Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu 22 Septemba 2014, Uwasilishaji wa Rasimu ya Tatu ya Katiba Mpya

Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu 22 Septemba 2014, Uwasilishaji wa Rasimu ya Tatu ya Katiba Mpya

Wadau, nipo ndani ya ukumbi wa bunge na kuna dalili zote leo Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi Andrew Chenge hatawasilisha Rasimu hiyo. Hii ni kutokana na kazi ya kuandaa rasimu hiyo kutokamilika. Tayari Mwenyekiti wa Bunge Maalum Sammuel Sitta amewasili kwenye viunga vya bunge

mkuu weka hii post kama update kwenye thred, ie click edit pale kwenye thred ili kuwe na mtiririko mzuri...pamoja sana
 
Mabadiliko yanayofanyika yanahusu kanuni za 36 hadi 39 zinazohusu upigaji kura. Amon anasema kuwa kanuni hizo zilirekebishwa zitawezesha wabunge walio nje ya ukumbi wa bunge kupiga kura popote walipo. Kuhusu kanuni ya 36, mabadiliko yanafanyika ambapo badala ya kupiga kura kwa kila ibara kwa wabunge wote, sasa wabunge watapigia kura sura husika. Amon anasema kuwa mbunhe ataeleza wakati wa kupiga kura ibara anazokubali na sile asizokubali. Hali hiyo itaokoa muda na hivyo zoezi hilo kufanyika kwa muda mfupi.

Nadhani ni mabadiliko mazuri ili kuokoa muda
 
Pia kura zitapigwa kwa ibara,fuatilia bunge la katiba; kweli gratuity ya 150,000,000/= jamaa kapania kuipata
 
Kuhusu haki ya kupiga kura kwa wabunge, kanuni ilivyo hivi sasa inatoa fursa ya mbunge aliye ndani ya ukumbi wa bunge pekee.mhali hii inamnyima fursa mbunge aliye nje ya ukumbi wa bunge kwa ruhusa ya mwenyekiti kupiga kura. Marekebisho yanayokusudiwa, yatawezesha wabunge walio nje ya bunge kupiga kura kwa njia ya mtandao na simu. Hivyo, Ibara ya 36 inafutwa na kuandikwa upya, pia kanuni ya 38 itaongezwa ibara ili kukidhi matakwa hayo. Anasema kuwa jedwali la marekebisho limegawiwa kwa wajumbe
 
Najiuliza sana wamesema walivyoweka kanuni kwamba rais hawezi kuvunja bunge kwamba wote ukawa waliweka hiyo sheria sasa hawa kwann wanataka kuvunja sheria iliyowekwa nyuma kwamba wawaruhusu watu walio nje wapge kula na je wale walio nje kama wa ccm je hela wanapata au hawapati maana hauwezi kumbembeleza mtu kufanya mtihan wakati hajasoma wale walio njee hawajui kitu kuhusu ndan
 
badilisha heading kwanza...sitta hana mamlaka ya kubadili kanuni, hiyo ni mandate ya bunge
 
Naam, tunataka Katiba, wanaoandamana wao waendelee tu kuutafuta umaarufu.
 
Wameahirisha toka jana, katibu wa bunge alitoa ratiba hadi tar 24/09/2014 kwenye vyombo vya habari.
 
Ni dalili za kufeli.....................ukishaona kila sehemu munabadilisha mara sheria mara kanuni...................ujue hakuna kitu hapo......................!!!
 
Mwalimu Oluoch anakuwa mchangiaji wa kwanza. Anasema kuwa yeye haungi mkono hoja ya wajumbe walio nje ya bunge kupiga kura. Anasema kuwa hiyo nimkinyume cha sheria. Aoaonesha wasiwasi kama wabunge wanaoenda Hija wanaweza kupata muda wa kupiga kura. Hata hivyo Mwenyekiti anamsahihisha kuwa anachoongea Oluoch ni sheria ya uchaguzi ambayo haina uhusiano na hii ya bunge maalum la Katiba. Pia anamsahihisha kuwa kanuni hiyo haijawahusu wanaoenda hija tu bali kwa wale wote watakaokuwa nje ya bunge kwa sababu mbalimbali.
 
