Yalihamishwa makaburi na miili ndani, sembuse hawa Wamasai hai na nguvu zao

Yalihamishwa makaburi na miili ndani, sembuse hawa Wamasai hai na nguvu zao

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Binadamu tunapenda mno kulalamika, haswa sisi tunaojulikana kama raia wa nchi ya Tanzania. Huwa hatuna dogo hata siku moja ni mwendo wa malalamiko.

Zipo video zinazozunguka mitandaoni zikiwaonyesha wamasai wakihama kwa ridhaa yao wakielekea makao mapya huko Handeni. Wamejengewa nyumba na nadhani umeme na maji sio tatizo kwa wakati huu.

Kuna siasa nyingi nyuma ya suala hili la Ngorongoro, jamaa wa kimasai wamekubali kutumika baadhi yao, wakidai kuwa tayari kufa huku wakilinda rasilimali waliyorithi kutoka kwa wazazi wao miaka mingi iliyopita.

Wameikuta serikali ya awamu ya sita ikiwa na uwezo mkubwa wa kujenga hoja zenye sura ya kibinadamu, huko mitandaoni wakaonekana wanaharakati wa Kenya wakiishambulia serikali na mipango yake.

Hakuna aliyekurupuka kujibu tuhuma zao, wakitaka kuichafua taswira serikali ionekane hakuna la maana inalolifanya, wastaarabu hawajainua midomo na kujibu hizi tuhuma, humility at its level best.

Wakati sakata hili la Loliondo likiendelea nikakumbuka miaka ile ya nyuma wakati serikali ikitaka kujenga kipande cha barabara kutoka Chang'ombe kukatiza Ilala na kuja kutokea Msimbazi Centre mpaka Kigogo. Namna ambavyo ilibidi makaburi yaliyokuwa pembeni ya uwanja wa Karume yabomolewe na miili ya waliolala pale iweze kuhamishwa.

Zoezi lilifanyika licha ya kuwepo upingaji kutoka kwa wanaharakati kama hawa wa Loliondo, likamalizika na barabara ile ikajengwa. Leo hii imekuwa ni njia nzuri na ya muhimu kwa jiji la Dar kiasi ambacho makutano ya Pugu Road na njia ile ya Chang'ombe imebidi pajengwe fly over inayoelekea kukamilika.

Kama serikali iliweza kuhamisha miili ya jamaa zetu waliokwisha kulala usingizi wa milele, hawa wamasai walio hai itashindikana vipi kuwahamisha kwa ajili ya kulitunza eneo la Ngorongoro?. Kuna vita za kiuchumi kati yetu na majirani wa kaskazini ingawa viongozi wakuu kabisa kila wanapokutana hujenga hoja kana kwamba kila kitu kipo salama na amani inataradadi.

SSH na serikali yake wamekwenda kisayansi zaidi, kwa kuitangaza nchi kimataifa, wametafuta mtazamo chanya wa kidunia (positive image).

Wameweza kuitangaza dunia na imeweza kuujua upande mzuri wa Tanzania na hili ni lazima liwe ni donge linalowakereketa majirani wa kaskazini. Yale mambo ya kutuchukulia kama vile sisi ni mafala tusio na uelewa mpana wa dunia, yanakwenda kufika mwishoni.

Suala la Ngorongoro limenikumbusha miaka ile ya ujenzi wa barabara ya Ilala, ikabidi miili ya jamaa zetu ihamishwe. Muwe na siku njema wapendwa.
 
Mimi nashauri serikali isimamie inachokiamini. Hao wamasai wahamishwe kwa kuwa kama fidia wanalipwa, nyumba wanajengewa, eneo lingine la malisho wamepewa na kubwa zaidi usafiri wamepewa bure.

Serikali imetimiza wajibu wake vzuri hivyo wamasai nao watimize wajibu wao.

Wanaharakati wanaowasikiliza wanakula fedha nyuma ya mgongo wao
 
Wa kumlaumu ni Nyerere aliyeanzisha mfumo wa kuhamisha watu enzi za vijiji vya Ujamaa. Huo mfumo umebaki mpaka leo.
 
Back
Top Bottom