Jamii Forums inakukaribisha kwenye Mjadala wa Ugonjwa wa UVIKO-19 na Waliopata Chanjo
Ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika Clubhouse leo Septemba 2, 2021 kuanzia Saa 11:30 jioni hadi saa 2:00 usiku
Link:
UVIKO-19: Mjadala wa waliopata Chanjo - JamiiForums
=====
UPDATES:
=====
Dkt. Elisha Osati: Kila siku napokea watu ambao wanataka niwahakikishie wakachanjwe. Sio kwamba hawataki ila wanataka uhakika Tukiendelea kutoa elimu itakuwa jambo zuri. Bahati mbaya hatutoi takwimu lakini tuna wagonjwa wengi katika Wodi zetu
#JamiiTalks #UVIKO3
Dkt. Aikande Kwayu: Wananchi hawawezi kuona tupo serious wakati kuna mikusanyiko mikubwa Ile imani ya kwamba ugonjwa upo, tukachanje lazima tuoneshe hatari ya ugonjwa na tuoneshe tupo serious kupambana
#JamiiTalks #UVIKO3
Dkt. Aikande Kwayu: Ni muhimu 'ku-engage' Viongozi wa Dini kwa nguvu sana kuhakikisha chanjo inaongelewa Misikitini au Kanisani Issue ya wasiwasi wa chanjo sio Tanzania tu ni duniani
#JamiiTalks #UVIKO3
Neema Lugangira: Tunahitaji Wataalamu wetu wa Afya kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa sahihi. Vituo vya Afya vipo ngazi zote
#JamiiTalks #UVIKO3
Mbaraka Islam: Sisi kama Vyombo vya Habari tuna wajibu mkubwa kusaidia jamii. Hili suala linahusu maisha ya watu Tufike mahala tuchukulie hii kama vita kwasababu watu wanakufa. Bahati mbaya tumeweka mzaha
#JamiiTalks #UVIKO3
View attachment 1921196View attachment 1921197View attachment 1921198View attachment 1921199View attachment 1921200View attachment 1921201View attachment 1921202View attachment 1921203View attachment 1921204View attachment 1921205