya Tanzania na Uganda, au Vita ya Kagera ilidumu kwa miezi sita kuanzia Novemba 1978 hadi Aprili 1979. Vita hiyo ndiyo iliyouangusha utawala wa Idi Amin Dada uliodumu kwa muda wa miaka minane.

Idd Amin aliingia madarakani Jumatatu ya Januari 25, 1971 alipoiangusha serikali ya Dk Milton Obote na aliondoka Jumatano ya Aprili 11, 1979 wakati majeshi ya Tanzania na ya Uganda yaliposhirikiana kumuondoa.

Mgogoro wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Uganda ulianza Jumatatu ya Januari 25, 1971 baada ya Amin kuipindua Serikali ya Dk Obote. Muda mfupi baada ya hapo, Rais wa Tanzania alimpa Dk Obote hifadhi ya kisiasa. Akiwa Tanzania Dk Obote alianza mipango ya kurejea Uganda akitumia ardhi ya Tanzania.

Mambo mengi ambayo yangeweza kusababisha Vita ya Kagera yalikuwa yametendeka tangu Januari 1971 hadi Oktoba 1978, lakini kwa kipindi chote hicho hakuna vita iliyozuka.

Vita hiyo ilianza rasmi siku ileile ya maadhimisho ya Uhuru wa Uganda, yaani Jumatatu ya Oktoba 9, 1978 baada ya mwanajeshi mmoja wa Uganda kuvuka mpaka na kuingia Tanzania kupata kinywaji na kukutana na mpenzi wake ambaye alikuwa raia wa Tanzania.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la Uganda la Jumanne ya Oktoba 9, 2017, wakati mwanajeshi huyo akiwa mpakani upande wa Tanzania kwa starehe zake, alijikuta akipambana na wanausalama wa Tanzania.

Mwanajeshi huyo alikamatwa na kuwekwa rumande. Mapema asubuhi ya siku iliyofuata, aliachiwa aondoke. Kwa kudhani amedhalilishwa na wanausalama wa Tanzania, alikimbilia kambini kwake upande wa Uganda, akachukua bunduki na kurejea upande wa Tanzania kulipiza kisasi.

Alipofika umbali fulani kutoka kituo alichokuwa ameshikiliwa, alifyatua risasi kwa mbali. Askari wa zamu wa kituo hicho walilazimika kukimbia. Hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa.

Alipojisikia vizuri kwa kitendo hicho, aliamua kurejea kambini kwake upande wa Uganda na kumdanganya kamanda wa kikosi chake aliyejulikana kwa jina la Luteni Byansi kwamba alitekwa na askari wa Tanzania, lakini akapambana nao.

Bila kutafakari sana, Luteni Byansi alimpigia simu Kamanda wa Kikosi cha Malire (MMRR) kilichoko Lubiri mjini Kampala, Kanali Juma Ali Oka (alikuwa maarufu kama Juma Butabika).

Bila kuwajulisha maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Uganda (UPDF), Kanali Butabika aliviamuru vikosi vya jeshi vilivyokuwa Ziwa Victoria kwenda kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Luteni Byansi kuishambulia Tanzania.

“Nilikuwa kamanda wa kwanza wa vifaru kuingia Tanzania. Tuliamriwa kushambulia. Tulikaa Tanzania kwa wiki mbili kabla ya kuamriwa kuondoka na kurejea Uganda,” Luteni Muzamir Amule wa UPDF alimwambia mwandishi Faustine Mugabe wa Daily Monitor katika mahojiano aliyofanyiwa mwaka 2015 nchini Uganda.

Kwa maoni yake, Kanali Butabika aliingiza Uganda vita isiyo na ulazima wowote.

“Unawapelekaje vitani wanajeshi kutoka Malire (Kampala) hadi Mutukula (Tanzania) bila kumtaarifu Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama au hata kamanda yeyote wa juu wa jeshi?” anahoji Luteni Amule katika habari hiyo.

Ijumaa ya Oktoba 27, 1978, mara baada ya uamuzi wa Kanali Juma Butabika, zilitumwa ndege tatu za kivita aina ya ‘MiG-21’ (Mikoyan-Gurevich) za Kirusi. Marubani bora zaidi wa ndege hizo nchini Uganda, Luteni David Omita, Luteni Atiku na Luteni Abusala walichaguliwa kwa kazi hiyo maalumu.

