#COVID19 Yaliyojiri JamiiForums Clubhouse kwenye Mjadala wa UVIKO-19, Umechanja au haujachanja? Nini mtazamo wako?

#COVID19 Yaliyojiri JamiiForums Clubhouse kwenye Mjadala wa UVIKO-19, Umechanja au haujachanja? Nini mtazamo wako?

Huu mjadala ungedumu kwa muda wa siku tatu, napendekeza. Kwa wakati huo huo uliopendekezwa, ili kuwapata wadau waliojiandaa wengi zaidi.

Maana inaweza kutokea baadhi ya maswali muhimu yakakosa majibu au majibu yasijitosheleze.

Au kuna taarifa ilitolewa humu JF kabla, kuwajulisha watu?
 
Nimechanja niko fiti na familia ,ukichanjwa unaondoa woga badala ya kusema eti woga ndio unaouwa .

Woga wa kutokuchanjwa ni hatari Sana ,ukichanjwa unajiamini Sana na haina madhara

Kwa watu wanaotoka/aliokatika familia duni kugharamia matibabu ya Corona ni ishu kuna waginjwa wanapewa bills za mil 5 hadi kumi ni hatari sana usipochanjwa

USSR
 
nafikiri kuweka vaccination status ya washiriki mmekosea maana wote hapo wamechanjwa, alternatively ilitakiwa kufanya jitihada za kuwapata ambao hawajachanja ili kubalance otherwise itachukuliwa kama ni kampeni ya kuhamasisha watu kuchanja na si kupata maoni huru
 
nafikiri kuweka vaccination status ya washiriki mmekosea maana wote hapo wamechanjwa, alternatively ilitakiwa kufanya jitihada za kuwapata ambao hawajachanja ili kubalance otherwise itachukuliwa kama ni kampeni ya kuhamasisha watu kuchanja na si kupata maoni huru
Na ndio ilivyo...Bashungwa hakuja bure
 
"Nimechanja nitashiriki"- uelekeo ushajulikana🤣
Mkuu umefungua link?

 
Jamii Forums inakukaribisha kwenye Mjadala wa Ugonjwa wa UVIKO-19 na Waliopata Chanjo

Ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika Clubhouse leo Septemba 2, 2021 kuanzia Saa 11:30 jioni hadi saa 2:00 usiku

Link: UVIKO-19: Mjadala wa waliopata Chanjo - JamiiForums

=====

UPDATES:
=====

Dkt. Elisha Osati: Kila siku napokea watu ambao wanataka niwahakikishie wakachanjwe. Sio kwamba hawataki ila wanataka uhakika Tukiendelea kutoa elimu itakuwa jambo zuri. Bahati mbaya hatutoi takwimu lakini tuna wagonjwa wengi katika Wodi zetu #JamiiTalks #UVIKO3

Dkt. Aikande Kwayu: Wananchi hawawezi kuona tupo serious wakati kuna mikusanyiko mikubwa Ile imani ya kwamba ugonjwa upo, tukachanje lazima tuoneshe hatari ya ugonjwa na tuoneshe tupo serious kupambana #JamiiTalks #UVIKO3

Dkt. Aikande Kwayu: Ni muhimu 'ku-engage' Viongozi wa Dini kwa nguvu sana kuhakikisha chanjo inaongelewa Misikitini au Kanisani Issue ya wasiwasi wa chanjo sio Tanzania tu ni duniani #JamiiTalks #UVIKO3

Neema Lugangira: Tunahitaji Wataalamu wetu wa Afya kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa sahihi. Vituo vya Afya vipo ngazi zote #JamiiTalks #UVIKO3

Mbaraka Islam: Sisi kama Vyombo vya Habari tuna wajibu mkubwa kusaidia jamii. Hili suala linahusu maisha ya watu Tufike mahala tuchukulie hii kama vita kwasababu watu wanakufa. Bahati mbaya tumeweka mzaha #JamiiTalks #UVIKO3



View attachment 1921196View attachment 1921197View attachment 1921198View attachment 1921199View attachment 1921200View attachment 1921201View attachment 1921202View attachment 1921203View attachment 1921204View attachment 1921205
Tusisahau pia kusikiliza hii.
 
Ni chanjo gani hapo nyuma walipewa wanadamu kwa ajili ya kujikinga na homa flani kisha wakachanjwa badae waliambukizwa nao wanaathirika? Kwa mfano chanjo ya polio, chanjo ya uti wa mgogo. Chanjo ya ini
sijaelewa swali lako
 
...Harafu kuna muuza genge kule Mbagala ugali wenyewe mtihani,panadol kuzipata kwa manati,yupo bize akipayuka hataki kuchanjwa....
 
Back
Top Bottom