barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,378
- 29,739
Baba jeni baibai hiyo....
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rais sio mtumishi wa umma moja kwa moja ila ni bosi wa watumishi wa umma.Sasa yeye mwenyewe mbona anajiona ni exceptional kwani yeye sio mtumishi wa umma?
Hio ni kutokana na katiba ya Lumumba au?Rais sio mtumishi wa umma ila ni bosi wa watumishi wa umma.
ni wivu tuAnamtisha CAG ili iweje? Baada ya kuliweka bunge mfuko na mahakama ninitegemea hii ofisi ataiweka mfukoni. Vta ya ufisadi ndio imeyeyuka tutegemee upigaji wa kutisha miaka 5 ya mwisho ya utawala wake.
Hapana. Ya ufipa.Hio ni kutokana na katiba ya Lumumba au?
Form iv - DIV ONE, Form vi - DIV ONE.. "Huyu ni kipanga sio kilaza"
Pambio na ziendelee kwa kiongozi wa malaika
Wataokumbukwa kama cag aliyedumu miaka 5 tu..Prof Mussa Assad atakumbukwa na vizazi vijavyo kama Mtanzania pekee kwenye awamu ya 5 aliyebakia amesimama dhidi ya ya utawala dhalimu, usioheshimu misingi ya Katiba, utawala wa sheria na utawala bora.
Jina lake litaandikwa kwenye kitabu cha mashujaa kwa wino wa dhahabu kwa kuwa alikataa kutepeta dhidi ya utawala wa kidikteta wa Magufuri. Amekataa katakata kulamba soli ya viatu vya Magufuri kama wanavyolamba wengine mfano Jaji Mkuu, Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, DPP na AG.
Profesa Mussa Assad umewatendea haki Watanzania na umeonyesha thamani ya elimu yako kwa kuibua upotevu mkubwa wa fedha za walipa kodi wa nchi yetu zipatazo Tsh 2.4 Trilion kwa kipindi cha miaka 4 kutoka utawala unaojifanya anachukua rushwa.
Yanayoendelea tunayaona kwa kupitia mteule anayekuja kuchukua nafasi yako. Hata kipofu anajua Charles Kicheere amekuja kubariki mazingira ya "plunder with impunity" kwa kipindi Magufuri atakapokuwa madarakani.
Kupumzika Prof Mussa Assad, kazi yako ilikuwa ni ya kutukuka, tutakukumbuka hata Muumba akiwa amechukua roho yako.
Mkuu usisahau Kuna hapa na pale pia.Hapo mbowe kute alilamba mazerooo tu
State agent
Ujumbe ufike kunakohusika.Rais Magufuli: Kwa CAG mpya nakutakia kazi njema. Usiende huko ukajifanya Muhimili. Mihimili ni mitatu tu na umeiona hapa Mahakama, Bunge na Sisi wa Serikali - Katika Kiapo chako ni Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, kwa hiyo mwenye Serikali yupo
Rais Magufuli: Kafanye kazi zako za ukaguzi vizuri bila kuonea mtu. Unapopewa kazi na Mihimili mingine kama Bunge, katekeleze. Usibishane nao - Ukipewa maagizo na Mahakama katekeleze, wewe ni Mtumishi. Lakini pia kasimamie hiyo ofisi, kasimamie watendaji wako
Rais Magufuli: Kuna baadhi ya watendaji wako wanapopewa jukumu la kwenda kukagua kwenye Balozi wanalipwa fedha hapa na wakifika kule wanaomba pesa - Sitaki nikutajie majina yao, wewe nenda kule kachambue mwenyewe kwenye ofisi hii. Ofisi ya CAG sio Clean kama mnavyofikiria
Rais Magufuli: Nenda ukapange nafasi za watu wako ili mauchafuuchafu haya ukayasafishe. Najua una Qualification nzuri tu na hatufanyi makosa ktk kuteua - Form 4 umetoka na Div. I, Form 6 Div. I. Hii ni kuonesha wewe ni Kipanga sio Kilaza. Ukachukua Shahada ya Sheria na Account
Rais Magufuli: Tunakuamini. Pia, una heshima, umetolewa kwenye Ukamishna Jenerali wa TRA hukusema neno, 'You're humble, very polite' ukaenda ukafanya kazi huko - Wapo wengine ukiwateua wanafikiri ni nafasi zao. Unampa U-DC ukimtoa ananza kulalamika, wakati hakulalamika ukimteua
Weweeeeee!Influenza,
Mambo yote Chapchap, bado Assad anajiuliza ni vipengele gani vimetumika? Basi agome kuachia ofisi basi.
Niliwahi kuuliza ukaguzi wa ofisi ya CAG unafanywa na nini...sikumbuki kupata jibu ya swali hilo.Rais Magufuli: Kuna baadhi ya watendaji wako wanapopewa jukumu la kwenda kukagua kwenye Balozi wanalipwa fedha hapa na wakifika kule wanaomba pesa - Sitaki nikutajie majina yao, wewe nenda kule kachambue mwenyewe kwenye ofisi hii. Ofisi ya CAG sio Clean kama mnavyofikiria
Tenaaa!!?Kicheere anaenda kukagua madudu yake TRA.
Wakati akitumbuliwa TRA tuliambiwa ali 'under perform'.
Sasa hivi kapewa kazi ya kukagua taasisi ambayo mwaka wa fedha uliopita yeye ndie alikuwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo.
Siye Team TANROAD tunamtakia kila la kheri.