Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

[HASHTAG]#UchaguziMdogo[/HASHTAG] Kata ya Ikweha, wananchi wanapigwa na mbunge wa CCM Mahamud Mgimwa na kuwatisha na bastola wasishiriki uchaguzi.
Kata ya Ikweha, waliotishiwa bastola na Mbunge Mahamud Mgimwa ni Mratibu Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga.
Chanzo. Chadema Media
kweki chadema media yani mtu mmoja apige wananchi wote
 
Acha Mapovu yawatoke Chadomo wamekung'utwa mpaka kata ya Matevez Arusha.

Ndo faida ya chama kununuliwa
kwa arusha hayo yalitegemewa. gambo amesimama imara kuhakikisha anabomoa chadema arusha kwa kumfunga LEMA na hata kupambana na madiwani wa arusha. kwa tume hii chini ya wakurugenzi hawa makada wapinzani wasahau.
 
Mwenye empty talks nani? Upinzani? Na nyie empty ballots?
 
Unajua watanzania ni watu wa ajabu sana. Ninyi wapinzani kamwe hamtashinda kwa mfumo huu wa uendeshaji uchaguzi ulivyo. Tume ya uchaguzi sio taasisi huru hawawezi wakasimamia haki hawa. Yaani wasimamizi wa uchaguzi ni makada wa chama tawala halafu nyie wapinzani mnategemea mtashinda?

Mkurugenzi wa halmashauri ambae ni kada wa chama tawala ndie msimamizi wa uchaguzi!!!

Mkuu wa wilaya ambae anatajwa kwamba ndie mwnyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ni kada wa chama tawala.

Amkeni kutoka kwenye usingizi, agenda yenu namba moja iwe ni mabadiliko ya katiba hasa eneo hili la uchaguzi.

Uwanja wa kwao
Refa wa kwao
Washika vibndera wa kwao
Kamisaa wa kwao

Halafu mnategemea kushinda????

Usikimbie kama huna breki
 
Matokeo yaliyotufikia toka kijichi ni km iguatavyo
Ccm 61%
CUF 22%
CDM 14%
Wapiga kura walikuwa 5000 na kidogo kati ya wapiga kura zaidi ya elfu 20 waliotarajiwa
Source wakala mkuu chadema
Kassim Bingwe
 
Unajua watanzania ni watu wa ajabu sana. Ninyi wapinzani kamwe hamtashinda kwa mfumo huu wa uendeshaji uchaguzi ulivyo. Tume ya uchaguzi sio taasisi huru hawawezi wakasimamia haki hawa. Yaani wasimamizi wa uchaguzi ni makada wa chama tawala halafu nyie wapinzani mnategemea mtashinda?

Mkurugenzi wa halmashauri ambae ni kada wa chama tawala ndie msimamizi wa uchaguzi!!!

Mkuu wa wilaya ambae anatajwa kwamba ndie mwnyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ni kada wa chama tawala.

Amkeni kutoka kwenye usingizi, agenda yenu namba moja iwe ni mabadiliko ya katiba hasa eneo hili la uchaguzi.

Uwanja wa kwao
Refa wa kwao
Washika vibndera wa kwao
Kamisaa wa kwao

Halafu mnategemea kushinda????

Usikimbie kama huna breki

Jakaya aliwalatea Katiba Mpya yenye Tume huru ya Uchaguzi wakataa kuendelea na Mchakato wa Katiba Mpya akawaita Ikulu akawabembeleza na Chai isiyo na Pipi Bali bites wakapewa wakakubali kuendelea na Katiba Mpya.

Waliporudi Bungeni akili Wakaacha Guest house wakamkabidhi Lipumba awaongoze nae akawaambia wasuse waondoke na kweli Wakaondoka!

Pamoja na Kususa na Jk akijua anakabidhi Nchi kwa Mtata akawaomba wamuunge Mkono walau tupige kura ya Maoni kabisa na Kazi ya Rais ajae iwe kutekeleza tu ya Katiba Mpya wakakataa nae kwa Uungwana wake akaridhia japo kwa Shingo Upande!

