Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Maalim Self yupo ktk hali ngumu sana, simulizi zake za "Yesu yu jiraani Kuja" haziaminiwi tena na watu wa Visiwa. Sasa ifike 2020 hawajamuona, watakugawana
 
Haki haiombwi hata siku moja. Hapa ni africa na mna deal na waafrica hawa sio wazungu hawa ni ccm ni kina barrow ni kina qaddafi ni kina mugabe.
Sasa mkidhani mtawashinda kwenye box la kura msahau.
Woga wetu ndio umaskini wetu
 
Kuna uchaguzi wa ZEC, huo ndio walioususa wakati ule. Huu ni wa NEC. Tulia kidogo uwe unapata nafasi ya kujisomea.
Hapana Mkuu Hata Uchaguzi wa NEC tulisusa wa Jimbo la Kijitoupele Uliofanyika march 20 , 2016
Kwa kweli CUF ni chama Cha Seif kwa iyo atachosema hata kama hakina maslah ni kufatwa tu vyenginevyo utafukuzwa chama
 
Bado kuna baadhi ya wananchi na hasa wapinzani wanaamini kama mabadiliko Tanzania yataletwa na waliokuwa viongozi wakuu waandamizi ndani ya CCM na serikali ya CCM ambao ni Edward Lowassa na Maalim Seif.

Ikumbukwe kuwa Lowassa na Maalim Seif wanalishwa, kuvalishwa na kulindwa na serikali ya CCM. Hii ina maana na mantiki kubwa sana kwenye siasa za nchi za Afrika. Yaani wanakaa kupanga mikakati ya kuiangusha serikali ya CCM huku wakilindwa na maofisa waliotumwa kufanya kazi na Rais.

Aliyewahi kusema ‘’wajinga ndio waliwao’’ hakukosea kwa sababu hata Tanzania katika uwanja wa siasa kuna wajinga wengi sana ambao ''wanaliwa'' na baadhi ya wanasiasa ambao ni political entrepreneur.

Nilikuwa ninashangaa na kucheka kila nikisoma mabandiko ya baadhi ya watu wakisema ‘’Uchaguzi mdogo wa ubunge na madiwani katika kata 20 ni kipimo cha uongozi wa Rais Magufuli’’.

Nikawa ninajiuliza, kama chaguzi ndogo ndio mizani ya kipimio cha utendaji wa Rais Magufuli kwa kutumia mawe ya mizani yanayoitwa Lowassa na Maalim Seif, basi itakuwa ni kupoteza muda kwa sababu haya mawe hayafai kutumika katika mizani. Haya ni mawe ya kugushi (fake).

Matokeo ya Uchaguzi mdogo wa Mbunge na Udiwani katika kata 20 tumeyasikia na kuyaona. Ni kipigo na kilio kwenye kambi za upinzani.

Ninafahamu kuna baadhi ya watu watakuja na nyimbo zenye chorus zinazosema uchaguzi haukuwa huru na haki kama vile wanalazimishwa kuingia kwenye chaguzi.

Mwaka 2015 wakati vyama vya upinzani vinapanga mkakati wa kukabiliana na CCM, Lowassa alijitokeza na kuwaambia kazi hiyo wamwachie yeye, wao kazi yao iwe ni kupiga kura na kurudi nyumbani. Matokeo yake tunayafahamu.

Huko Zanzibar, wakati CUF inaendelea kufanya vizuri wakati wa zoezi la kuhesabu kura, Maalim Seif alijitokeza na kuvuluga uchaguzi baada ya kujitangaza mshindi kinyume cha sheria ya uchaguzi. Yaliyojiri baadaye ni historia.

Kwa sasa Maalim Seif amewashawishi tena CUF waingie kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Dimani, Zanzibar wakati huku Bara, Lowassa akiwashawishi CHADEMA waingie tena kwenye uchaguzi wa madiwani wakati hawajajipanga ipasavyo. Matokeo yake tumeyaona. Wamepata kipigo kama cha mwizi!

Waingereza hupenda kusema, “It is difficult to see the picture when you are inside of the frame.”

Wajinga wataendelea kuimba Mabadiliko Lowassa, Lowassa Mabadiliko huku CCM ikiendelea kuwapa kipigo cha kisiasa katika chaguzi mbali mbali.
 
ACHA KUJIDANGANYA WEWE UNAYEKURUPUKA.

Wala usifikiri wanachadema na wanaCUF original wanachonganishwa na huu uzushi wako hapa

Una akili ndogo sana.

Ulisikia hotuba ya LOWASSA jana ilivyo strong? Iliwaingia sana vijana wa Lumumba.


Hahaha...vijana wa CCM mnatia huruma na UZUSHI wenu wa kila siku.

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Wapinzani.wamelowanishwa mbaya.
Chaliiiiiiiiii.

Na hapo bado 2020 Nimejiandaa kumsupport JPM kuanzia humu JF
mpaka majukwaaani.

Nawahakikishia majimbo.yote kanda ya ziwa yatarudi ccm
Wale ambao kweli wanapigania ''mabadiliko'' wanahitaji kutoa nje ya fikra zilizowafunga ili waweze kuona ukweli wa kinachoendelea ndani ya vyama vyao.
 
Hawa jamaa wasipojipanga 2020 wanapotea kwenye siasa, kumbuka matunda ya kazi anazofanya Magufuli na serikali yake yatakuwa yameanza kuonekana hata kwa watu wasio na uwezo wa kuyaona kwa sasa.
Tuliambiwa uchaguzi mdogo wa ubunge na madiwani ni kipimo cha uongozi wa Rais Magufuli kama anakubalika au la!
 
Wale ambao kweli wanapigania ''mabadiliko'' wanahitaji kutoa nje ya fikra zilizowafunga ili waweze kuona ukweli wa kinachoendelea ndani ya vyama vyao.

Wanafikiri kuzungusha mikono ndio maendeleo. Wataishia kuandika na kukodoa mimacho Jf, wananchi wanaona nini rais wao anafanya.

Wananchi wanaona namna viongozi waandamizi chadema walivo wapiga dili.

Nani wa kumwamini Mbowe, Nani wa Kumwamini Lowasa.

Acha dozi iwaingie
 
Kanda ya ziwa IPI wakati njaa inawua wananchi?

Dogo ukianzia Shelui, Igunga, Nzega, Mwanhuzi,Tinde,Kagongwa,Isaka,Bukene,Lunzewe, katoro,Kasamwa, Katunguru, lamadi, Kiabakari,Majita, Kiogoto, Rorya, kote vyakula.vipo vya kutosha njoo ujionee mnatunga stori.za.kusadikika nani atawasikiliza
 
Back
Top Bottom