Nilidhanigi ma wewe una msimamo!
Hatuwezi kufanana kwenye kila kitu ndugu yangu mimi ni mpinzani wa ccm tangu 1984, na sijawahi kukipenda hicho chama tangu wakati huo
Msimamo wangu ulibaki hivyo hata baada ya vitisho vya kufukuzwa kazi na utumishi.. Nilibaki na msimamo huohuo nimekosa mengi sana kwakuwa tu nilikuwa siivi na ccm na sijawahi kujutia huo uamuzi
Siasa za mageuzi zilikuwa 1992 Mimi nikiwa mpinzani Binafsi miaka 8 kabla, naifahamu ccm vizuri sana na nina kila sababu ya kuwa na msimamo wangu katika hili
Waliosoma Enzi za kunywa uji wa 'bulga' kupewa mikebe na madaftari bure kupata elimu ya uhakika mpaka kipato cha sita kwa Ada nafuu mno na hatimaye chuo kikuu watanielewa zaidi, ccm baada ya kifo cha Moringe Sokoine ilipoteza dira na mwelekeo, aliyotabiri mchonga miaka ile ndio yanatokea sasa....
barafuyamoto ninapochagua kushabikia upinzani nina sababu na maana kamili ninajitambua na nina msimamo thabiti katika hili... Nchi hii leo hii wananchi wamekuwa raia daraja la pili, huku wageni wakitukuzwa na kupewa kipaumbele kwenye kila sekta
Yako wapi madini yetu??? Tumeachiwa nini? Mashimo ya nguchiro na panyabuku na mazalia ya mbu... Viko wapi viwanda vyetu? Viko wapi vyama vyetu vya ushirika? Michezo yetu? Maliasili zetu?
Tumetapanya na kuharibu kila kitu, tumefisha vyote kwa ajili ya mlungula na ten percent...! Uroho na kukosa uzalendo
barafuyamoto tulikuwa na ccm nzuri sana ccm ya mchonga meno nchi ilikuwa inaongozwa kwa vision chama kilikuwa kimeshika hatamu na tulikuwa tunaona kabisa tulikotoka tulipo na tuendako, tuliheshimika na kuaminika kama chama kama nchi na kama taifa... Leo hii Heshima na uaminifu wa ccm vipi wapi?
Tumesafiri tumeona kwa wenzetu tuliokuwa nao miaka ile leo wametuacha mbali sana... Tulikosea wapi? Ghiliba ulozi kukengeuka kwa chama na kuacha misingi yake... Kuipa siasa thamani kubwa vimetufikisha hapa tulipo na hii yote ni kupitia ccm
Haya siyaandiki Leo niliandika sana wakati ule wa wa gazeti la MTANZANIA kupitia safu ya shusha pumzi sikubakisha kitu na baadhi ya makala ziliniponza na mengi lakini sikuacha kuandika
Nina amani sasa nina furaha sasa kuona sasa mabadiliko yanakuja nilitamani nilione hili namwomba Mola anisaidie kuona mwisho wake.. Hatukupambana majukwaani kwakuwa kila mtu ana jinsi yake ya kupambana....mageuzi ya Tanzania Yana jasho langu na Lowassa nilimkubali tangu zamani na huo ndio msimamo wangu