Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu 22 Septemba 2014, Uwasilishaji wa Rasimu ya Tatu ya Katiba Mpya

Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu 22 Septemba 2014, Uwasilishaji wa Rasimu ya Tatu ya Katiba Mpya

Jamani muogopeni mungu hija ni ibada takatifu.msiwapelekee hizo kura za kimagumash.wataharibu hija zao.
 
la kwanza ni lile la twiga kupanda ndege bila kuonekana na sasa lingine la pili ni kipiga kura kokote duniani wakati hata uraia wa inchi mbili hawataki hii ndo tanzania yetu ya amani
 
Nimeangalia bunge hapa Nimeona samwel sita ametambulisha Wageni hapa Ambao ni wasanii anasema ni wasanii Zaidi ya hamsini Wageni wa Paul makonda najiuliza huyu hizi gharama nani anamgharamikia
 
Jamani muogopeni mungu hija ni ibada takatifu.msiwapelekee hizo kura za kimagumash.wataharibu hija zao.
Ufafanuzi umeshatolewa na sheikh Jongo. Anasema kuwa wakati wa hija watu wanapata fursa yamkutosha hali ambayo inaweza pia kuwaruhusu kupiga hija. Ametaja siku ambazo mahujaji wanakuwa busy namkwa mwaka huu inaweza kuanzia tarehe 4 Oktoba siku ambayo zoezi la upigaji kura litakuwa limemalizika
 
Ni bunge na Pwagu na Pwaguzi hilo,, Hiyo kamati ya uandishi inaandika nini? maana kuna vipengele vingi tuu hawajakubaliana na havikuamuliwa kwa kura sasa kamati ya uandishi inaandika maoni yote au inaandika nini haswa??
 
Ni bunge na Pwagu na Pwaguzi hilo,, Hiyo kamati ya uandishi inaandika nini? maana kuna vipengele vingi tuu hawajakubaliana na havikuamuliwa kwa kura sasa kamati ya uandishi inaandika maoni yote au inaandika nini haswa??

Bunge la samweli sita lina maajabu ya 8 ya dunia, wacha wajiandikie maana hata viongozi wa tz wanaongoza maiti (kwa mujibu wa Museven)
 
Bunge la samweli sita lina maajabu ya 8 ya dunia, wacha wajiandikie maana hata viongozi wa tz wanaongoza maiti (kwa mujibu wa Museven)
Mkuu, wabunge waliobaki bungeni wapo makini sana. Hakika wana dhamira njema kwa watanzania kwa vile na wao ni sehemu ya raia wa Tanzania
 
Mkuu,mujue pia hakuna mtu anayehitaji huu upuuzi wako. Kama unaona kuwa hutaki kusikia mjadala huu, kaa pembeni. Waache wahitaji wajue kinachojiri

Mkuu mimi ni mnazi wa JF.
Siwezi kuvumilia kuona watu wanatumia JF ku promote uhuni.
Ni hilo Mkuu na utaniwia radhi
 
Nipo hapa hapa jf ila nasita kuchangia uzi wako ili kukupa haki ya kufikisha kile ukionacho huko bungeni.
Nashukuru sana Mkuu. Tuvumiliane Mkuu. Ni upepo tu huu
 
Kwa kweli leo Mr. 6 kaonyesha uwezo na weledi wa hali ya juu katika kuendesha bunge.
 
Mkuu, wabunge waliobaki bungeni wapo makini sana. Hakika wana dhamira njema kwa watanzania kwa vile na wao ni sehemu ya raia wa Tanzania

Nimeheshimu maoni yako kwa kuwa unayo haki kikatiba kutoa maoni ilimradi hujakiuka sheria za nchi. Nimekusoma mkuu, lete updates zaidi.
 
Hamis Kigwangala anapendekeza upigajimkura ambao ni Proxy Voting. Kwamba, wabunge wanaweza kuwapigiamkura wabunge wenzao ambao hawapo bungeni. Pia anasema kuwa wabunge wanaweza kupiga kura kabla ya siku ya kupiga kura. Hali hiyo itarahisisha upigaji huo wa kura
 
Wanabodi,

Niko hapo Dodoma asubuhi ya leo kuja kuishuhudia kwa macho Rasimu ya Tatu, nimessafiria ungo, huko njia pia nikakutana na Waheshimiwa mawaziri 8 wa serikali ya JMT na wawili wa SMZ, wamejazana kwenye ungo huo huo, likija kutokea la kutokea kwa hizi nyungo kugomea njiani, one can not imagine!. Dar-Dom ni dakika 40 tuu!.

Kwanza rasimu bado, nimeambiwa na taarifa rasmi kuwa itakuwa tayari kesho, taarifa isiyo rasmi, hata kesho haitakuwa tayari!, what a waste kukimbilia Dodoma!.

Tukiwa njiani kwenye ungo wetu, nilipata fursa kuzungumza na Wanzanzibari ambao ni wajumbe wa BMK, kiukweli walinieleze kuwa kufuatia wajumbe wengi wa BMK wakutokea Zanzibar, wamekwenda Hijja, hakuna namna yoyote Akidi ya 2/3 kutoka Zanzibar, haiwezi kutimia!, hivyo asubuhi hii BMK, limeleta marekebisho ya kanuni, kuwaruhusu wajumbe wa BMK kupiga kura mahali popote walipo, iwe ni ndani ya ukumbi wa bunge au nje ya ukumbi, popote walipo, kwa sababu zozote.

Kanuni hii, pia itawaruhusu wana UKAWA, wasiokubaliana na misimamo batili ya vyama vyao kususia BMK, waweze kupiga kura za siri mahali watakapokuwepo!. Nimeshikwa sikio kuwa wana UKAWA, wamemuomba M/Kiti wa BMK, kuruhusiwa kupiga kura za siri wakiwa mafichoni!, wameeleza wamelazimishwa kususia kuhudhuria vikao vya BMK, kinyume cha ridhaa na utashi wao!, wamekubali tuu kususia kukubali collective responsibilities, kuepuka kuitwa wasaliti na kutengwa!.

Kama hili litafanyika, ni hakika 100%, AKIDI Itatimia!.

Katika jokes hizi na zile tukiwa ungoni, mjumbe mmoja wa BMK, alisema AKIDI lazima, itimie, isipotimia itamilizwa ili kuhalalisha ghara kubwa zilizotumika kwenye BMK hadi sasa!.

My Take.
Kama kura muhimu kuliko zote, ambayo ni uchaguzi wa Rais na Wabunge, Tanzania hatuna utaratibu wa kupiga kura nje ya kituo cha kupigia kura!, kisheria kura ni kama kutia saini kwenye mkataba, "the place of contract" ni very crucial, kama sheria ya BMK, ilisema BMK litapiga kura, neno BMK kisheria ni "the place" lilipo BMK!, ikimaanisha ni ndani ya ukumbi wa BMK tuu na sio mahali pengine popote nje ya BMK!.

Kura yoyote itakayopigwa nje BMK, sio valid vote!. Marekebiso hayo ni kuhalalisha tuu ile dhana ya AKIDI isipotimia!, "itatimilizwa!"

Wasalaam.

Pasco
Dodoma.

Mode: Hii sio yanayojiri, hii ni opinion article!.
 
Nimeheshimu maoni yako kwa kuwa unayo haki kikatiba kutoa maoni ilimradi hujakiuka sheria za nchi. Nimekusoma mkuu, lete updates zaidi.
Pamoja sana Mkuu. Hakika una busara ya hali ya juu sana. Nakuomba ukamfanyie Ushauri Nasaha mkuu Bramo ili mapepo yake yatulie
 
Back
Top Bottom