Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Leo mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi yuko mkoani Njombe na kwa sasa anaongelea afya na Bima ya Afya.
Ameeleza kuwa walianza na vituo vya afya na kinachofata ni bima ya afya, pia ameelezea walishaanza na wamejitahidi kutoa huduma za bure kwa wazee, watoto wenye umri chini ya miaka mitano na wagonjwa wenye magonjwa makubwa wanahudumiwa na serikali.
Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano, wagonjwa kusafirishwa nje wamepungua kwani hata operesheni za moyo zinafanyika Dar es Salaam, operesheni za kubadilisha figo zinafanyika Dodoma na hospitali ya Njombe ikikamilika pia hayo yatafanyika.
Endelea kuwa nami kukujuza yanayojiri Njombe
===========
MAGUFULI: Ndio maana tumekuja tena kuomba kura kwa sababu tunafahamu mikakati, tunafahamu mbinu lakini pesa pia zipo. Hatuitaji fedha za kukopa nje, fedha ziko hapahapa, zilikuwa zimekaliwa na mafisadi, mafisadi tumewabana zinaenda kwa wananchi.
===
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Magufuli amesema sababu ya kugombea Urais kwa Muhula wa Pili ni mipango mizuri waliyonayo kwenye Ilani yao ya Uchaguzi
Kati ya mipango hiyo, ametaja pia kujenga Uwanja wa Ndege Mkoani Njombe, kwa kuwa watu wa Njombe ni wakulima wazuri. Amewatania kwa kusema, ndege pia zitatumika kusafirisha Ulanzi kuwafikia watu wa Dar
Pia, amesema atakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Njombe na kuwezesha watanzania wote kuwa na Bima ya Afya na kabla ya kuwa na Bima ya Afya, kwanza wamepanga kujenga Vituo vya Afya, Hospitali na kuongeza bajeti ya kununua madawa
Ameyasema hayo alipokuwa Viwanja vya Polisi, Makambako Mkoani Njombe katika mkutano wa kampeni.