Kumbukumbu nyingine zinaonyesha kulikuwa na rubani mwingine aliyeitwa Walugembe. Mwaka mmoja kabla, marubani hao watatu—Luteni Omita, Luteni Atiku na Luteni Abusala—walikuwa wamerejea kutoka mafunzoni nchini Urusi.

Uganda ilinunua ndege 20 za aina hiyo mwaka 1977 kuziba pengo la zile aina ya MiG-15 zilizoharibiwa Jumapili ya Julai 4, 1976, wakati makomandoo wa Israel walipoivamia Uganda katika shambulio linalojulikana kama Operation Entebbe.

Ndege hizo zilipaa kutoka Entebbe kwenda kuishambulia Tanzania. Ndani ya muda mfupi zikawa zimeshambulia na kurejea Uganda.

Zilipogeuka, ndege ya Luteni Omita ilipigwa kombora na wanajeshi wa Tanzania. Kombora hilo liliharibu bawa lake la kushoto na ikashika moto. Lakini kati ya sekundi chache kabla ya kushika moto, Luteni Omita alifanikiwa kuruka kwa parachuti.

Hadi wanajeshi wa Tanzania wanafika yalipokuwa mabaki ya ndege hiyo, rubani huyo alikuwa ameshatoweka.

Nchini Uganda, wanajeshi wenzake wakiamini kuwa Luteni Omita ameuawa na majeshi ya Tanzania, walimwona akirejea kambini kwa mguu. Baadaye alipelekwa Entebbe kukutana na Idi Amin ambaye alimpongeza kwa ujasiri wake.

Jumapili ya Oktoba 29, 1978, kwa mujibu wa matangazo ya kituo cha redio cha Voice of Uganda ya Oktoba 30, 1978, Idi Amin aliwapandisha vyeo Omita, Atiku, Abusala na Walugembe kuwa makanali na kuwafanyia tafrija.

Tafrija ya kuwapandisha vyeo ilifanyika mjini Entebbe kwenye Uwanja wa Ndege wa Jeshi.

Wakati Idi Amin akiwa katika sherehe hiyo, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilifanya shambulio lake la kwanza kabisa eneo la Kikagati ndani ya Uganda na kuingia kilometa kadhaa bila ya upinzani wowote.

Itaendelea kesho
Source Mwananchi la leo 10 Dec 2018
Kuna sehemu sikuielewa. Hapo aliposema kuwa maafisa wa jeshi ngazi za juu hawakuwa na taarifa akiwemo idd amin mwenyewe. Ila baada ya ndege vita kushambumbulia Tanzania idd amin akawapongeza na kuwapandisha vyeo. Aliwapandisha vyeo bila kujua wamefanya operation gani?
 
KABLA ya kupambazuka askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walianza kushambulia vilima vya Kikanda, Nsambya na Simba. Majeshi ya Idi Amin yalijua wanajeshi wa Tanzania wangeingia Uganda kushambulia, lakini hawakujua kwa hakika shambulio hilo lingefanyika lini na wapi na kwamba lingefanyika kutokea upande gani.

Kwa jinsi mashambulizi yalivyokuwa makali na ya kushtukiza, Redio Uganda ilitangaza kuwa Uganda imevamiwa na majeshi ya Tanzania na Cuba. Ingawa Cuba ilikanusha habari hizo, Idi Amin aliendelea kuzisisitiza kiasi kwamba jarida la To the point international liliandika, “Dikteta wa Uganda anapiga kelele”.

Kwa mujibu wa kitabu cha War in Uganda, usiku mmoja kabla ya kushambulia vilima vya Simba, baadhi ya makamanda wa brigedi walikutana kwa mazungumzo na kupata kinywaji. Kwa wakati wote huu, kila upande—Tanzania na Uganda—ulikuwa ukijaribu kunasa mawasiliano ya upande wa pili.

