Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kampeni ya Dkt. Magufuli kuwania Urais 2020-2025 mikoani Iringa na Njombe (Sept 29, 2020)

mapokezi au fiesta, kumbuka hata Hashimu Rungwe angeambatana na watoa burudani plus kusomba watu kama mifugo kwenye mikutano yake pasingetosha...kiukwel watu wengi huenda kuona show ya bure kwenye mikutano ya Jiwe na ndio maana hata akimaliza kuhutubia watu huwa hawaondoki kwasabb show huwa inaendelea.
 
Leo mgombea wa CHADEMA Mh Tundu Antipasi Munghwai Lissu alipaswa kufanya mikutano yake ya kampeni mkoani Kilimanjaro. Ratiba iliyotolewa awali ilisema TUNDU atafanya mkutano mkubwa Wilayani Hai.

Taarifa zilizotufikia zinasema kuwa Mh TUNDU ameshindwa kuendelea na kampeni baada ya kuona mapokezi makubwa ya Dkt. Magufuli aliyoyapata Mkoani IRINGA Jana. TUNDU amelazimika kupumzika ili aweze kujitathimini na kutafuta njia mpya ya kumkabili Dkt. Magufuli. TUNDU aliaminishwa IRINGA ni ngome yake, lakini baada ya mtiti wa jana TUNDU amechanganyikiwa.

Wakati Tundu akitafuta njia ya kurudi tena Iringa, mgombea Ubunge wa Jimbo la IRINGA kupitia CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa amefungua program ya kutafuta wafuasi wa kumsaidia mitandaoni.

Mikutano iliyoendelea Leo Ifunda, Mafinga, Nyololo, Makambako na Silali inazidi kumchanganya Tundu.

#JPM2020
ndabila wa ileje vip ndugu...
 
Waelezee ukweli JPM anazidi kupasua anga balaa
 
Leo mgembea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi yuko mkoani Njombe na kwa sasa anaongelea afya na Bima ya Afya, ameeleza kuwa walianza na vituo vya afya na kinachofata ni bima ya afya, pia ameelezea walishaanza na wamejitahidi kutoa huduma za bure kwa wazee, watoto wenye umri chini ya miaka mitano na wagonjwa wenye magonjwa makubwa wanahudumiwa na serikali.

Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano, wagonjwa kusafirishwa nje wamepungua kwani hata operesheni za moyo zinafanyika Dar es Salaam, operesheni za kubadilisha figo zinafanyika Dodoma na hospitali ya Njombe ikikamilika pia hayo yatafanyika.

Endelea kuwa nami kukujuza yanayojiri Njombe

===========

MAGUFULI: Ndio maana tumekuja tena kuomba kura kwa sababu tunafahamu mikakati, tunafahamu mbinu lakini pesa pia zipo. Hatuitaji fedha za kukopa nje, fedha ziko hapahapa, zilikuwa zimekaliwa na mafisadi, mafisadi tumewabana zinaenda kwa wananchi.

===
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Magufuli amesema sababu ya kugombea Urais kwa Muhula wa Pili ni mipango mizuri waliyonayo kwenye Ilani yao ya Uchaguzi

Kati ya mipango hiyo, ametaja pia kujenga Uwanja wa Ndege Mkoani Njombe, kwa kuwa watu wa Njombe ni wakulima wazuri. Amewatania kwa kusema, ndege pia zitatumika kusafirisha Ulanzi kuwafikia watu wa Dar

Pia, amesema atakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Njombe na kuwezesha watanzania wote kuwa na Bima ya Afya na kabla ya kuwa na Bima ya Afya, kwanza wamepanga kujenga Vituo vya Afya, Hospitali na kuongeza bajeti ya kununua madawa

