Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kampeni ya mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Magufuli Bagamoyo, Pwani. Kikwete asema haoni hofu ya CCM kushindwa

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kampeni ya mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Magufuli Bagamoyo, Pwani. Kikwete asema haoni hofu ya CCM kushindwa

Joined
Aug 8, 2013
Posts
10
Reaction score
33
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Dkt. Magufuli yupo mkoa wa Pwani eneo la Bagamoyo na anaeongea sasa ni aliyekuwa mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete. Pia kwenye mkutano wa leo yupo Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

Ridhiwani kawaomba Wanachalinze wenzake kumchagua Dkt. Magufuli kwani miaka mitano imekuwa mafanikio kwao ikiwemo hospitali ya wilaya Chalinze tangu Uhuru ambayo inamaliziwa. Pia barabara nne kutoka Kibaha kwenda Chalinze zinazoanza kujengwa. Ridhiwani amesema yeye kama Mbunge wao anamuamini sana Dkt. Magufuli.
=======

JAFFO: Wilaya ya Kisarawe ilikuwa na historia haina maji, ametupa mradi wa bilioni 10.6, watu wa Kisarawe leo hii maji wanatumia na kusaza zaidi ya lita milioni 6 zinaingia kwa siku na matumizi lita milioni 1.2 na ndio maana Dawasa leo hii wanahamisha yale maji kuyatoa Kisarawe kwenda Kazimzungwi, Masaki, Kibuta mpaka Chang'ombe A.

Mwisho ndugu Jaffo amesema Dkt. Magufuli mkoa wa Pwani ameutendea haki ikiwemo hospitali za wilaya, vituo vya afya, amekarabati shule zote kongwe, elimu bure Pwani na nchi nzima zaidi ya bilioni 23.86 na trilioni 1.31 mpaka leo hivyo tarehe 28 waende wakampe kura Dkt. John Pombe Magufuli kwa wema wa ilani ya chama cha mapinduzi.

MAGUFULI NJIANI BUNJU:
Magufuli:
Tumetenga bilioni 74 tutaanza kuyasambaza maji Bunju A na Bunju B, ahadi zangi mimi si za uongo, msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Ninawaomba tarehe 28 ndugu zangu wa Bunju mfanye mabadiliko.

Mimi ni mtumishi wenu, ninawapenda watu wote mpaka wamachinga mimi ni wangu. Nataka tufanye mabadiliko ya kweli na ninyi wanakawe ninawaomba sana tarehe 28 mkafanye mabadiliko ili nikija hapa mje mniulize kwamba mheshimiwa ulituahidi, tulifanya ulichotuomba, mbona hujatimiza ili dhamira yangu ikanisute.

Ninawaomba vijana msidanganywe na vitu vya bure vya kuambiwa mjipange barabarani. Zipo nchi ambazo mapaka leo zipo kwenye vita, amani ni kitu kikubwa mno. Usijiangalie wewe tu kama kijana kwa sababu unaweza ukakimbia, muangalie mdogo wako uliemuacha nyumbani, mama yako, babu yako, muangalie bibi yako kama anaweza akakimbia kama wewe, ni lazima tuitunze amani yetu.

Tanzania ina asali na mnafahamu watu wanaokwenda kuvuna asali wanachofanya, hawajali ile asali imetengenezwa na nyuki. Anaenda na moto na moshi, wanachoma nyuki wote wanakufa, wao wanachukua asali. Hivyo ndivyo wanavyoiona mabeberu Tanzania.

Tanzania ina kila kitu, haijali maisha yenu na ndio maana tulipopata korona walizungumza tutakuwa tunaokota maiti barabarani, nikasema hili halitawezekana kwa sababu Mungu wetu yupo na Mungu anatupenda wote watanzania.

Wapo wengine wanaowashawishi kuandamana, nimecheki wana tiketi zao za kwenda Ulaya. Kwa hiyo wanawaacha hapa mnaumizana, wao wanaondoka. Angalieni nchi zilizoingia kwenye migogoro. Sifahamu watanzania kama mnataka mambo ya kumwaga damu, tunahitaji amani.

Ukiona mtu anakwambia msipofanyikia hivi, ingieni barabarani. Yule siku ya kumkomesha ni tarehe 28, zipo nchi zimeteseka, leo zinalia sitaki kutoa mifano. Zipo nchi hata za Ulaya ambazo mpaka leo zinapigana. Tanzania nchi hii ni tajiri na mimi siku zote nimekuwa nikiwaambia, nchi hii ni tajiri na kila mtu anaitazama.

Nitasikitika sana kuona watanzania wanaumizana kwa sababu ya suala la uchaguzi, tuchague salama na najua wa kushindwa wameshajijua wanashindwa wanataka waache vurugu hapa, msikubali kamwe, akikwambia kwenda kuandamana, mwambie aende yeye, mke wake na baba yake. Kwamba unataka tukaandamane, nenda wewe pale kaandamane, sisi tutakuwa tunakuangalia, utaona kama ataenda, wasiwatumie nyinyi kama ngao.

