- Thread starter
- #61
Suala la Palestina ni tofauti sana na suala la makaburu wa SA. Unalingamisha embe na kitumbua.
Palestine ni ardhi ambayo imekaliwa na jamii kubwa tatu kwa miongo mingi, huku wayahudi wakiwa ndiyo jamii kubwa, mpaka wakati wa Ottoman. Wakati wa Otyoman empire ndipo Wayahudi wengi walielekea Ulaya, na hivyo kuifanya jamii ua Waarabu kuwa majority kqenye eneo la Palesrine.
Mwaka 1947, UN iliamua Palestine land ugawanywe maeneo mawili, eneo moja ambalo lilikuwa 60% ya eneo la Palestine, liunde Taofa la Israel; na 40% ikabakizwa kwa waarabu. Mgawanyo ulizingatia proportionality ya historical population. Kwa ujinga tu, waarabu wakagoma kwa madai kuwa Israel imepewa maeneo mazuri ya kilimo na uvuvi. Kwa kudanganywa na Iran, Misri na Syria, Waarabu wa Palestine wakaaminishwa kuwa nchi za kiarabu zitawasaidia hao waarabu wa Palestine kuwaua na kuwapoteza kabisa Wayahudi. Mambo yakawaendea kinyume. Mwaka 1948, wakapigwa na kupoteza 60% ya ile 40% waliyopewa. Mwaka 1956 wakajaribu tena, wakapigwa na kupoteza tena maeneo mengine. Mwaka 1967, wakaandaa vita kubwa zaidi, wakapigwa na kupoteza maeneo mengine mengi zaidi ikiwemo milima ya Golan, Gaza na Westbank. Kama siyo ujinga na ubinafsi wa nchi za kiarabu, sahizi waarabu wa Palestina, wangekuwa na nchi yao.
Hakuna aliyewapora haki, zaidi ya ujinga na ubinafsi yao. Waliikataa 40%, leo wanalilia mipaka irudi ya mwaka 1967, ambayo kiuhalisia ni kama 15% ya eneo walilokuwa wamepewa mwaka 1948.
Mwaka 1993, makubaliano yakafikiwa kuwa kuanzishwe Taifa la Palestine lakini kwa hatua. Kwanza wapewe mamlaka ya ndani, huku wakiangaliwa uadilifu na uaminifu wao maana waarabu hawaaminiki. Na hilo hata Gadafi aliwahi kulinena. Wakapewa mamlaka ya ndani, mara wakaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe, mara kwenda kujilipua ndani ya Israel, mara mashambukizi ya kushtukiza. Wakawa wameshindwa.
1. Badala kujikita kwenye mambo ya kufikirika ili kuhalalisha unachokitaka pitia historia hapa:
Israel Gaza war: History of the conflict explained
2. Zingatia palikuwa na option pia ya kuwapeleka Uganda mayahudi hawa kutokea Ulaya na kuwa si kweli kuwa majority walikuwa wao mashariki ya kati.
3. Kwamba Kwanini hili ni la ukombozi?
4. Haipo Siri kuwa Israel inayakalia maeneo ya wapalestina; Israel inalijua hilo, dunia inalijua hilo na hakuna asiyelijua hilo.
5. Iliyobakia leo Palestina imezungushiwa fensi na iko chini ya himaya ya Israeli.
6. Kila kinachotoka, kuingia au kinachoendelea Gaza au West Bank ni kwa hisani ya Israeli.
7. Kwani text book definition ya neno ukoloni ni nini ndugu?
8. Kwani definition text definition ya ukombozi dhidi ya mkoloni ni nini?
9. Kwani ANC, TANU, KANU, MPLA, ZANU PF, au yeyote dhidi ya mkoloni huwa anataka au alitaka nini?
10. HAMAS anapigania ardhi yake na kujitawala kama taifa huru - Palestina.
11. Palestina habagazwi na mataifa, UN na popote ije kuwa wewe ndugu?
12. Kuvitenganisha vita vya HAMAS na vyovyote vya ukombozi ni kutaka kujitoa ufahamu kulazimisha udini usipokuwamo!