Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Haki haiombwi hata siku moja. Hapa ni africa na mna deal na waafrica hawa sio wazungu hawa ni ccm ni kina barrow ni kina qaddafi ni kina mugabe.
Sasa mkidhani mtawashinda kwenye box la kura msahau.
Woga wetu ndio umaskini wetu

Hamkumuweza JK, JP mtamuweza wapi?
 
mbona chagadema mpo kimya au uchaguzi huu mmevurumishiwa za Uso? sio kawaida yenu domo kutulia hivi.!!!
 
Kila thread mods wanaziunganisha, tuwekeeni basi Matokeo ya kata zote bara zilizo fanya uchaguzi
 
Pamoja na yote hayo, wewe unaona leo hii tuna uongozi bora au unawalaumu "wapinzani" kwa kutuangusha na kutuharibia misingi ya demokrasia ya kweli kwa kutomsikiliza JK?

Katiba Mpya waliyoisusia ilikuwa na Tume huru na Haki ya kuhoji Ushindi wa Rais Madarakani.
Jakaya alikusudia Kuwasaidia Wapinzani Indirect na ikiwezekana wapate Wabunge wengi ikiwezekana iundwe Serikal ya Umoja wa Kitaifa Kama alivyowafanyia Zanzibar 2010lakin walipoteza hiyo bahati kwa kususia Katiba Mpya na kumchukua Lowassa Kama Mgombea wao!
 
Jeshi la Polisi Lavamia Mkutano wa ACT Wazalendo kwa Lengo la Kumkamata Zitto Kabwe Taarifa tulizopokea kutoka Kahama niù kuwa Jeshi la Polisi limevamia Mkutano wa Kampeni wa ACT Wazalendo katika Kata ya Isagehe kwa lengo la kumkamata Kiongozi wa Chama, ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto. Hata hivyo, bado hawajamkamata kwa kuwa alishaondoka katika eneo la mkutano mara alipomaliza kuhutubia lakini wanashilikia moja ya magari yaliyoko kwenye msafara wake.Tunaamini hatua hii ya Jeshi la Polisi inatokana na msimamo wa chama chetu juu ya tishio la baa la njaa nchini na mambo mengine ya kitaifa, pamoja na kuzidiwa kwa CCM katika kampeni zinazoendelea katika Kata ya Isagehe. Tunaendelea Kufuatilia kinachoendelea na tutaujulisha umma kila hatua. Katika hatua hii tunalaani hatua hizi za kuendelea kugandamiza Demokrasia na juhudi Ovu za Serikali ya CCM za kutaka kulazimisha Ushindi katika maeneo ambayo chama chao hakikubaliki. Tunawasihi wanachama wetu na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa watulivu tukiendelea kufuatilia jambo hili. Ado Shaibu Katibu - Kamati ya Itikadi, Mawasiliano ya Umma na Uenezi Januari 21, 2017




Kwa hali hii kwa nini ccm isishinde?

Mpo ulingoni bondia mwenzio kafungwa kamba mikono unaweza kushindwa kweli?


Kila mkutano wa upinzani lazima polis wavamie

Wanakuwa bize kwenda polis kuliko kupiga kampeni bado madc na wakurugenz hajafanya yao hatar sana

Mnakuja kujitekenya na kucheka huku
 
Katiba Mpya waliyoisusia ilikuwa na Tume huru na Haki ya kuhoji Ushindi wa Rais Madarakani.
Jakaya alikusudia Kuwasaidia Wapinzani Indirect na ikiwezekana wapate Wabunge wengi ikiwezekana iundwe Serikal ya Umoja wa Kitaifa Kama alivyowafanyia Zanzibar 2010lakin walipoteza hiyo bahati kwa kususia Katiba Mpya na kumchukua Lowassa Kama Mgombea wao!

Nafikiri tuna uelewa tofauti. Mimi najua kuwa wanasiasa wawe wa chama tawala au wa upinzani wanafanya kazi kwa maslahi yetu Watanzania. Kwa msingi huo, kauli ya kwamba "JK alikusudia kuwasaidia wapinzani" kwangu mimi haina mantiki yoyote. Hii ni nchi yetu Watanzania; si ya "wapinzani". Labda ingekuwa kwamba JK alitaka kusaidia kutuletea mfumo bora wa demokrasia nchini kwa kufanyia kazi hoja za msingi za wapinzani basi tungesikitika sana kwa nini hao jamaa walimpuuza?

Pili, mimi binafsi siamini kabisa katika kitu kinachoitwa "serikali ya umoja wa kitaifa" kama ile ya Z'bar. Huwa naona serikali za aina hiyo hazilengi kushughulikia matakwa yetu wananchi badala yake ni mpango wa wanasiasa (wa chama tawala na upinzani) kugawana madaraka bila kubugudhiana kwa maslahi binafsi. Ni kama leo hii nisikie Mh. Mbowe, Lissu, Lema, n.k. wameteuliwa na Magufuli kuwa mawaziri katika serikali hiihii na wameridhia! Nitachukulia kama mzaha mbaya kwa Watanzania.

Tatu, kama kweli unaamini kuwa wapinzani walipoteza bahati ya kutuimarishia demokrasia kwa kususia Katiba Mpya na kumchukua Lowassa Kama Mgombea wao, inabidi pia useme kama hii imetuathiri vipi wananchi? Je, leo hii mambo yetu shwari au kuna kilichoharibika? Kama hali ya demokrasia na utawala wa sheria imeharibika, tufanye nini? KAMA HAKUNA TATIZO KWA WANANCHI, kwa nini tujali kwamba hao wapinzani waliharibu fursa zilizotolewa na JK wakati tumeridhika kabisa na serikali tuliyo nayo? Can't we just ignore these "wapinzani"?
 
Back
Top Bottom