Ameyasema hayo alipokuwa Viwanja vya Polisi, Makambako Mkoani Njombe katika mkutano wa kampeni
Magufuli asitufanye Watanzania kuwa wajinga kama hao wanachama wa CCM kwani waliokuwa wanakwenda kutibiwa nchi za Nje walikuwa wananchi wanyonge au vigogo huko Chamani na Serikalini kama akina Ndugai aliyekwenda India na familia na wasaidizi wawili na kukaa Hotel ya Nyota 5 miezi 5. Magufuli Rais na Waziri wake wa Afya walikubali kulipa gharama hizo na zile kubwa za matibabu kwa kukaa nje ya Hospital na madaktari kwenda kumhudumia kumbe angeweza kupanga nyumba karibu na Hospital kama alivyofanya Nyerere London na Lissu Ubelgiji. Kama mtu yeyote angefuatilia matibabu ya Ndugai India angekuta Wahindi bado wanashangaa mgonjwa toka nchi masikini akakaa Hotelini miezi 5 kumbe angeweza kupata hata chumba cha VIP Hospitalini ikawa nafuu kwa Tanzania mlipaji. Mabilioni Serikali iliyolipa ndo umeleta urafiki wa kishetani (unholy alliance) kati ya Magufuli na Ndugai na kufanya Bunge kuwa kama Idara ya Serikali ya Magufuli ili kufunika kombe mwanaharamu apite.
Kuhusu matibabu anayodai sasa kwa juhudi za Awamu ya Tano yanapatikana nchini lakini nani wananufaika na matibabu hayo kama si walewale waliokuwa wanatibiwa nje ya nchi na kugharimiwa na Serikali kwa sababu gharama ni kubwa mno kwa mkulima au mfanyakazi wa chini kumudu. Bima ya Afya kwa wote amerukia tu ni mpango wa Lissu na wanachama wa CCM wamemponda sana wakihoji fedha atapata wapi utadhani Magufuli anatoa pesa mfukoni kwake kununua madege au kujenga Uwanja wa Kimataifa kijijini kwake. Hospitaliii ya Muhimbili ilijengwa na wakoloni na kuboreshwa mara kwa mara na Awamu ya Kwanza na Awamu zilizofuata, Mloganzila imejengwa na Kikwete, ya Dodoma na Mkapa RIP, KCMC na Bugando zimejengwa na Wakristo. Zahanati na Vituo vya Afya vinavyoimbwa kila wakati na kila mahali vingi vimejengwa kwa nguvu za wananchi na vingi vimekataliwa kufunguliwa kwa kujengwa chini ya viwango kwa sababu ya 10% ndo maana ni takwimu tu zinatajwa lakini havionekani. Wakazi wa Mkoa wa Njombe hawahitaji kiwanja cha Ndege kubeba ulanzi wanahitaji utekelezaji Mradi wa barabara toka Njombe mjini kupitia Lupembe mpaka Morogoro kuunganisha na TANZAM kufupisha safari kwenda Dar es Salaam. Mradi huu muhimu ulibuniwa Awamu ya Nne lakini Awamu ya Tano ya maneno bila vitendo ilipoingia madarakani ikawa mwisho wa safari na sasa anazungumzia Uwanja wa Madege.
 
*SAMBAZA UWEZAVYO ILI WANANCHI WENGI ZAIDI WA ROMBO WAPATE UJUMBE HUU**

*Ziara ya Mhe. Tundu Lissu Rombo**

Itakuwa kesho kuanzia saa 6 kamili mchana ambapo atafanya mkutano mkubwa sana Tarakea katika viwanja vya stendi ya mabasi Tarakea mjini, akitokea Jimbo la Siha kupitia west Kilimanjaro, kabla ya mkutano wake wa Tarakea Tundu Lissu atasalimia wakazi wa Kamwanga, Endonet na Rongai watakaokuwa eneo la Rongai, na baada ya kumaliza mkutano wa Tarakea akiwa njiani kuelekea Moshi kumalizia mkutano wake wa mwisho kwa siku ya kesho Moshi mjini, njiani atawasalimia wakazi wa maeneo yafuatayo...

Tarafa ya Mashati atawasalimia wale watakaokuwa wamesimama eneo la Mashati soko la zamani, hususan wale watakaosgindwa kuhudhuria mkutano mkubwa wa Tarakea.

Tarafa ya Mkuu atawasalimia wananchi eneo la kiboro.

Tarafa ya Mengwe atasalimia wananchi eneo la Mamsera.

Ninatumia fursa hii adhimu kuwaomba wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa kujitokeza kwa wingi kumpokea na kumsikiliza Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA katika mkutano wake huo utakaofanyika Tarakea, lakini pia kwa wale watakaoshindwa kufika Tarakea, tujumuike katika maeneo yaliyotajwa hapo juu ambapo atafanya mikutano midogo midogo

*HII SIO YA KUKOSA**

*BERNADINE NGOWI**
*M/kiti CHADEMA**
*ROMBO**
29/09/2020

Sasa sjui siha ni wapi utajaza mwenyewe
Safi sana kamanda, umesomeka!
 
Aliyebaki kutibiwa nje na mabeberu ni Lisu tu

Ni kweli kabisa, kama Kingunge aliumwa na mbwa akafa akipatiwa matibabu kwenye hospitali yetu kubwa, Lisu kwa risasi 16 saa hii kampeni hizi Magufuli angeongea kisukuma? Ukiona mtu anatibiwa magonjwa makubwa hapa nchni, ujue kakosa hela ya kwenda nje na sio uzalendo.
 
CCM ndio magwiji wa siasa za Tanzania, mtaelewa tuu.

JPM ANATOSHA
CCM USHINDI NI JADI
 
Nani achague chama chakavu wewe.

Watu tunataka Haki ,Uhuru na Maendeleo ya Watu.
 
Leo mgombea wa CHADEMA Mh Tundu Antipasi Munghwai Lissu alipaswa kufanya mikutano yake ya kampeni mkoani Kilimanjaro. Ratiba iliyotolewa awali ilisema TUNDU atafanya mkutano mkubwa Wilayani Hai.

