Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Chato: Mkutano wa mgombea Urais Dkt. Magufuli (CCM) - Septemba 14, 2020

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Chato: Mkutano wa mgombea Urais Dkt. Magufuli (CCM) - Septemba 14, 2020

Joined
Sep 8, 2020
Posts
67
Reaction score
133
MKUTANO WA MGOMBEA URAIS JOHN POMBE MAGUFULI KUTOKEA CHATO, GEITA UKO LIVE

40A3FF45-EA4E-4DFA-94A8-7E30DF28D007.jpeg

7638201E-093E-44DD-B35C-A159AE3064D1.jpeg

542F62DC-7A31-4775-BC47-F9321F0A62E9.jpeg


20056143-5250-40A4-A0F7-416C0F11911C.jpeg

0F3166A7-95BD-4897-BD2E-213EAEE7EC16.jpeg


===

MAGUFULI: Ndugu zangu wa Chato na Geita kwa ujumla, mwaka 1995 nilikuja kuomba kura kwa nafasi ya ubunge, mkanipa miaka 5, nikaja tena mwaka 2000, nikaja tena 2005. Katika vipindi vyote vinne nikiwa mbunge wenu na katika vipindi hivyo vyote vinne vya miaka 20, mara mbili mlinipitisha bila kupingwa, sikupingwa na chama chochote.

Kwa hiyo katika miaka 20 niliyokuwa mbunge wenu, miaka 10 ndio niligombea, miaka kumi mingine nilipita free, ninawashukuru sana. Katika hio miaka 20 mliyonifundisha nikiwa mbunge, napenda nikiri nilijifunza mengi na nyinyi ndio mkawa chanzo cha kuwafanya wale wengine katika nchi hii wanijue na ndio maana miaka 5 iliyopita niliweza kuaminiwa na chama changu cha Mapinduzi katika nafasi nyingine ya juu zaidi ya Urais.

Nawashukuru wana Chato, nawashukuru watanzania wote kwa kuniamini katika miaka mitano iliyopita katika nafasi ya Urais.

Dkt. Magufuli: Kuhusu masuala ya Afya kwenye ilani ya mwaka huu, tunataka Watanzania wote wawe na Bima ya Afya. Mpaka mwisho wa mwaka huu Watanzania watakuwa zaidi ya Milioni 60.

Dkt. Magufuli: Wakati Mimi mnanichagua kuwa Mbunge Jimbo hili lilikuwa linaitwa Biharamulo Mashariki haikuwa Wilaya. Miaka 5 iliyopita Tanzania ilikuwa na Uchumi wa Chini lakini sasa Dunia nzima inajua kuwa Tanzania iko Uchumi wa Kati, jipongezeni.

MAGUFULI: "Lakini watu bila kutumia busara wakasema fungia, tukasema hapana serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Magufuli hakuna lockdown au mjukuu wa lockdown. Tutaendelea kutamba barabarani kwa sababu tunaamini Mungu wetu yupo na Mungu ni mkubwa, hakuna kinachoshindikana mbele ya Mungu.

Eti hata kanisani usiende, hata msikitini usiende, ni shetani alitaka kutawala dunia lakini hatatawala Tanzania, shetani ataendelea kushindwa kwa sababu tunajitambua, nchi yetu inaamini pia katika imani za watu tofauti. Huwezi ukawazuia masheikh hawa, mapadri hawa, maaskofu hawa wasiende kumtukuza Mungu na kumuabudu, tulisimama imara na Mungu ametusikia.

Sasa inawezekana hata haya yote hamyapendi, sasa fanyeni makosa mkachagua hao, siku ametawala, siku hiyohiyo anawaweka lockdown"

Dkt. Magufuli: Daraja la Busisi tuliloanza kulijenga ndio litakuwa Daraja refu zaidi Afrika Mashariki. Litakuwa na urefu wa Kilomita 3.2 na ujenzi wake unagharimu Bilioni 700. Hakuna Mtu alitegemea tutapata fedha sisi wenyewe za ujenzi. Haya ni maajabu

Dkt. Magufuli: Tani moja ya Ndizi ukisafirisha kwa njia ya barabara unalipa 127,000/= lakini leo tani moja ya ndizi ukitumia Meli utalipa 27,000/= Tunapeleka utajiri kwa Wananchi, tunapeleka utajiri kwa Wafanyabiashara. Hii ndio Tanzania tunayoitaka

Dkt. Magufuli: Katika Wagombea wa Urais hakuna anayeweza kutekeleza haya hata robo tu. Ninawaambia ukweli lakini kama mnataka kujaribu jaribuni, mtakuja kuniambia siku moja. Huwezi kumuona mtu anazungumza mtakuwa mnakula ubwabwa wakati hata kwake haumtoshi huo ubwabwa

Huwezi ukazungumza ni maisha ya bata, hakuna vya bure. Hata misaafu yote imezungumza na asiyefanya kazi na asile.