Baada ya kupata kinywaji, makamanda wa brigedi walirejea katika vituo vyao na kuanza kucheza kitimbi. Kwa mujibu wa kitabu hicho, makamanda hao walianza kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe kwa kutumia redio za upepo.

Mmoja akauliza, “Wacuba wameshakaa tayari upande wa kulia?” Halafu akajibiwa na askari mwingine: “Tayari afande.” Yule wa kwanza akauliza tena, “Waisraeli wameshajiweka tayari upande wa kushoto?” Halafu akajibiwa, “Wako tayari afande.” Kisha akaendelea, “Na je, Wamarekani nao wameshakaa tayari eneo la kati?” Akajibiwa, “Wako tayari afande.” Kisha akasema, “Haya. Twende kazi.”

Majeshi ya Idi Amin yalikuwa yanafuatilia mawasiliano hayo ya redio. Baada ya kusikia mawasiliano hayo, ndani ya dakika chache majeshi ya Uganda yakaanza kulikimbia eneo hilo mmoja baada ya mwingine.

Katika mawasiliano ambayo JWTZ iliyanasa kutoka Uganda walisikia kamanda wa vikosi vya eneo hilo akiwasiliana na makao makuu mjini Kampala akisema, “I see! Kweli wanakuja sasa.” Kisha sauti kutoka Kampala ikajibu, “Sawa. Wapigeni.” Kamanda aliyekuwa akiongea katika mawasiliano hayo alikuwa eneo la vita akiwasiliana na aliyepo makao makuu mjini Kampala. Alipoambiwa wapigeni, yeye akajibu, “Tubadilishane. Wewe njoo huku (vitani) na mimi nije huko (ofisini).”

Siku iliyofuata Idi Amin, kwa kuyaamini maneno ya makamanda wa brigedi waliotaja Wamarekani, Waisraeli na Wacuba, aliingia kwenye studio za Redio Uganda na kuanza kutangaza kuwa nchi yake imevamiwa na Watanzania, Waisraeli, Wacuba na Wamarekani.

Kusikia taarifa hizo, vyombo vya habari vya dunia vikashangazwa na madai ya Amin. Ingawa ilikuwa ni uongo kuwa kulikuwa na Wacuba, Waisraeli na Wamarekani walioivamia Uganda, ukweli ni kwamba Idi Amin alizipata habari hizo kutoka kwa wanajeshi wake ambao nao waliamini kile kitimbi kilichochezwa na makamanda wa JWTZ.

Ni kweli kwamba makamanda wa JWTZ ndio waliosema hayo, na hayo waliyoyasema yakanaswa na redio za mawasiliano za jeshi la Amin ambalo baada ya kuziamini walizipeleka kwa Amin ambaye naye aliziamini na kuitangazia dunia.

Lakini Meja Jenerali David Msuguri, ambaye kwa sasa ndiye alipokea kijiti kutoka kwa Brigedia Jenerali Tumainieli Kiwelu kushambulia majeshi ya Amin, alikemea kitendo cha makamanda hao. Hata hivyo kitimbi hicho kilifanikiwa sana kwa sababu kiliyatia kiwewe majeshi ya Amin.

Mashambulizi makali yakafanywa na JWTZ katika vilima vya Kikanda, Nsambya na Simba. Majeshi ya Idi Amin yalielemewa katika maeneo hayo. Mizinga mikubwa ya Tanzania ikavunja nguvu ya jeshi la Amin.

Upande wa Kaskazini mwa vilima ambako majeshi ya Amin yangeweza kupata mwanya wa kukimbia ulikuwa umezingirwa na brigedi za 201 na 208. Majeshi ya Amin hayakujua yalivyozingirwa.

Walishtukia tu wanashambuliwa na wakastaajabu zaidi kuwa hata walikokuwa wanakimbilia nako kulikuwa kumezingirwa na wapiganaji wa JWTZ. Katika shambulizi hilo moja la siku hiyo moja peke yake, kiasi cha wanajeshi 250 wa Idi Amin waliuawa.

Walipochunguza maeneo waliyoshambulia, makamanda wa Tanzania walitambua kuwa wenzao wa Uganda hawakujua namna ya kutumia vizuri maeneo yaliyoinuka kukabiliana na adui.