=========

05:00 ASUBUHI; DKT. MAGUFULI AMEINGIA VIWANJA VYA MWANAKALENGE, BAGAMOYO

POLEPOLE:
Watu hawa Watanzania na wanaCCM walikuwepo hapa tangu saa 12 asubuhi, shauku yao ya kukusikia imekuwa kubwa sana, watu hawa wako tayari kukusikiliza wewe. Kwa ruhusa yako moja kwa moja kwa kuwatambua viongozi watakaotuongoza kwa sala na dua fupi. Tunaye Sheikh Khamis Mtupa, sheikh mkuu wa mkoa wa Pwani na tunae baba Padri Beno kikondo kutoka kanisa Katoliki, naomba kumkaribisha sheikh Hamis Mtupa, sheikh mkuu wa mkoa wa Pwani.

TAMKO LA MUFTI
Sheikh MTUPA:
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa niaba ya mheshimiwa Mufti na Sheikh mkuu wa Tanzania na kwa niaba ya Waislamu wa mkoa wa Pwani napenda kukanusha rasmi kupitia hadhara yako hii tukufu, Waislamu wa mkoa wa Pwani na Tanzania kwa ujumla hatujafanya makubaliano yoyote kuanzia ngazi ya msikiti, kata, wilaya, mkoa, Taifa kwamba kura za waislamu zitakwenda kwa mgombea fulani. Kauli hiyo ipuuzwe na izikwe karibuni.

KIKWETE: Mimi mwanasiasa unasema nisome salam fupi, una hatari wewe! Ndugu mgombea mie Bagamoyo ni kwetu kwa hiyo niliposikia unakuja kwenye kampeni kwetu na mie ni Mwanabagamoyo kindakindaki kwa kuzaliwa nikaona siwezi kukosa lazima niwepo kuungana na Wanabagamoyo wenzangu, Wanapwani wenzangu kukukaribisha, karibu Pwani, karibu Bagamoyo.

Nakupa pole kwa kazi kubwa unayoifanya ya kampeni, nimeifanya kwa hiyo naijua adha yake. Naujua ugumu wake lakini naijua raha yake na raha yake ni hii (anaonyesha watu). Unakuwa umechoka sana lakini ukiwakuta watu wamejaa, wana furaha, nyuso zao zina bashasha, roho yako inakuwa baridiii.

Pole, hongera lakini mpaka sasa umefanya kazi nzuri, umeendesha kampeni vizuri na mimi sina wasiwasi utashinda, utasinda sana na chama chetu kitashinda, kitaendelea kuongoza taifa letu. Siioni hofu wala sioni sababu ya CCM kushindwa au mgombea wetu wa Urais kushindwa au wagombea wetu wa ubunge wengi kushindwa.

Hilo silioni kwa sababu sioni sababu ya hilo lakini kwanini? Kwa sababu chama chetu chini ya uongozi wako, kimeiongoza vizuri nchi yetu, mambo mengi mazuri yamefanyika na wananchi hilo wanatambua na kwa hilo shukrani yao wataionyesha tarehe 28 kwenye sanduku la kura.

Endelea kupambana lakini andelea ukiamini hakuna litakaloharibika. Tanzania ilivyo leo sivyo ilivyokuwa 2015 wakati nakukabidhi nchi, tumepiga hatua kubwa ya maendeleo. Nchi ni tulivu, jamani tunataka nini tena? Nani kama CCM, nani kama Magufuli? Asante sana mheshimiwa Rais, karibu sana.
 
Ridhiwani ni mbunge tayari ana subiri kupewa barua na tume.
 
Kuna mabasi kama yote toka Kisarawe, DSM, Chalinze, na Morogoro plus nyomi ya wasanii. Kwahiyo watu mnaowaona kwenye TV siyo wa Bagamoyo.

Sambamba na hilo shule zote za msingi na sekondari zimefungwa leo hapa Bagamoyo. Na walimu wamewekewa daftari la mahudhurio uwanjani. Yaani badala ya kuwahi kuripoti shuleni wanaripoti uwanjani.

CCM HOIIIIIIIIIII!!
 
Kuna mabasi kama yote toka Kisarawe, DSM, Chalinze, na Morogoro plus nyomi ya wasanii. Kwahiyo watu mnaowaona kwenye TV siyo wa Bagamoyo.

Sambamba na hilo shule zote za msingi na sekondari zimefungwa leo hapa Bagamoyo. Na walimu wamewekewa daftari la mahudhurio uwanjani. Yaani badala ya kuwahi kuripoti shuleni wanaripoti uwanjani.

CCM HOIIIIIIIIIII!!
Acha uongo.

Mimi ni mwalimu katika shule moja maeneo hayo.

Unachoongea si kweli.
 
Mbona naona hizi kauli zimejaa vitisho tu hakuna la ziada?

Mbona mwenzie kasema akishindwa kwa haki atakuwa wa kwanza kujitangaza kwamba kashindwa, yeye mbona hazungumzi lolote kama anaipenda kweli amani?

Azungumzie neno HAKI then atakuwa ameeleza kila kitu!!
 
Kumbe mnalive yenu huku?

Huko kwingine dunia imesimama inapiga makofi kwa Lissu
 
Back
Top Bottom