Uongozi ni kutoa sadaka, nimeamua kutoa maisha yangu ya uongozi kama sadaka kwa watanzania. Hii kazi ndugu zangu ni ngumu lakini nina uwezo wa kuifanya tena katika kipindi cha miaka 5.

Shule zilikuwa hazitoshi, mimi nakumbuka, nilipokuwa nikisoma hapa Chato shule ya msingi, tulioenda sekondari tulikuwa wawili tu katika mwaka wetu, nilikuwa mimi na marehemu Rutamigwa Mungu amtangulie mbala ya haki. Sio kwamba wale ambao hawakwenda sekondari hawakuwa na akili, walikuwa na akili sana lakini nafasi hazikuwepo.

Ndio maana tulipoingia madarakani, tukasema katika kipindi hiki cha miaka 5 ni lazima tuweke miakakati ya kuhakikisha watoto wetu wanaenda shuleni ili kuhakikisha vijana wengi wanakwenda shukleni ndio maana tukafuta ada.

Dkt. Magufuli: Mtu anasimama, tena ameshiba, mashavu yamevimba anasema Mimi mkinichagua hakuna kodi. Utaiendesha vipi nchi? Unapohitaji kura ni vyema Watanzania wakaujua ukweli.

Dkt. Magufuli: Hatuchagui Mtu kwa kuangalia sura, Mimi sura yangu mbaya kweli. Tunachagua mtu kwa ajili ya kuleta maendeleo. Kalemani unafanya kazi nzuri. Kwasababu bado una Uwaziri hadi tutakapoapishwa, nenda ukaanze mipango ya kupeleka taa za barabarani Bukombe.

Dkt. Magufuli (CHATO): Mtu anasimama ameshiba ugali anasema ndege hazina faida, yeye alikotoka huko alikuja na Bajaji? Angetoka huko alikokuwa na Bajaji mpaka hapa, mambo mengine yanaudhi. Watanzania wanajua wapi wametoka, wapi walipo na wapi wanakwenda.

=====
MAGUFULI: MZEE MKAPA NDIYE ALIYENIOKOTA HUKO ‘JALALANI’

Mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Magufuli amesema akimfikiria Hayati Rais Mkapa huwa anaumia kwenye nafsi yake

Amesema Rais Mkapa ndiye aliyemuokota ‘Jalalani’ amesema hayo kwa kuwa kuna watu wanadai siku hizi mtu akipata kazi anasemwa amokotwa jalalani na Magufuli

Dkt Magufuli amesema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa Kampeni uliofanyika Chato mkoani Geita. Aidha amewataka wananchi kuendelea kumuamini

Katika Kampeni hizo Magufuli amesema walisimama imara kukomesha uhalifu, kama maeneo ya Kibiti na Biharamulo. Amewapongeza sana vyombo vya ulinzi na usalama.



 
Naiomba Serikali itolee ufafanuzi hii kauli, ili kuondoa sintofahamu kwa wananchi,hususani wafanyakazi

Serikali imekopa mifuko ya hifadhi za jamii PSSSF na NSSF na haijaweza kurudisha. MBAYA zaidi, mwaka huu kuanzia April hivi, Mifuko imeshindwa kulipa mafao. Jana Mh. Lisu akasema kuwa CCM imechukua pesa Za KAMPENI huko kwenye mifuko ya PSSSF na NSSF. Je wafanyakazi mnalipwa mafao yenu ya uzee na fao la kukosa ajira kwa wakati?

Mimi sijui, kamuulizeni aliyesema ..ni Mh. Lisu. Sikilizeni clip za Mwananchi Youtube.

Na akiwa Morogoro, akasema Vigogo wa CCM wamepora mashamba makubwa mvomero, Morogoro. Mkapa elfu 60, Familia ya Mwinyi elfu 60, Sumaye 2000 etc. Sehemu mbali mbali za nchi na zile ranch. Wananchi wanakosa maeneo ya kulima na kulishia mifugo...

Ni Mh. Lisu alisema...Youtube.

Sasa hizi ndio hoja za kujibu kwa Serikali..na Sio kusema kuna mtu anatukanwa..
 
Nyamikoma,Kamwanga,lwenge,bugurura , buseresere na katoro ni miji na vijiji vilivyopo Mkoa wa Geita,JPM atoe kauli ni lini watapatiwa maji Safi na salama, na vijiji hivyo vitapatiwa lini nishati ya umeme? Na Barabara? Mji wa katoro na buseresere vumbi inawapa watu tibii hakuna lami,na mji unakuwa kwa kasi
 
MKUTANO WA MGOMBEA URAIS JOHN POMBE MAGUFULI KUTOKEA CHATO, GEITA UKO LIVE

Tumia hizi Links Chini Kufuatilia Kila kitu kutokea Chato, Geita


HAPA LAZIMA MUISOME
 
MKUTANO WA MGOMBEA URAIS JOHN POMBE MAGUFULI KUTOKEA CHATO, GEITA UKO LIVE

Tumia hizi Links Chini Kufuatilia Kila kitu kutokea Chato, Geita

👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿

👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿


👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿

 
Back
Top Bottom