Yaliojiari Pasaka hii na matukio yasiokuwa ya kawaida..

sosoliso

Platinum Member
Joined
May 6, 2009
Posts
8,543
Reaction score
9,480
Nadhani wote humu mko wazima na makini (wenyewe wanasema gado)..
Yametokea matukio kadhaa kwenye wakati wa sikukuu hii ya Pasaka.. Kuna mengine ambayo yalinilazimisha kuyaundia tume ili kufahamu ukweli na mengine ambayo ni ya kupeana habari..

Ninaomba
Erickb52 na YNNAH mtoe ripoti ya mlioyagundua katika uchunguzi wenu dhidi ya sifa zilizotolewa na Bishanga kwa manoah.. Jee zilikuwa ni sifa za ukweli na dhati au alikuwa anamng'ong'a mwenzie na kumzunguka kwa mai waifu wake mimisa..?
Bujibuji alipata maswahibu ya gari yake kufunikwa na kifusi cha mchanga wa ghorofa lililodondoka majuzi pale Indira Gandhi/Morogoro street.. Na sasa ameamua kwenda kumnyang'anya mamsapu wake kile kimgongo wa chura alichomuhonga.. (sosi manoah)..

Arushaone
hajaonekana toka Alhamisi.. Haijulikani alipo na habari zimepelekwa mpaka Polisi..
saudari alikamatwa na mkia wa fisi (ambao ni nyara ya serikali) na mpaka sasa anashikiliwa katika kituo kidogo cha polisi pale mabatini..
Safari_ni_Safari alimtishia maisha babu Asprin.. babu akamuahidi atakiona kilichomtoa kanga manyoya.. Safari_ni_Safari ameingia mitini.. Babu Asprin naomba utoe tishio dhidi yake ili arudi nyumbani kwake.. ametubu..
The secretary alijigeuza yeye ni mwalimu wa baioloji na kung'ang'ania kwenye pointi ya riprodaksheni.. Hili lilileta athari kwa wengi..
Arabela hakueleweka kabisa sikukuu hii.. naona alikuwa anammendea sana mwenyekiti wa tume ya Erickb52 na akadiriki hata kubisha hadharani.. wakati huo huo akawa anafliti na babu Asprin..
Passion Lady nae hakueleweka kabisa kwenye kipindi hiki cha sikukuu..
YNNAH nategemea kazi nzuri imefanyika na ninasubiri ripoti ambayo nitaiweka hadharani..

Mwisho.. Mwenyekiti wa mahusiano
Baba V hajaonekana kabisa katika kipindi hiki.. Kuna yeyote mwenye habari zake..?

Its
sosoliso & Paloma..


 
sosoliso mbona hujasema ya Paloma wako, hujui ndo anahusika na kumshawishi JK kuwaita Ikulu wale wajeda?
 
Last edited by a moderator:
Mshaaanza maneno yenu, ntaenda kuwasomea kama ile niliyomsomea Kaka Alfani, Kuva na Mchana Mwema, sasa ile ilikua cha mtoto ndio maana hawajaondoka....sasa ntakayowasomea nyie LAZIMA muondoke tu......nimeuza vijitwiga viwili tu, kenge kumi na viji-nyati ishirini mkaanza maneno, nimeuza kale ka-eroplane kwa dola mia tano tu kama chuma chakavu bado maneno hayaishiiii, jamani nyie
Baby sosoliso umesahau kashfa inayomhusisha Elli kule kulikoporomoka machimbo ya kokoto arusha.....!
 
Last edited by a moderator:
Nawatakieni maandalizi mema ya Pasaka na kheri katika kipindi chote cha Ijumaa kuu na Pasaka kwa ujumla.
 
usitake kunambia zile vitu walikuchanganyia kina sosoliso zinaanza kufanya kazi!..nakuambiaga kila siku my manoah awa watu kaa nao kwa kujilinda
Nawatakieni maandalizi mema ya Pasaka na kheri katika kipindi chote cha Ijumaa kuu na Pasaka kwa ujumla.
 
Last edited by a moderator:

mkuu njoo tu, mimi ndie mtaalamu wa kusoma ile mambo walio msomea baba mwanaisha... jua la jioni hawalioni!!
 
Ona unavobabaika! Unaanza kujiorodheshea mwenyewe! Lols! Utawajua tu kwa magamba yao!
 
Mkuu wa itifaki...wrong...iti-nini cjui.... Ntakutafuta umsomee na Asprin...kazidi mno jamani!
mkuu njoo tu, mimi ndie mtaalamu wa kusoma ile mambo walio msomea baba mwanaisha... jua la jioni hawalioni!!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…