Ni kwamba, wanasheria upande wa mashtaka ni lazima wawe na "burden of proof" lakini kutokana na umahiri wa mawakili wa upande wa utetezi, hoja dhaifu za kisheria zinabomolewa ile mbaya.
Shahidi wa jana na wa leo wameboronga sana. "Cross examination' imewaweka katika mazingira magumu sana. Nafikiri "examination in chief" inaonekana kama kichekesho.
Mathalani, kwa siku ya jana hata "re examination" kwa Goodluck wala haikutajika. Achilia mbali ya majibu yenye utata ya leo ya shahidi ambaye ni "Police Inspector" ambaye hana kumbukumbu zake yeye mwenyewe pamoja na mahitaji ya lazima yalipo katika PGO.