Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa mpaka 15, Nov 2021

Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe na wenzake, kesi imeahirishwa mpaka 15, Nov 2021

Hii kesi sasa imefika patamu... Askari Shahidi kaingiaje na kibuti?? Kwa hiyo alikuwa anapewa nondo kwenye simu anaweka kwenye diary au alikuwa anatoa kwenye diary anaweka kwenye simu??

NB: Polisi wa Tanzania wana uwezo mdogo Sana. Nakubaliana na Waziri Simbachawene. Wanapaswa kubeba silaha na kuwepo kwenye lindo!
Khaaah!
 
Mrukeruke tu kama maharage lakini Mbowe ni Gaidi

4.-(1) Hapana mtu yeyote katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nahapana raia wa Tanzania aishiye nje ya Jamhuri ya
Muungano akayeruhusiwa kufanyakitendo cha kigaidi na mtu
yeyote atakaye fanya hivyo atakuwa ametenda kosa la jinai.

(2) Mtu atatenda kosa la kigaidi ikiwa kwa nia ya ugaidi atatenda
au hatatenda kitendo ambacho-

(a) kinaweza kufanya uharibifu mkubwa kwa nchi au shirika
la kimataifa; au

(b) kimekusudiwa au kinaweza kusemekana kuwa kimekusudiwa-
(i) kutishia uma kwa kiwango kikubwa;

(ii) kuilazimisha Serikali kufanya au kutokufanya kitendo
chochote;


(iii) kudhoofisha au kuharibu kwa kiwango kikubwa misingi ya kisiasa,
kikatiba, kiuchumi au miundo ya kijamii ya nchi au shirika la
kimataifa; au


(iv) kuishawishi Serikali hiyo au shirika hilo la kimataifa; au

(c) kinahusisha au kusababisha, kulingana na mazingira-

(i) shambulio kwa maisha ya mtu ambalolinaweza kusababisha kifo;
(ii) shambuliokwa uadilifu wa mtu;
(iii) utekaji wa mtu.



Sasa hapo hivyo ulivyovionesha vinahusika vimeshathibitishwa mpaka sasa? Na je una uhakika vitathibitishwa? Hamna kitu hapo!
 
Kuna ushirikiano mkubwa wa kihalifu kati ya serikali, mahakama na vyombo vya dola. Haya ni matokeo ya kuwa na serikali iliyoingia madarakani kwa wizi wa kura, kwa vyovyote lazima itatenda kazi zake kwa njia za kihalifu.
Hivi kwanini vile vitu yaani simu na ile diary havijakaguliwa leo leo kabla hajarudishiwa?? Nimesikia Jaji akisema atabakiza diary huku simu akisema arudishiwe shahidi. Wanaweza kuja weekend hii nakufanya mabadilisho. Hawa watu ni mabingwa wa kufanya editing nyaraka za Mahakama. Ni hayo Tu Mh Tindo
 
mawakili wa utetezi wanakosa cha kuzungumza wanakosa hoja za msingi mpaka wanaona vitu kama diary na peni vinamsaidiamshahidi kutoa maelezo? inamaana simu anaweza kuitumia hapokupata majibu kweli? hapo hakuna mawakili wa utetezi ni njaa tu zinawasumbua
Du! Hata aibu huna?
 
Mawakili wa serikali wametikishwa sana na hoja za upande wa utetezi kiasi cha kupoteza umakini wa kuzungumza kwa hoja kama mawakili wasomi wanavyotakiwa kujibeba wakiwa wanatekeleza majukumu yao.
Wakiingia kwenye mstari ulionyooka watanasa nakuweka mengine wazi.
 
Naona kesi ndogo ya diary imeibuka ndani ya kesi ndogo ya kesi kubwa. Kazi ipo
 
shahidi kaingia na nyenzo kizimbani tayari wa vita - bila kujali masharti ya kizimbani yakoje - ye anasema ati ni vita mula ushindi ni lazima ije nvua lije jua.. 🤣🤣🤣🤣

Wamezidiwa pakubwa, kesi iendelee tuone mengi zaidi toka upande wa jamhuri, mawakili wa serikali na polisi .
 
Naona raha mimi jinsi kesi hii ya kishetani inavyoivua CCM na Serikali yake dhalim nguo hadharani
 
Kesi ya kutunga, mashahidi wanaokotwa tu njiani eti kwa sababu ni Askari Wa upelelezi...

Yaani shahidi wa Jana Jumanne akaibiwa nondo toka stoo ya mahakama...

