Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa mpaka 15, Nov 2021

Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa mpaka 15, Nov 2021

Kuna jamaa hapo pichani tumesoma naye chuo na alikuwa Ana feli Sana Ni mbishi Sana na kweli alikuwa mwanasiasa kutwa kuiponda ccm..kweli asee mpk kwenye kesi ameenda Basi anaipenda cdm toka moyoni nimeamini Leo
Taja majina yake na yako tupime kama kweli mlisoma pamoja, otherwise, Acha uongo!
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Salaam Wakuu,


Leo tarehe 12/11/2021 anatarajiwa kusikilizwa shahidi mwingine katika muendelezo wa kesi Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe.

Kujua jana kesi ilipoishia, soma: Kesi ndogo ya Freeman Mbowe: Shahidi akamilisha ushahidi wake, Shahidi mwingine kuendelea tarehe 12/11/2021

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

FD-q4B6XwB0d7Ul

Picha: Watu mbalimbali waliohudhuria kesi Mahakama Kuu leo 12/11/2021
Mawakili wa Jamhuri walishafika mapema, waliomba dakika 10, wakapewa, zimefika 30. Wao wanataka kupinga uamuzi mdogo wa jana kuhusu kielelezo chao cha D.R (detention register) kukataliwa.

======
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa

Wakili wa Serikali, Robert Kidando: anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali

Jenitreza Kitali
Abdallah Chavula
Pius Hilla Esther
Martin Tulimanywa
Majige Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala: anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi

Jeremiah Mtobesya
Paul Kaunda Fredrick
Kihwelo Dickson
Matata Idd Msawanga
John Mallya
Nashon Nkungu
Alex Massaba
Khadija Aron
Evaresta Kisanga

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja tupo tayari Kuendelea Wakili

Peter Kibatala: Nasisi tupo tayari Kuendelea

Jaji: Shahidi Wenu..?

Wakili wa Serikali: Robert Kidando Yupo amefuatwa

Jaji: Majina yako

Shahidi: anaitwa Askari namba H4323 Msemwa

Jaji: Miaka

Shahidi: 31

Jaji: Dini Yako

Shahidi: Mkrito

Shahidi: Mimi Askari namba H4323 D/ C Msemwa Naapa Kwamba yote nitakayo Sema ni ya Kweli

Wakili wa Serikali: Umesema Unaitwa Nani

Shahidi: naitwa Askari namba H4323 Msemwa

Wakili wa Serikali: Kazi yako nini

Shahidi: Askari Polisi

Wakili wa Serikali: Kituo cha kazi Upo wapi

Shahidi: Nipo Oysterbay

Wakili wa Serikali: Kabla ya Hapo ulikuwa wapi

Shahidi: Kituo cha Polisi Msimbazi na Baadae Kituo cha Polisi Central

Wakili wa Serikali: Central ya wapi

Shahidi: Central Ya Dar es Salaam

Shahidi: Anaweza Kuletwa na Mtu yoyote hata Kama wananchi au Maaskari watakao Kuwa Wamemkamata

Wakili Wa Serikali: Mtuhumiwa anapoletwa Je ni Vitu gani hufanyika

Shahidi: Kumpekua Mashtaka, Kwanza ni Kuona Kama ana viambatanisho Vya Reference namba Na siyo Mtuhumiwa lazima. Awe amefunguliwa kesi, Unaweza Kumfikisha Mtuhumiwa akafunguliwa Kesi pale pale WS: Mtuhumiwa ambaye Kesi imeshafunguliwa analetwa na nani

Wakili wa Serikali: Chumba cha Mashitaka Maana yake nini

Shahidi: Chumba Cha Mapokezi, Tunaita CRO pale ambapo Mteja anapokelewa

Wakili wa Serikali: Wateja wa aina gani wanaopokelewa

Shahidi: Wanakuja Kufungua Kesi na Watuhumiwa wote hao ni Wateja Kwa Polisi

Wakili wa Serikali: Majukumu yanayohusiana na Mashitaka (CRO)

Shahidi: Kufungua Kesi, Kupokea Watuhumiwa na Kutoa Au Kupokea Huduma Mbalimbali zinazohitaji Huduma za Kipolisi

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama sasa CRO inahusika Kupokea Watuhumiwa, Je Utaratibu Wa Kupokea Watuhumiwa Ukoje