Samweli Sita leo anaongozq bunge la Katiba kubadili kanuni za bunge ili hata kama mjumbe yuko nje ya nchi apige kura hii maana yake ni kwamba si lazima mjumbe ahudhurie vikao vya bunge anaweza kukaa nyumbani ana tuma sms ,
 
Mkuu Chabruma hapo hakuna historia yoyote inayoandikwa, hiyo ni ile katiba ya ccm, wananchi RASIMU yetu ilisitishwa kujadiliwa bungeni TRH 16.4.2014. Na Kazi kukusanywa maoni ya wananchi haikuwa jukumu la Sita bali Jaji Joseph Sinde Warioba.
 
Seleman Jafu naye anachangia. Anasema kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilikuwa na mapungufu mengi. Hata hivyo anashukuru kuwa sheria hiyo imetoa fursa ya kutunga kanuni kwa kadri itakavyokuwa. Anakubaliana na mapendekezo ya kubadili kanuni badala ya kuongeza muda ambao kimsingi anasema kuwa ni kuvunja kanuni
 
Mkuu Chabruma hapo hakuna historia yoyote inayoandikwa, hiyo ni ile katiba ya ccm, wananchi RASIMU yetu ilisitishwa kujadiliwa bungeni TRH 16.4.2014. Na Kazi kukusanywa maoni ya wananchi haikuwa jukumu la Sita bali Jaji Joseph Sinde Warioba.
Mkuu, historia ni historia tu. haijalishi inawekwa na nani. Unajua hata wale wanariadha wanatengeneza rekodi ambazo zinabaki kwenye kumbukumbu
 
Paul Makonda anachangia sasa. Anashukuru Kamati ya Kanuni kwa kuleta mabadiliko hayo ambayo anayaona ni ya lazima. Anasema kuwa si rahisi wananchi wengi watu zaidi ya 600 kuwepo mahala pamoja kwa wakati mmoja. Anasema kuwa kinachofanyika si kuokoteza kura. Kura hazitawahusu wale ambao hawakushiriki kwenye mijadala. Anamshauri Oluoch kuwa ubunge hautafutwi kwa njia ya uongo bali kwa kusema ukweli. Hata hivyo Oluoch anatoa taarifa kuwa hajawahi kutangaza kuwa anataka ubunge na kwa taarifa hii anatangaza kuwa hana nia ya kugombea ubunge sehemu yoyote. Hata hivyo, Makonda anasema kuwa yeye na Oluoch wapo kwenye kamati moja na kwamba alimdokeza kuwa anataka kugombea ubunge. Hivyo kama leo Oluoch anakana, yeye anamshukuru Oluoch kwa kuwa muwazi

Aidha, Makonda anawashangaa wale wanaotishia kuandamana eti kushinikiza bunge lisiendelee. Anawashangaa vijana kutumika na wanasiasa kwa sababu zisizo na Msingi. Anamshangaa Mbowe kuchochea maandamano ilhali yeye yupo South Africa akilala kwenye Hotel yenye hadhi ya juu ambayo analipa Dola 700 kwa siku. Anasema kuwa katiba hii ina mambo mengi mazuri ambayo hayakupiganiwa na wabunge wa upinzani ikiwa ni pamoja na uwepo wa baraza la vijana, haki za wakulima, wafugaji, wavuvi nk
 
Mkuu, historia ni historia tu. haijalishi inawekwa na nani. Unajua hata wale wanariadha wanatengeneza rekodi ambazo zinabaki kwenye kumbukumbu

Mkuu ni kweli historia ni historia, maana hata tunakumbuka leo historia mbaya ya Hitler na wengineo.

Je ni kweli kabisa Rasimu hiyo ya tatu ni ya wataz?
 
Mkuu ni kweli historia ni historia, maana hata tunakumbuka leo historia mbaya ya Hitler na wengineo.

Je ni kweli kabisa Rasimu hiyo ya tatu ni ya wataz?
Ni ya Watanzania wote kutokana namkukidhi matakwa ya kisheria na utashi wa kisiasa
 
Ingekuwa inawezekana, wangebadili hizo kanuni haraka ili hili Bunge lisilo na maana kwa Taifa liishe hata leo. Maana likiisha hata siku moja tu kabla, tutakuwa tumeokoa milioni 150 ambazo zinaweza kufanya jambo la maana kuliko kutumika na hawa waharibifu.

Kuna tatizo gani kama sheria zinaruhusu.
 
Back
Top Bottom