Katika kilima cha Nsambya, JWTZ ilikuta handaki moja na simu moja tu ya mawasiliano. Katika eneo la kilima cha Kikanda Watanzania walistaajabu sana walipogundua mizinga mikubwa ambayo makombora yake ndiyo yaliyokishambulia kikosi cha Luteni Kanali Salim Hassan Boma eneo la Mutukula, ilikuwa nyuma ya mlima badala ya juu ya mwinuko.

Wakati mapambano yakiendelea kwenye vilima hivyo, ndege za kivita za Amin zilijaribu kusaidia wanajeshi wake lakini bila mafanikio. Ndege hizo zilishindwa kuokoa jahazi kwa sababu kufikia wakati huo ndege nyingi za Uganda zilikuwa zimeshatunguliwa na JWTZ.

Tangu wapiganaji wa JWTZ walipovuka mpaka na kuingia ardhi ya Uganda Jumamosi ya Januari 20, 1979 na kuteka vilima vilivyotajwa hapo juu pamoja na kiwanja cha ndege za kijeshi cha Lukoma kilichoangukia mikononi mwa JWTZ Jumanne ya Februari 13, Tanzania ilikuwa imeshaangusha ndege 19 za Jeshi la Uganda.

Kilichoanza kumkatisha tamaa Idi Amin ni ile kasi ya Tanzania kuangusha ndege za jeshi lake. Kilichomtia kiwewe zaidi ni kasi ya kukamata silaha kutoka kwa majeshi yake. Baadhi ya marubani waliosikia ndege zao zilivyokuwa zikitunguliwa na majeshi ya Tanzania waliingiwa na kiwewe na hivyo wengine walitoroka kazini.

Kilichofanya Jeshi la Anga la Uganda lifikie katika hali mbaya kiasi hicho ni upungufu—na pengine ukosefu wa wataalamu, upungufu wa vipuri vya ndege na marubani wa ndege za kijeshi kukimbia.

Kwa hiyo wakati mji wa Masaka ukianguka mikononi mwa JWTZ tayari Jeshi la Anga la Idi Amin lilikaribia kuwa mahututi.

Hata hifadhi yake ya silaha nayo ilianza kuwa na mushkeli. Kwenye kilima cha Simba, JWTZ ilikamata vifaru sita.

Baadaye vifaru hivyo vilianza kutumiwa na jeshi la Tanzania. Silaha mbalimbali kuanzia bunduki za kawaida hadi mizinga mikubwa ilikamatwa eneo hilo.

Baada ya kukamilisha kazi ya kuteka vilima vya Kikanda, Nsambya na Simba sasa njia ikawa imesafishwa tayari kwa kuushambulia mji wa Masaka. Nini kilitokea?

Tukutane toleo lijalo
Handithi njoo Utamu kolea!!!!!!
 
Kuna sehemu sikuielewa. Hapo aliposema kuwa maafisa wa jeshi ngazi za juu hawakuwa na taarifa akiwemo idd amin mwenyewe. Ila baada ya ndege vita kushambumbulia Tanzania idd amin akawapongeza na kuwapandisha vyeo. Aliwapandisha vyeo bila kujua wamefanya operation gani?
Usiulizeulize hiyo ni Hadithi Bwana!!!!
 
Ninawaomba wahariri na wasimamizi wengine , hizi nyuzi za vita ya Kagera ,na wasifu wa Makamanda walipigana huko na maeneo mbalimbali Afrika ziwekwe pamoja ,yaani chini ya jina moja mfano "vita ya Kagera " au "mashujaa wetu" na iwekwe sticky thread hapo juu. Mtu akifungua humo ndani anakutana nyuzi mbalimbali mfano ile ya sherehe ya kuzaliwa Jenerali Musuguri, wasifu wa jenerali Walden,jenerali Kiwelu, Gen.Ramadhani Haji Fakhi,Kanali Mahfoudh nk.
 
Dah! Haijaendelea kwanini Leo nimesoma kitu...
 
Tanzania tulikua wachokozi, bila sisi kuwahifadhi waasi wa Uganda tungeepusha vita.
 
Masikini mleta uzi, sijui alifariki au alitekwa!!!
 
Back
Top Bottom