Shahidi: Pindi Mtuhumiwa amepokelewa Polisi Pale Chumba Cha

Wakili wa Serikali: Tofauti na Mtuhumiwa Kueleza Mwenyewe, Je Taratibu Zingine ni zipi

Shahidi: Ukiondoa hiyo ya Yeye Kusema, Kama Mtu ni Kibaka wakati Unampekua unaweza Kuona Majeraha

Jaji: Kibaka ni Mtu gani

Shahidi: Mtu ambaye ameletwa baada ya Kupigiwa na Wananchi

Wakili wa Serikali: Hali ya Ki Afya ya Mtuhumiwa hapo Chumba Cha Mashtaka hutokea Vipi

Shahidi: Uelezwa na Yeye Mwenyewe wakati tunaandika Taarifa zake kama Nzuri tunaandika "Good" Kumaanisha Mzima na Kama ni Magonjwa tunaandila "Sick" Kumaanisha Mgonjwa.

Wakili wa Serikali: Kama Mlikuwa wengi tutajie hao wengi ni akina nani

Shahidi: Assistant Inspector Fatuma, PC Emanuel, PC Semeni na Constable Samweli

Wakili wa Serikali: Kazi yako Siku hiyo ilikuwa nini

Shahidi: Nilipangiwa Charge Room

Wakili wa Serikali: Ambapo kazi yake ni nini

Wakili wa Serikali: Zamu ya namna gani

Shahidi: Zamu ya Masaa 12, Kwa hiyo Robo saa Kabla Natakiwa Kuwa kazini

Wakili wa Serikali: Ukiwa Kama Askari za wa zamu, Siku hiyo Majukumu yako yalikuwa yapi

Shahidi: Tulikuwa Wengi na incharge anagawa Majukumu

Wakili wa Serikali: Kwani Dhumuni la Kuangalia Afya ni nini

Shahidi: Ni sababu ya Kutaka Kujua Kama hali ya Mtuhumiwa ni nzuri

Wakili wa Serikali: Endapo Mkaona hali yake Ki Afya siyo Nzuri Mnafanyeje

Shahidi: Tunajaza KWENYE Fomu ya PF3 na Tunampeleka Hospitali, Wale wenye Malaria tunawapeleka Hospitali na Bado Wakirudi tunajaza Mgonjwa

Wakili wa Serikali: Eleza Mahakama tukufu Kwamba 07 August 2020 ulikuwa wapi

Shahidi: Mnamo tarehe 07 August 2020 Alfajiri nilikuwa naingia Kazini, Central Dar es Salaam Kama Askari Wa Zamu Chumba Cha Mashtaka. Ni kafanya Utaratibu Wa Kawaida Upekuzi Kuwa andika Kwenye Detention Register

Wakili wa serikali: Baada ya kuwa Detain Ukafanya nini

Shahidi: Kuwachukua watuhumiwa na Kuwapeleka Mahabusu

Wakili wa Serikali: Mahabusu ya wapi

Shahidi: Ya Central palepale

Shahidi: Walifika Central Ilala Eneo la CRO wakiwa na Watuhumiwa na Moja kwa Moja Baada ya Kufika Afande Jumanne akauliza pale, Nani anahusika na Watuhumiwa Nikamwambia Mimi hapo, Akasema Hawa watuhumiwa Wamekamatwa Moshi na Reference Namba zao hizi hapa

Shahidi: Kuingiza na Kuwatoa Watuhumiwa Chumba cha Mahabusu

Wakili wa Serikali: Unakumbuka Siku hiyo ilikuwaje

Shahidi: Alifika Afande Kingai, Afande Jumanne Na Askari Wengine Wakiwa wameshikilia Bunduki Wakiwa Pamoja na Watuhumiwa Wawili

Wakili wa Serikali: Afande Kingai na Afande Jumanne ni akina nani hasa

Shahidi: Afande Kingai Kwa sasa ni RPC..

