Yaliyojiri Ikulu Dar: Rais Magufuli amtaka CAG Kichere kutojifanya Muhimili mwingine, amwambia anaweza kuondolewa hata akiwa na mwaka mmoja

Binafsi nakubaliana na hii kauli haiwezekani uwe na uwezo wa kuteua na ukakosa uwezo wa kutengua.

Kuna wakati ililazimu bunge liweke shinikizo ndipo waziri atenguliwe na hapa nakumbuka sana enzi za Spika Makinda.

Nimeupenda sana huu msimamo. Haiwezekani uteue kwa mujibu wa katiba halafu usitengue kwa mujibu wa katiba. Hiyo katiba ni ya sayari gani au tunakwama katika tafsiri?

Maendeleo hayana vyama!
 
Anamtisha CAG ili iweje? Baada ya kuliweka bunge mfuko na mahakama ninitegemea hii ofisi ataiweka mfukoni. Vta ya ufisadi ndio imeyeyuka tutegemee upigaji wa kutisha miaka 5 ya mwisho ya utawala wake.
ni wivu tu
 
Prof Mussa Assad atakumbukwa na vizazi vijavyo kama Mtanzania pekee kwenye awamu ya 5 aliyebakia amesimama dhidi ya ya utawala dhalimu, usioheshimu misingi ya Katiba, utawala wa sheria na utawala bora.

Jina lake litaandikwa kwenye kitabu cha mashujaa kwa wino wa dhahabu kwa kuwa alikataa kutepeta dhidi ya utawala wa kidikteta wa Magufuri. Amekataa katakata kulamba soli ya viatu vya Magufuri kama wanavyolamba wengine mfano Jaji Mkuu, Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, DPP na AG.

Profesa Mussa Assad umewatendea haki Watanzania na umeonyesha thamani ya elimu yako kwa kuibua upotevu mkubwa wa fedha za walipa kodi wa nchi yetu zipatazo Tsh 2.4 Trilion kwa kipindi cha miaka 4 kutoka utawala unaojifanya anachukua rushwa.

Yanayoendelea tunayaona kwa kupitia mteule anayekuja kuchukua nafasi yako. Hata kipofu anajua Charles Kicheere amekuja kubariki mazingira ya "plunder with impunity" kwa kipindi Magufuri atakapokuwa madarakani.

Pumzika Prof Mussa Assad, kazi yako ilikuwa ni ya kutukuka, tutakukumbuka hata Muumba akiwa amechukua roho yako.
 
Wataokumbukwa kama cag aliyedumu miaka 5 tu..
 
Ujumbe ufike kunakohusika.
 
Niliwahi kuuliza ukaguzi wa ofisi ya CAG unafanywa na nini...sikumbuki kupata jibu ya swali hilo.
 
Leo baada ya kumuapisha CAG mpya ambaye kimsingi kateuliwa kinyume cha sheria za nchi kwa mujibu wa sheria ya subsection 3 iliyoko hapa nchini, ambayo ilitaka CAG aongezewe mkataba la sivyo utaratibu wa kutomuongezea mkataba sheria inasema shruti ufuate ibara ya 144 ya katiba inayohusu namna kumuondoa CAG (isome hapa chini) :

Lakini katika muendelezo uleule wa kuvunja katiba rais amemuagiza CAG mpya kufuata maagizo ya mihimiliingime wakati wa utekelezaji. wa majukumu yake, Agizo hili ni. kinyume cha Katiba ibara ya 143(6) kinachozuia CAG kufuata maagizo ya mtu yeyote au ya idara yoyote. Katika hili huu ni msiba mkubwa sana kwa Taifa.
Ibara ya 143 kipengele cha 6 kinazuia kabisa CAG kupokea maagizo kwa mtu yeyote, lakini inashangaza leo Rais Magufuli anamwagiza CAG kutii maagizo atakayopewa. hii ni ajabu sana

Tenaaa!!?
 
Tumia busara kidogo, usiweke kifungu kimoja, weka kifungu chote cha Katiba 144.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…