Yaliyojiri Bungeni Dodoma: Jumatatu, Tarehe 10 Machi 2014

Wadau, nipo ndani ya ukumbi wa Bunge na kwa jinsi inavyoonekana kikao hakiwezi kuanza muda huu. Mahudhurio bado ni machache. Pia kile kikao cha Mashauriano kinaendelea
 

kaka nimekukubali sana katika update za bunge, jumamosi nimepitia update zote safi sana
 
mida yenyewe hiyo tusiokuwa bungeni na kwenye tv tunawategemea sana.

Twende kazini
 
Taswira ya Ukumbi wa Bunge dakika tatu kabla ya saa 5 kamili asubuhi
 
Tanganyika nchi ninaekupenda tunakuhitaji
Hasa ktk kipindi hiki muhimu tutakupigania
Kwa njia zote
 
Wadau, nipo ndani ya ukumbi wa Bunge na kwa jinsi inavyoonekana kikao hakiwezi kuanza muda huu. Mahudhurio bado ni machache. Pia kile kikao cha Mashauriano kinaendelea

Hapa ndipo penye matatizo yote.
 
Tanganyika nchi ninaekupenda tunakuhitaji
Hasa ktk kipindi hiki muhimu tutakupigania
Kwa njia zote
Mkuu, wakati ukifika sote kwa pamoja tutaimba wimbo huo. Ila kwa sasa tujadili Kanuni za Bunge Maalum
 
kaka nimekukubali sana katika update za bunge, jumamosi nimepitia update zote safi sana
Nashukuru sana kaka. Tupo pamoja na tutaendelea kuwa pamoja kwa uwezo wa Rabana mpaka mwisho wa Bunge hili
 
@Chabruma na wewe ni mjumbe??? kweli JK aliona viazi
Simiyu Yetu ni yule jamaa aliyeiba simu bungeni P.M
Mkuu, swali hili nimelijibu kwenye mijadala iliyopita hasa ule wa Jumamosi. Mie si mjumbe ila Simiyu Yetu ndo mjumbe. Hatujuani ila tunafahamiana kikazi
 
Mkuu, si matatizo bali ndo chombo muhimu katika kulipatia ufumbuzi suala hili

Ndiyo ni chombo muhimu lakini kwa kadiri wanavozidi kuchelewa kufikia maamuzi ndivyo kodi zetu zinavyozidi kuteketea, mkuu mimi nina uchungu na kodi zetu tu na si vinginevyo japo napenda maridhiano yaliyo bora.
 
Haya mkuu, majina ya wajumbe wote haya hapa.
Mkuu Skype heko sana, nafikiri mdau alihitaji list ya wajumbe wanaounda kamati ya mashauriano, namu napenda kuwajua ni akina nani ili tujue uamuzi wa siri/wazi utakuwa muelekeo upi?
 
mwigulu si yuko kalenga au kasharudi?
Mkuu, Mwigulu alikuwepo sikunya Ijumaa na Jumamosi. Leo sijamuona ila nina hakika kuwa yupo kwq vile kuna vikao vya CCM vinaendelea na Mwenyekiti taifa yupo hapa kwa siku tatu
 
Simiyu yetu kanuni zenyewe anazielewa kweli? Nategemea atakuwa mtu wa ndiyoooooooo! na kugonga meza kama magamba wenzake hasa mwigulu anapochangia kwa kila jambu bila hata kuelewa vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…