Wakili wa Serikali: Kipindi Hicho alichofika

Shahidi: Afande Kingai alikuwa RCO Arusha na Afande Jumanne alikuwa anatokea Polisi Makao Makuu, Ndiyo nilikuwa nafahamu hivyo

Wakili wa Serikali: Walifikia Eneo gani

Wakili wa Serikali: ikawaje

Shahidi: Afande Kingai alirudi Kumchukua Mtuhumiwa

Wakili wa Serikali: Mtuhumiwa Yupi

Shahidi: Adam Hassan Kasekwa

Wakili wa Serikali: Umesema Kwa Mujibu Wa Reference Ulizoluwa Umeletewa Hawa watu walikuwa na kosa Gani

Shahidi: akula Njama za Kufanya Vitendo Vya Kigaidi

Wakili wa Serikali Watuhumiwa Walioletwa ni akina nani

Shahidi: Walikuwa ni Watuhumiwa Wawili wa kiume

Wakili wa SerikaliJe Kuwatambua Kwa Majina

Shahidi: Mohamed Abdilah Ling'wenya na Adam Hassan Kasekwa

Wakili wa Serikali: Kingai na wenzake baada ya Kuwapeleka Mahabusu wote walikwenda wapi

Shahidi: Baada ya Kuwapeleka Mahabusu Watuhumiwa Wote na Kuwajaza Majina yao, Umri wao, Afya zao na Kosa wanalotuhumiwa nalo Baada ya Hapo nikawapeleka Mahabusu, Wao wakina Kingai Wakaondoka

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kwamba Baada ya Kuwa wamerejeshwa Mahabusu, lini tena ulishughulika nao Shahidi: Mimi Ndiyo nilikuwa Mtunza Mahabusu, Niligawanya Muda wa kuwatembelea. Muda wa Asubuhi Wakatikuwapelekea Uji kwa Watuhumiwa Wote na Kushusha Chai za Ndugu wengine
Mbona shahidi Kama karirishwa. Ndio maana wakiuliwa maswali hawategemei maswali magumu maana wamekaririshwa. Home Boy wangu kuwa mkweli. Hawajamaa hawajaletwa hapo central ...au umeahidiwa cheo? Ila mwisho WA uongo NI ubaya. Makinika. Tambua kuwa unajijengea uadui mkubwa Sana ..Leo Una nguvu he kesho yako waijua?
 
UNAWEZAJE KUSHINDANA NA MWENYE NYUMBA UKIOLEWA LAZIMA UTOE SASA WEWE UNALETA UJANJAHAPA MUMEO ANAKUITA IMESHASIMAMA HUKO KAINAME
HIVI huwa unaona raha gani kutetea UOZO kila kukicha? Mwenzio Ndugai ameshahamaki kwa bunge lake kuitwa dhaifu.
 
ERYTHROCYTE VIPI WAZUNGU SIKU HIZI WAMESHAKATA PUMZI YA KUSHABIKIA UGAIDI WA MBOWE?
Wazungu wana akili kubwa sana. Walikuwa wanataka kusikia ushaidi muhimu wa shaidi wa kwanza kwani kiini cha kesi yote kinapatikana kwa shaidi wa kwanza

Sasa shaidi wa kwanza na ndio aliyefungua amekuja na ushaidi wa kichekesho. Wazungu wameshajua hapo hakuna kesi. Sasahivi wanasubilia matokeo ya hizo komedi zenu mahakamani ili na wao wafanye mambo yao
 
Wale tuliambiwa na makamanda ni mabalozi wako wapi?
Au baada ya kujua mbivu na mbichi wameamua kila mtu abebe mzigo wake.
Kwasababu wameshaona hapo hakuna kesi. Wanasubilia hukumu tu, kama itakuwa ya haki watatulia na kama haitakuwa ya haki wafanye mambo yao
 
HIVI huwa unaona raha gani kutetea UOZO kila kukicha? Mwenzio Ndugai ameshahamaki kwa bunge lake kuitwa dhaifu.
Wako wapi AKINA Makinda.na wengineo...umwite MWENYE nyumba, anaanyaanya Tu Bungeni .kujimwambafai..Mnakinishe asijisahau KILA MTU. Atapita watakuja na wataviacha wengine WAJE. Yuko wapi aliyetuanzishia upoteaji watu? Yuko wapi Mzee WA ruksa..Yuko wapi Swahiba yangu Mhenga mwenzangu WA Msoga. Naye Ndungai atapita.. awe MAKINI asije olewa akitoka kwenye kiti hicho.
 
Suley2019
Uandishi wako unachanganya sana hauna mtiririko mzuri km waandish wengine wanao ripot kwa maandishi moja kwa moja kutoka mahakmn.
Doo punguza haraka.
 
Uwasilishaji wa leo siyo mzuri. Majibizano yamechanganywa sana, tofauti na siku nyingine.
 
Muda wa Kazi ofisini huwa Ni saa mbili Sasa kwanini mahakamani kila siku wanaingia Saa tano?
 
Back
Top Bottom