Wapinzani wangekuwa na Think tanks za Kutosha wakati wa Jk wangeweka Misingi mingi na mizuri sana ya Demokrasia Tatizo ni kuwa Wote waliwekeza akili zao kwa Lipumba na Tundu Lissu kuwaamulia cha kufanya!
 
katika Kata 22 zilizofanya uchaguzi mdogo Chama cha Mapinduzi kimeibuka na ushindi wa kishindo kwa kushinda kata 21 huku chama cha demokrasia na maendeleo kikiambulia kata moja pekee mkoani Manyara katika kata ya Duru.
Pia Chama cha Mapinduzi kimeibuka na ushindi mnono katika Jimbo LA Dimani Zanzibar dhidi ya mgombea wa muungano wa ukawa.
mkuu huo ni uwongo. fuatilia taarifa zako vizuri
 
Vyama vingi havikuja tuwe na ushabiki wa kama Yanga na Simba. Ila ni kuleta fikra kinzani chanya zitakazotufikisha mbali kijamii na kiuchumi. Jambo unalotakiwa kufurahia ni kuwa sera au fikra zako zitatekelezwa sio chama chako kimeshinda. Kwa kuwa hatuna Dira kama nchi hata uwepo wa vyama umekuwa ni deal za kujipatia maisha tu lakini si kufikisha maendeleo kwa wananchi. Pole Tanzania pole Africa tuna miaka mingi sana ya kuwa binadamu tutakaolewa nini maana ya
Mkuu hiki ulichokiandika ni kikubwa sana kwa akili yake ndogo kuelewa.
 
Lowassa fisadi..CDM
Lowassa siyo fisadi .. CCM
Lowassa fisadi...CCM
Lowassa siyo fisadi...CDM

Tushike lipi?
Mwenye majibu sahihi tafadhali yasiyo ya kisiasa.
Mimi sijawahi kusikia CCM wakisema Lowasa siyo fisadi.
 
Bado kuna binadamu mwenye akili timamu anapanga foleni kuipigia kura ccm,!!! maajabu haya
Dharau zenu ndio zinazofanya ccm iendelee kushinda. Siajabu mkaja na threads kutukana waliopiga kura.
 
Leo ndo leo uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani Zanzibar na uchaguzi wa madiwani kata 20 Tanzania bara.

Ni chaguzi zitazotoa mwelekeo na mabadiliko na ukubalikaji wa vyama tangu uchaguzi mkuu wa 2015.

Karibuni tupeane updates na matukio yanayojiri huko.

.......Updates...........

* Uchaguzi wa Ubunge unafanyika kwenye jimbo la Dimani, Wilaya ya Magharibi “B”, Mkoa wa Mjini Magharibi – Zanzibar

Uchaguzi wa madiwani unafanyika kwenye kata Ishirini (20) katika Halmashauri Kumi na Tisa (19) za Tanzania Bara, kata hizo ni...

1. Ngarenanyuki (Meru DC, Arusha),
2. Igombavanu (Mufindi DC, Iringa),
3. Ikweha (Mufindi DC, Iringa),
4. Kiwanja cha Ndege (Morogoro MC, Morogoro),
5. Ihumwa(Dodoma MC, Dodoma),
6. Kijichi (Temeke MC, Dar es Salaam),
7. Kahumulwa (Sengerema DC, Mwanza)
8. Maguu (Mbinga DC, Ruvuma),
9. Ng’hambi (Mpwapwa DC, Dodoma),
10. Kimwani (Muleba DC, Kagera),
11. Kinampundu (Mkalama DC, Singida),
12. Isagehe (Kahama TC, Shinyanga),
13. Kasansa (Mpimbwe DC, Katavi),
14. Duru (Babati DC, Manyara),
15. Malya (Kwimba D.C, Mwanza),
16. Misugusugu (Kibaha TC, Pwani),
17. Mateves (Arusha D.C, Arusha),
18. Nkome (Geita DC, Geita),
19. Lembeni (Mwanga DC, Kilimanjaro) na
20. Tanga (Songea MC, Ruvuma)
--
siyoi koroi, Uchaguzi udiwani Kata ya Ngarenanyuki DED na ccm wapora daftari la wapiga kura.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bwana Christopher Kazeri anatembelea vituo akiwa ameambatana na viongozi wa ccm.

