Yale matamko ya Ubalozi wa Marekani kuhusu COVID-19 nchini yameishia wapi?

Nani alikataa kuwa hauko? Rais JPM ameliweka wazi tutaishi nao kama magonjwa mengine mfano mafua, malaria, nk. Wale walio uzindua ugonjwa huu walitumia mbinu ýa kuingiza dunia nzima katika hofu...
Una point juu ya Covid19 na nchi kukataa ushoga, lakini mengine ni mawazo yako yasiyo na tija.
 
Mungu ni mwema sana katika nchi yetu ya Tz.
Ametenda na atazidi kutenda hata kwa yale ambayo hatujui.
Ninakubaliana na maoni yako!

Kwa tunaoamini uwepo wa Mwenyezi Mungu tunaweza kusema kuna muujiza umetendeka nchini!
 
Kwa mtu anayechanganua masuala kwa undani utagundua kuwa matamko ya Ubalozi wa Marekani kuhusu kile walichokuwa wanakiita ''Hali mbaya ya maambukizo nchini'' kimepotea baada ya tamko lao la mwisho la mwezi Mei 2020..
We unasema marekani, mbona humsemi kigogo aliyefia kutangaza vifo vya ajali za gari ni corona, mpaka kaikimbia akaunti yake kaja na nyingine siku hizi.

Marekani ilikuja kugundua yule balozi mwanamke ni mliberali, wakamfurusha, balozi m republic alipokuja, kasafisha kabisa kuwa Tanzania ni salama na yeye aliingia ikulu bila barakoa
 
Nashukuru kwa kunijulisha mengine ambayo sikuyajua!

Siasa zina mambo mengi sana ambayo yamejificha!
 
Mpiga zumari wao wa Corona Lissu kasahau kazi aliyotumwa ya kueneza uongo na uvumi kuhusu corona anatafuta wadhamini nchi nzima akiwa havai hata hiyo barakoa. USA, Lissu na WHO wameaibika sana kuhusu corona Tanzania.
Sasa wakimuona katikati ya watu akiwa hajavaa chochotr si anawapa wakati mguu jamaa zake?
 
Lakini yeye havai barakoa ingawaje anakutana na umati wa watu wasiofaa barakoa 🙂
Huo unaofanyika ni usanii wa kisiasa!

Jamaa anachohubiri nje ya nchi ni tofauti na anachokifanya!
 
Alishajinasibisha ye ni mkenya kabisa. So ni balozi kivuli wa kenya tanzania anayepambania urais wa tanzania.
Wanasiasa wa Kenya wanamtumia tu ili kuonyesha wananchi wao kuwa njia waliyoitumia ni bora kuliko iliyotumiwa na serikali ya Tanzania!
 
Sasa wakimuona katikati ya watu akiwa hajavaa chochotr si anawapa wakati mguu jamaa zake?
Hawezi kuendelea kupambana na ukweli!

Ukweli ni kuwa Watanzania wengi wanakubaliana na njia iliyotumiwa na serikali katika mapambano ya Corona
 
Haikuwepo ila tuliahidi kuwalinda watanzania . Na tumetekeleza ikiwemo kwenye corona.
Huyo jamaa hajui kuwa kazi ya msingi kwa Rais ni ulinzi wa raia na mali za nchi!
 
Mchawi wa matamko alikuwa ni Kaimu Balozi wa Marekani

Kuondolewa kwa kale kaBetina na "shogaake" balozi wa UK ndo kupotea kwa yale matamko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…