Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa mpaka 15, Nov 2021

Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa mpaka 15, Nov 2021

jbhmmm.png
 
Kibatala: MHESHIMIWA JAJI tunaomba Tujirizishe kama Shahidi hana Diary na Kama Kwenye Diary anaandika Chochote.. Na Pia kama Shahidi ana simu pale kizimbani.... Na Kama ameingia na Vitu Visivyoruhusiwa kizimbani tunaomba aondolewe kuwa Shahidi..

Kibatala: Zitoke pande mbili za Mawakili Chini ya Mahakama tukamkague Kwanza Kabla Kesi haijaendelea...

Shahidi: ANAONYESHA DIARY, PENI, KARATASI NA SIMU JUUUUUU kabla hajakaguliwa...

Kibatala: Tunaomba vitu hivyo viwe chini ya uangalizi wa mahakama kabla hatujaendelea na kesi

Afisa wa Mahakama anaenda Kizimbani Kuchukua DIARY, PENI na SIMU kutoka kwa shahidi wa Jamhuri.. Shahidi anatikisa kichwa kama ishara ya kusikitika...
Katiba mpya ni lazima na ni sasa.
 
ni sheria gani inayosema shahidi hatakiwi kuwa na material yeyote? wakati sheria inaruhusu kama kuna kitu unataka kufanya reference unaiomba mahakama na unasoma kabisa sehemu za kumbukumbu zako? acha kupoteza wenzako bush lawyer wewe.
Vipi vifungu vya Sheria vinasemaje?
 
Madaktari wanaingia na nondo sembuse njagu.
Njagu si aliapa anapopewa unjagu na Leo mahakamani kaapa,he PGO haijui akiwa mahakamani.
Swali,nani amempa maono Kibatala atabiri kuwa jamaa ana nondo?
Siku 3 mfululizo mlikuwa na J4 ambaye amekiri kusimamishwa kazi kwa utovu wakumbambikia meno halafu upande wa serikali bado unamtumia mahakamani.
Muuguzi analalamikiwa na wagonjwa,Dr unamtumia tena akathibitishe dawa kwa wagonjwa.
 
Huku mwenendo wa kesi ukiwa unaendelea kwenye kesi ya uhujumu uchumi insyomkabili Freemani Mbowe na wenzake Shahidi wa upande wa mashitaka afande Msemwa amekutwa na Simu, dairy akiwa kizimbani.

Wakili wa utetezi Kibatala ameinia hoja hiyo mbele jaji leo

View attachment 2007987

View attachment 2007988

View attachment 2007989
mawakili wa utetezi wanakosa cha kuzungumza wanakosa hoja za msingi mpaka wanaona vitu kama diary na peni vinamsaidiamshahidi kutoa maelezo? inamaana simu anaweza kuitumia hapokupata majibu kweli? hapo hakuna mawakili wa utetezi ni njaa tu zinawasumbua
 
Kisheria shahidi hatakiwi kuwa na materials yoyote pindi anapokuwa kizimbani kutoa ushahidi. Ila huyu wa leo Detective Constable Msemwa amekutwa na diary, pen na simu. Hii imeleta idea kwamba majibu yote aliyokuwa anaongozwa kuyatoa, ni kama alikuwa anayasoma.

Vitu vyote hivyo vimewekwa pendings, then baadae vitakaguliwa kuona endapo kuna details zinahusiana na hii kesi, then maamuzi yatafanyika.

My take:

Shahidi alipo ni mbele ya benchi la mawakili wa upande wa Jamhuri, how come wameshindwa kuliona ili kosa? Hata kama hapatakutwa na chochote kwenye hiyo diary cha kuathiri kesi, ila najiuliza hawa mawakili wa upande wa serikali, umakini wao upoje??
Hii kesi jamuhuri inatamani itemane nayo ila inashindwa itaitema vipi[emoji1][emoji1]
 
Hivi uko timamu kiakili au unaandika tuu ilimradi uandike?
Ukiingia kwenye mijadala ya watu timamu andika kwa kufikiri kwanza, maana waweza kuwa na hoja basi iweke vizuri sio kama mtu aliyekamatia mpini.
nyie akili mmeziweka rehani hatutaki ugaidi MBOWE NI GAIDI
 
ni sheria gani inayosema shahidi hatakiwi kuwa na material yeyote? wakati sheria inaruhusu kama kuna kitu unataka kufanya reference unaiomba mahakama na unasoma kabisa sehemu za kumbukumbu zako? acha kupoteza wenzako bush lawyer wewe.
Ingekuwa sio kosa, basi visingezuiliwa na mahakama.