Taarifa zilizotufikia zinasema kuwa Mh TUNDU ameshindwa kuendelea na kampeni baada ya kuona mapokezi makubwa ya Dkt. Magufuli aliyoyapata Mkoani IRINGA Jana. TUNDU amelazimika kupumzika ili aweze kujitathimini na kutafuta njia mpya ya kumkabili Dkt. Magufuli. TUNDU aliaminishwa IRINGA ni ngome yake, lakini baada ya mtiti wa jana TUNDU amechanganyikiwa.

Wakati Tundu akitafuta njia ya kurudi tena Iringa, mgombea Ubunge wa Jimbo la IRINGA kupitia CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa amefungua program ya kutafuta wafuasi wa kumsaidia mitandaoni.

Mikutano iliyoendelea Leo Ifunda, Mafinga, Nyololo, Makambako na Silali inazidi kumchanganya Tundu.

#JPM2020
KWA UPUMBAVU HUU WEWE NI POLEPOLO AU BUSHIRI HUNA HATA AIBU! LAKINI SISHANGAI MAANA HATA MARINDA HUNA
 
Ukishajenga uwanja unamsaidiaje mkulima asiyepanda ndege au mmachinga azungushaye bidhaa mtaani au Mama ntilie huku mtaani. Wezesha wananchi wapate hela kisha kusanya kodi ujenge miundombinu yako. Unajenga hospital kwani watanzania wote ni wagonjwa?
 
Leo mgombea wa CHADEMA Mh Tundu Antipasi Munghwai Lissu alipaswa kufanya mikutano yake ya kampeni mkoani Kilimanjaro. Ratiba iliyotolewa awali ilisema TUNDU atafanya mkutano mkubwa Wilayani Hai.

Taarifa zilizotufikia zinasema kuwa Mh TUNDU ameshindwa kuendelea na kampeni baada ya kuona mapokezi makubwa ya Dkt. Magufuli aliyoyapata Mkoani IRINGA Jana. TUNDU amelazimika kupumzika ili aweze kujitathimini na kutafuta njia mpya ya kumkabili Dkt. Magufuli. TUNDU aliaminishwa IRINGA ni ngome yake, lakini baada ya mtiti wa jana TUNDU amechanganyikiwa.

Wakati Tundu akitafuta njia ya kurudi tena Iringa, mgombea Ubunge wa Jimbo la IRINGA kupitia CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa amefungua program ya kutafuta wafuasi wa kumsaidia mitandaoni.

Mikutano iliyoendelea Leo Ifunda, Mafinga, Nyololo, Makambako na Silali inazidi kumchanganya Tundu.

#JPM2020
Hovyooo kabisa, kwa taarifa yako muda huu anatokea Rombo anakuja Moshi baada ya kufanya mikutano Hai, Sanya Juu, Kamwanga, Tarakea, Mkuu, Himo.

MATAGA mjipange kudanganya wasiojua.
 
Leo mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi yuko mkoani Njombe na kwa sasa anaongelea afya na Bima ya Afya.

Ameeleza kuwa walianza na vituo vya afya na kinachofata ni bima ya afya, pia ameelezea walishaanza na wamejitahidi kutoa huduma za bure kwa wazee, watoto wenye umri chini ya miaka mitano na wagonjwa wenye magonjwa makubwa wanahudumiwa na serikali.

View attachment 1584449

Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano, wagonjwa kusafirishwa nje wamepungua kwani hata operesheni za moyo zinafanyika Dar es Salaam, operesheni za kubadilisha figo zinafanyika Dodoma na hospitali ya Njombe ikikamilika pia hayo yatafanyika.

Endelea kuwa nami kukujuza yanayojiri Njombe

===========
View attachment 1584452
View attachment 1584451
View attachment 1584450

MAGUFULI: Ndio maana tumekuja tena kuomba kura kwa sababu tunafahamu mikakati, tunafahamu mbinu lakini pesa pia zipo. Hatuitaji fedha za kukopa nje, fedha ziko hapahapa, zilikuwa zimekaliwa na mafisadi, mafisadi tumewabana zinaenda kwa wananchi.

===
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Magufuli amesema sababu ya kugombea Urais kwa Muhula wa Pili ni mipango mizuri waliyonayo kwenye Ilani yao ya Uchaguzi

Kati ya mipango hiyo, ametaja pia kujenga Uwanja wa Ndege Mkoani Njombe, kwa kuwa watu wa Njombe ni wakulima wazuri. Amewatania kwa kusema, ndege pia zitatumika kusafirisha Ulanzi kuwafikia watu wa Dar

Pia, amesema atakamilisha ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Njombe na kuwezesha watanzania wote kuwa na Bima ya Afya na kabla ya kuwa na Bima ya Afya, kwanza wamepanga kujenga Vituo vya Afya, Hospitali na kuongeza bajeti ya kununua madawa

Ameyasema hayo alipokuwa Viwanja vya Polisi, Makambako Mkoani Njombe katika mkutano wa kampeni.

Hongera Sana jpm,nimekusikiliza hata huko mbeya mwanzo mwisho
 
Back
Top Bottom