kweki chadema media yani mtu mmoja apige wananchi wote[HASHTAG]#UchaguziMdogo[/HASHTAG] Kata ya Ikweha, wananchi wanapigwa na mbunge wa CCM Mahamud Mgimwa na kuwatisha na bastola wasishiriki uchaguzi.
Kata ya Ikweha, waliotishiwa bastola na Mbunge Mahamud Mgimwa ni Mratibu Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga.
Chanzo. Chadema Media
kwa arusha hayo yalitegemewa. gambo amesimama imara kuhakikisha anabomoa chadema arusha kwa kumfunga LEMA na hata kupambana na madiwani wa arusha. kwa tume hii chini ya wakurugenzi hawa makada wapinzani wasahau.Acha Mapovu yawatoke Chadomo wamekung'utwa mpaka kata ya Matevez Arusha.
Ndo faida ya chama kununuliwa
SurePole wewe pekeyako
Mimi ni binadamu
Baki na unyama wako
Lowassa fisadi..CDMMkuu kama magu hakushinda, kwanini lawama mnawapa wananchi kwamba waliichagua ccm...Na kudai acha waisome namba?
Unajua watanzania ni watu wa ajabu sana. Ninyi wapinzani kamwe hamtashinda kwa mfumo huu wa uendeshaji uchaguzi ulivyo. Tume ya uchaguzi sio taasisi huru hawawezi wakasimamia haki hawa. Yaani wasimamizi wa uchaguzi ni makada wa chama tawala halafu nyie wapinzani mnategemea mtashinda?
Mkurugenzi wa halmashauri ambae ni kada wa chama tawala ndie msimamizi wa uchaguzi!!!
Mkuu wa wilaya ambae anatajwa kwamba ndie mwnyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ni kada wa chama tawala.
Amkeni kutoka kwenye usingizi, agenda yenu namba moja iwe ni mabadiliko ya katiba hasa eneo hili la uchaguzi.
Uwanja wa kwao
Refa wa kwao
Washika vibndera wa kwao
Kamisaa wa kwao
Halafu mnategemea kushinda????
Usikimbie kama huna breki
mkuu huo ni uwongo. fuatilia taarifa zako vizurikatika Kata 22 zilizofanya uchaguzi mdogo Chama cha Mapinduzi kimeibuka na ushindi wa kishindo kwa kushinda kata 21 huku chama cha demokrasia na maendeleo kikiambulia kata moja pekee mkoani Manyara katika kata ya Duru.
Pia Chama cha Mapinduzi kimeibuka na ushindi mnono katika Jimbo LA Dimani Zanzibar dhidi ya mgombea wa muungano wa ukawa.
Mkuu hiki ulichokiandika ni kikubwa sana kwa akili yake ndogo kuelewa.Vyama vingi havikuja tuwe na ushabiki wa kama Yanga na Simba. Ila ni kuleta fikra kinzani chanya zitakazotufikisha mbali kijamii na kiuchumi. Jambo unalotakiwa kufurahia ni kuwa sera au fikra zako zitatekelezwa sio chama chako kimeshinda. Kwa kuwa hatuna Dira kama nchi hata uwepo wa vyama umekuwa ni deal za kujipatia maisha tu lakini si kufikisha maendeleo kwa wananchi. Pole Tanzania pole Africa tuna miaka mingi sana ya kuwa binadamu tutakaolewa nini maana ya
Mimi sijawahi kusikia CCM wakisema Lowasa siyo fisadi.Lowassa fisadi..CDM
Lowassa siyo fisadi .. CCM
Lowassa fisadi...CCM
Lowassa siyo fisadi...CDM
Tushike lipi?
Mwenye majibu sahihi tafadhali yasiyo ya kisiasa.
ObligadoMkuu hiki ulichokiandika ni kikubwa sana kwa akili yake ndogo kuelewa.
Dharau zenu ndio zinazofanya ccm iendelee kushinda. Siajabu mkaja na threads kutukana waliopiga kura.Bado kuna binadamu mwenye akili timamu anapanga foleni kuipigia kura ccm,!!! maajabu haya
Hivi hapa maana ya UKAWA ni nini sasa?Matokeo Rasmi kata ya Isagehe-Kahama ni km ifuatavyo;
-NCCR-MAGEUZI-KURA=11
-CHAUMA-KURA=11
-C.U.F-KURA=30
-CHADEMA-KURA=439
-ACT-WAZALENDO-KURA=578
-C.C.M-KURA=1562.
Kura zilizoharibika ni -49.
Leo ndo leo uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani Zanzibar na uchaguzi wa madiwani kata 20 Tanzania bara.
Ni chaguzi zitazotoa mwelekeo na mabadiliko na ukubalikaji wa vyama tangu uchaguzi mkuu wa 2015.
Karibuni tupeane updates na matukio yanayojiri huko.
.......Updates...........