Muda huu bado wanajadiliana issue nyingine, after that ndio hivyo vifaa vitakaguliwa. Nasubiria kwa hamu huo ukaguzi.

Right now, acha niconcentrate kusikiliza. Ni raha kuhudhuria hapa mahakamani.
 
Kibatala: Na sisi Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Nne tunapinga Kwa Nguvu 1. Shahidi siyo Competence, na Competence Inagawanyika MAKUNDI Mawili (a) In ISOLATION Kwamba haja' lay Foundations Kwamba inamuhusu, Kama Mimi Ningekuwa Ndiyo Wakili wa Serikali, Kwa kuwa Shahidi alidai Kwamba. Alisainishwa Mahala fulani, ilikuonyesha NEXUS kati ya Ofisi ya Msajili na Shahidi, Kwamba Barua Isingemfikia Kwa kuelea Hewani, Wameweka toroli Mbele ya Farasi na Hiyo Ndiyo inaondoa Competence ya Shahidi ambayo pia ni R Prequisite ya Tendering.

Mambo mazito upande wa wanaowaongoza mashahidi wa jamhuri kupitia kwa wakili wa serikali (WS)
 
ni sheria gani inayosema shahidi hatakiwi kuwa na material yeyote? wakati sheria inaruhusu kama kuna kitu unataka kufanya reference unaiomba mahakama na unasoma kabisa sehemu za kumbukumbu zako? acha kupoteza wenzako bush lawyer wewe.
Wewe naona hujafikia hata kiwango cha kuitwa bush lawyer.

Document ambayo shahidi anaruhusiwa kuiwakilisha kama ushahidi wake huwa imewasilishwa mbele ya mahakama wakati wa uwasilishaji hoja. Ndiyo maana vielelezo huwa vinatolewa na mahakama kumpa aliyewasilisha. Siyo unakurupuka tu mikaratasi yako unaenda kusimama kizimbani.
 
KIBATALA: Hatari ambayo Tusingependa Kufika huko, Ni Naibu Msajili N.N Ntandu Kuja kuwa Shahidi Kwenye kesi hii, Mahakama itahusishwa Kuja Kuziba Gap Fulani aje Kuulizwa Ulimkabidhi Shahidi Kwa Madhumuni Gani wakati Shahidi Siyo Muhusika.

Kibatala: Sijasikia Shahidi akisema Kwamba Barua hii ni Nakala Kwake na Kwa Mamlaka yapi.. Lakini Pia Barua Kama ambayo Ina Purport Kupokea Exhibit Kwenye Mahakama, Ilitakiwa iwe preceded na Law, It's Jurisdiction Issue..

Dah mambo hadharani! Kuna mikono mingi nyuma ya pazia inahusika kuingilia mwenendo wa kesi hii ya kihistoria.
 
Ingekuwa sio kosa, basi visingezuiliwa na mahakama.

Muda huu bado wanajadiliana issue nyingine, after that ndio hivyo vifaa vitakaguliwa. Nasubiria kwa hamu huo ukaguzi.

Right now, acha niconcentrate kusikiliza. Ni raha kuhudhuria hapa mahakamani.
kesi hii wengi mnaojadili hamjui kabisa procedure za mahakamani, na huwa ni ngumu sana kuwaelewesha. subiriini kesi ifike mwisho mtapata jibu. yaani kitu very trivial utakuta mnashikilia bango as if ndio kinachoamua kesi yote. hayo ni mambo ya kawaida mahakamani, pale ni vita vita mura, ila mwisho anayeshinda ndio ananyanyua bango.
 
Back
Top Bottom