Yale Mabango ya Barabarani Mama ametimiza mwaka huu mbona hayapo?

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Wakuu !

Nawasalimu kwa jina la JamiiForums, Where we dare to talk openly

Kama kichwa cha huu uzi kinavyonieleza hapo juu. Kumbe hawa Watendaji wa Serikali huwa wanaelewa sana yale maneno ambayo huwa yanazungumzwa na Viongozi wa Chadema majukwaani (Tundu Lissu na John Heche). Hawa jamaa wanaeleweka sana majukwaani na Wananchi huwa wanaunga mkono yale wanayoyazungumza.

Suala la Mabango ya Mama ametimiza wameyazungumzia sana majukwaani na Kimsingi yale mabango hayana tija wala faida kwa maisha ya Watanzania wote.

Tangu wameingia madarakani mwaka huu mwezi January wamezunguka mikoa mingi na yale waliyoyazungumza yameeleweka vyema akilini mwa watu wote 😂😂😂

Naona mwaka huu mpaka mwezi June yale mabango hayapo tena barabarani nadhani ni kwa sababu ya kelele zilizopigwa na hawa Makamanda.

Wakuu hebu tujiulize kwa nchi kama Tanzania inayomtegemea Mzungu katika kujiendesha yale mabango yana umuhimu gani? Mabango nchi nzima yanasifia tu. Halafu Mimi mwenyewe yale mabango huwa najua kutengeneza. Bango la 150cm*90cm gharama yake sio chini ya shilingi 350,000. Na kama ninavyojua serikalini kitu chenye thamani ya 200,000 utaambiwa uandike 500,000. Nimefanya kazi nyingi za Serikali na hilo nina ushahidi nalo.

Unatengeneza Computer za ofisi ya Serikali vifaa kama ram, processor, hard disk utaambiwa andika mara tatu zaidi ya gharama halisi. Hapa mtaona ni namna gani kulivyo na upigaji. Sasa kwenye haya mabango nchi nzima ni fedha kiasi gani zinateketea pasipo na ulazima?

Hoja yangu ni kwamba, Nchi yetu imekosa viongozi wenye huruma na utu na wamekuwa wabinafsi na wanaangalia maisha yao tu.

Nchi ambayo
1. Wanafunzi wa chuo wanasomeshwa na Serikali kwa mikopo yenye riba wakimaliza masomo wanarudi mitaani kuwa madereva bodaboda, maafisa ubashiri, Wadangaji, vibaka na wapiga debe nk
2. Nchi ambayo watu hawana uhakika wa lishe bora achana na milo mitatu. Maana kwa sasa mwananchi anakula mihogo saa 5 asubuhi baada ya hapo ni kunywa maji mpaka jioni atafute tembele na Unga Robo.
3. Nchi ambayo upatikanaji wa huduma za afya ni duni
4. Nchi ambayo miundombinu ya barabara ni mibovu kupindukia. Ikinyesha mvua kubwa mikoani Dar es Salaam nyanya, vitunguu, viazi vinaadimika na vinapanda bei Kisa magari yamekwama kuleta bidhaa kwa sababu mvua zimeharibu barabara.
5. Nchi ambayo ukienda serikali ya mtaa kupata huduma bila shilingi 2,000 hupati huduma
6. Nchi ambayo ukiamka asubuhi unakuta vocha imepanda bei vocha ya sh 10, 000 utaambiwa sh 1,100 😏
7. Nchi ambayo Chawa amemfisia Kiongozi wa nchi anaanza kuwananga na kuwatukana Wanafunzi wa vyuo hawana hela 😫
8. Nchi ambayo jiji la biashara la Dar es Salaam Huduma za usafiri wa Umma zipo chini ya kiwango.
9. Nchi ambayo ukiongea lugha tofauti na Chama Dora maisha yako yanakuwa hatarini kama digidigi
10. Nchi ambayo haki yako ya kupata huduma za kibinadamu kuzipata ni ngumu na ukitaka kuzipata uwe tayari kutoa sana rushwa (Namba ya Nida, Cheti cha kuzaliwa, Pasipoti ya kusafiria)
11. Nchi ambayo huduma ya maji safi na salama ni ya kusuasua.

Yapo mengi sana Wakuu, halafu sasa hapo unakutana na Mabango barabarani yaliyojaa kila aina maneno ya sifa njema ambazo hata Malaika hawana ( Unafiki na Uongo ni mbaya sana). Naamini hili suala la mabango ya Mama ametimiza mwaka huu limesitishwa kutokana na Kelele za Viongozi wa CHADEMA (Tundu Lissu na John Heche) Pongezi nyingi ziende kwao. Mungu aendelee kuwapa nguvu na siha njema waendelee kuwafumbua watu akili na fahamu zao. Pamoja na figisu na changamoto wanazozipitia.

Ushauri kwa Viongozi wa Serikali na taasisi za Umma, hii bado inahitaji kujengwa na kila Mtanzania kwa moyo wote, akili zote na nguvu. Uongo, Hadaa na sifa za kubandika mabango yenye sifa zisizo na uhalisia hazina tija. Tukubali sisi bado tunajitafuta na Maendeleo yanayoonekana ni kodi za kila Mtanzania iwe ni direct or indirect tax.

Kwa Pamoja Tuijenga nchi yetu, Unafiki, sifa za kijinga na Uchawa hazina faida kwa Taifa letu.

Nawasilisha.
 
Halafu wakiyaweka tena malalamiko yataanza
 
Tuko tunaprint ya October
 
Back
Top Bottom