* Uchaguzi wa Ubunge unafanyika kwenye jimbo la Dimani, Wilaya ya Magharibi “B”, Mkoa wa Mjini Magharibi – Zanzibar
Uchaguzi wa madiwani unafanyika kwenye kata Ishirini (20) katika Halmashauri Kumi na Tisa (19) za Tanzania Bara, kata hizo ni...
1. Ngarenanyuki (Meru DC, Arusha),
2. Igombavanu (Mufindi DC, Iringa),
3. Ikweha (Mufindi DC, Iringa),
4. Kiwanja cha Ndege (Morogoro MC, Morogoro),
5. Ihumwa(Dodoma MC, Dodoma),
6. Kijichi (Temeke MC, Dar es Salaam),
7. Kahumulwa (Sengerema DC, Mwanza)
8. Maguu (Mbinga DC, Ruvuma),
9. Ng’hambi (Mpwapwa DC, Dodoma),
10. Kimwani (Muleba DC, Kagera),
11. Kinampundu (Mkalama DC, Singida),
12. Isagehe (Kahama TC, Shinyanga),
13. Kasansa (Mpimbwe DC, Katavi),
14. Duru (Babati DC, Manyara),
15. Malya (Kwimba D.C, Mwanza),
16. Misugusugu (Kibaha TC, Pwani),
17. Mateves (Arusha D.C, Arusha),
18. Nkome (Geita DC, Geita),
19. Lembeni (Mwanga DC, Kilimanjaro) na
20. Tanga (Songea MC, Ruvuma)
--
siyoi koroi, Uchaguzi udiwani Kata ya Ngarenanyuki DED na ccm wapora daftari la wapiga kura.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bwana Christopher Kazeri anatembelea vituo akiwa ameambatana na viongozi wa ccm.
Sheria za uchaguzi haziruhusu viongozi wa vyama vya siasa kupiga kambi kwenye vituo vya uchaguzi.
Hii imeweza kutokea Ngarenanyuki tu mkurugenzi wa halmashauri ambaye ni msimamizi wa uchaguzu kutembea na viongozi wa ccm.
mkurugenzi akiwa ameambatana na makada wa ccm wamewanyang'anya mawakala wa vyama daftari lenye majina ya wapiga kura.
Safari ya demokrasia kwa nchi yetu bado sana.
Hii haikubaliki popote.
Tume ya taifa ya uchaguzi kwa mtindo huu huu uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki.
--
Francis12, UPDATES MCHAGUZI MDOGO JIMBO LA DIMANI Z'BAR.
Kumetokea mgogoro kati ya mawakala wa CUF na Askari Polisi. Hali hii imepelekea mawakala wa CUF kuondolewa kwa nguvu kwenye vyumba vya kupigia kura na hivyo mawakala wa CCM kubaki peke yao.
Sababu za mgogoro huu ni kama ifuatavyo:
-Mawakala wa CUF amegundua baadhi ya masanduku yamejazwa kura ambazo zimeshapigwa tiki kwa mgombea wa CCM.
-Mawakala wa CUF wamegundua kuwa kuna watu hawamo ndani ya daftari la kupiga kura ila wamekuja kupiga kura na wameruhusiwa kupiga licha ya majina yao kukosekana kwenye daftari.
-Chumba number 6 kituo cha Kibondeni, imegundilikana kwamba masunduku yote yaliyopo yamejazwa kura ambazo zimeshapigwa tayari.
-Wapiga kura wengi jimbo la Dimani ni hewa.
-Police wameanza kupiga watu maeneo ya Fuoni kituo cha Kibondeni baada ya watu hao kudai kuna kura feki kwenye kituo hicho.
-Katika kituo hicho cha Fuoni mabasi yamekua yakisomba watu na kuwaleta kupiga kura. Watu hao si wakazi wa jimbo la Dimani. Picha hapo chini inaonesha moja ya mabasi yanayotumika kusomba watu na kuwapeleka vituoni kupiga kura.
==========
MATOKEO YA AWALI
==========
Jimbo la Dimani Zanzibar
View attachment 462825
Unajua watanzania ni watu wa ajabu sana. Ninyi wapinzani kamwe hamtashinda kwa mfumo huu wa uendeshaji uchaguzi ulivyo. Tume ya uchaguzi sio taasisi huru hawawezi wakasimamia haki hawa. Yaani wasimamizi wa uchaguzi ni makada wa chama tawala halafu nyie wapinzani mnategemea mtashinda?
Mkurugenzi wa halmashauri ambae ni kada wa chama tawala ndie msimamizi wa uchaguzi!!!
Mkuu wa wilaya ambae anatajwa kwamba ndie mwnyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ni kada wa chama tawala.
Amkeni kutoka kwenye usingizi, agenda yenu namba moja iwe ni mabadiliko ya katiba hasa eneo hili la uchaguzi.
Uwanja wa kwao
Refa wa kwao
Washika vibndera wa kwao
Kamisaa wa kwao
Halafu mnategemea kushinda????
Usikimbie kama huna breki
UPAWAHivi hapa maana ya UKAWA ni nini sasa?