Sheria za uchaguzi haziruhusu viongozi wa vyama vya siasa kupiga kambi kwenye vituo vya uchaguzi.

Hii imeweza kutokea Ngarenanyuki tu mkurugenzi wa halmashauri ambaye ni msimamizi wa uchaguzu kutembea na viongozi wa ccm.

mkurugenzi akiwa ameambatana na makada wa ccm wamewanyang'anya mawakala wa vyama daftari lenye majina ya wapiga kura.

Safari ya demokrasia kwa nchi yetu bado sana.
Hii haikubaliki popote.

Tume ya taifa ya uchaguzi kwa mtindo huu huu uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki.

--
Francis12, UPDATES MCHAGUZI MDOGO JIMBO LA DIMANI Z'BAR.

Kumetokea mgogoro kati ya mawakala wa CUF na Askari Polisi. Hali hii imepelekea mawakala wa CUF kuondolewa kwa nguvu kwenye vyumba vya kupigia kura na hivyo mawakala wa CCM kubaki peke yao.

Sababu za mgogoro huu ni kama ifuatavyo:

-Mawakala wa CUF amegundua baadhi ya masanduku yamejazwa kura ambazo zimeshapigwa tiki kwa mgombea wa CCM.

-Mawakala wa CUF wamegundua kuwa kuna watu hawamo ndani ya daftari la kupiga kura ila wamekuja kupiga kura na wameruhusiwa kupiga licha ya majina yao kukosekana kwenye daftari.

-Chumba number 6 kituo cha Kibondeni, imegundilikana kwamba masunduku yote yaliyopo yamejazwa kura ambazo zimeshapigwa tayari.

-Wapiga kura wengi jimbo la Dimani ni hewa.

-Police wameanza kupiga watu maeneo ya Fuoni kituo cha Kibondeni baada ya watu hao kudai kuna kura feki kwenye kituo hicho.

-Katika kituo hicho cha Fuoni mabasi yamekua yakisomba watu na kuwaleta kupiga kura. Watu hao si wakazi wa jimbo la Dimani. Picha hapo chini inaonesha moja ya mabasi yanayotumika kusomba watu na kuwapeleka vituoni kupiga kura.

==========

MATOKEO YA AWALI

==========

Jimbo la Dimani Zanzibar
View attachment 462825

Chama cha upinzani ni kupinga kila kitu maana kwa akili zao za mchangani wenye uwezo wa kushinda ni wao, chama tawala kikishinda ni fujo na kudai wameibia. Puuuuu!!!!!
 
Unajua watanzania ni watu wa ajabu sana. Ninyi wapinzani kamwe hamtashinda kwa mfumo huu wa uendeshaji uchaguzi ulivyo. Tume ya uchaguzi sio taasisi huru hawawezi wakasimamia haki hawa. Yaani wasimamizi wa uchaguzi ni makada wa chama tawala halafu nyie wapinzani mnategemea mtashinda?

Mkurugenzi wa halmashauri ambae ni kada wa chama tawala ndie msimamizi wa uchaguzi!!!

Mkuu wa wilaya ambae anatajwa kwamba ndie mwnyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ni kada wa chama tawala.

Amkeni kutoka kwenye usingizi, agenda yenu namba moja iwe ni mabadiliko ya katiba hasa eneo hili la uchaguzi.

Uwanja wa kwao
Refa wa kwao
Washika vibndera wa kwao
Kamisaa wa kwao

Halafu mnategemea kushinda????

Usikimbie kama huna breki

Nadhani ifike mahali watanzania tujue kuwa Haya ni matumizi mabaya ya kodi zetu. Uchaguzi gani huu, si wateuliwe kutoka chama tawala hatuna sababu ya kuharibu fedha za umma wakati chama tawala kimeshateua viongozi wake?
 
Back
Top Bottom