Huyu wa leo naye kwa sababu ya maandalizi ya haraka haraka amepewa nyaraka ambayo hata siyo ya kwake eti itumike kama kielelezo cha ushahidi wake...

Hawa mawakili wa Jamhuri kwa kushirikiana na maafisa wa mahakama hakika ni WAJINGA SANA na NIA YAO kwa watuhumiwa hawa kwa hakika wala hata siyo KUTENDA HAKI na haki hiyo ionekane INAVYOTENDEKA...

Hivi utaletaje barua iliyokuwa addressed kwa mtu mwingine na kuifanya kuwa yako ili uitumie kama ushahidi ili mwenzako ahukumiwe..??

Hivi kuna Jaji gani mjinga anaweza kukubali UJINGA HUU...?

Huyu Jaji, Mimi ninaamini kabisa kuwa, hata kama iko nguvu ya nje kumlazimisha kuwahukumu kifungo kina Mbowe na wenzake, lakini haiwezekani kuwa kwa njia za kijinga namna hii kwa uongo wa mchana kweupe kiasi hiki...

Ni Bahati mbaya sana kuwa huyu Jaji anashirikiana na watunga uongo WAPUMBAVU na WAJINGA SANA kiasi cha kumpa wakati mgumu sana Jaji kuwabeba beba kila wakati...

Hii nyaraka nayo haitapokelewa kwa hakika nawaambia for the same grounds kama ambavyo D.R ya Jumanne ilikataliwa jana kwa mujibu wa sheria..

Hongereni sana mawakili wa utetezi. Mko makini sana na mnafanya kazi kubwa sana kuzidhibiti hila za UOVU WA HAWA HAYAWANI....!!

NB:

OUT OF CONTEXT:

Hivi njia na utaratibu wa kuchangia mfuko wa mawakili na kesi za wapigania haki wa CHADEMA uko wapi...?
 
MBOWE NI GAID KATIBA SIYO KIPAUMBELE KWA SASA TUNATENGENEZA UCHUMI HIYO KATIBA ITASAIDIA NINI ZAIDI YA HUO UCHU WENU WA MADARAKA TU
Uchumi wa kukosa winchi ya kuinua tani 26 nchi nzima kwanye bwawa la nyerere? Sijui kwanini mazezeta bado wengi nchi hii.
 
Hapana, You are deadly wrong, Katiba ya Tanzania ibara ya 13 inasema kuwa kila mtu anahesabiwa innocent hadi hapo Mahakama itakapojiridhisha kuwa ametenda Kosa na ibara ya 107 ikasema kuwa Mahakama pekee ndio yenye mamlaka ya Mwisho katika kutoa HAKI. Sasa wewe kuendelea kusema MBOWE ni Gaidi kabla ya mahakama, madhara yake kisiasa ni kwamba kesi hii ni ya Kisiasa na maamuzi yamekwishafanyika Nje ya Mahakama which is very fatal in all countries abiding to rule of law and constitutionalism.

Uko sahihi. Ninaona kauli za IGP na Rais zikiwa sehemu ya shauri hili. Je Jaji atakuwa tayari kuonesha kuwa Rais hakuwa sahihi? Je Jaji yuko tayari kuonesha maneno ya IGP “mbowe sio malaika, ushahidi tunao…” hayataathiri uamuzi wake??

Ninaona kesi hii ikikwama huko mbele hasa pale mahakama itakapoombwa kuita mashahidi wanaotakiwa na utetezi!
 
Nlikuwa najuiliza hiv kwa nn kesi huwa haziruhusiwi kulipotiwa kwenye vyombo vya habari?? Ckuwa nmeelewa ila kwa Sasa ninajua kabisa kwa Nini, ukiwasoma mawakili wote, Ni Kama vile huwa wanasoma walichokisema baada ya kutoka mahakamani, na wanasoma na maoni mbalimbali, then wanachanganya na taalum, kinachokuja kutekea wanaenda na puplic mood, na hlo Ni Jambo la hatari mno mno kisheria(wanasheria watakuwa wanajua hasa madhara yake)

Ila itoshe tu kusema kesi hii itachukua mda mrefu mno kwa sababu kila hatua itakuwa na mapingamizi na ukiangalia Ni Kama wanacheza na puplic mood, na nanaweza kuhis na jaji au majaji wanaweza kuingia humo.

Anyway hyo ndo transparence..
Justice must not only be done but seem to be done... anzia hapo huku ukijikumbusha kuwa hiyo ni open court, ingia hata google.

Pia mapingamizi hayo ni ya kisheria ndio maana wananukuu vifungu vya sheria na maamuzi ya kesi za nyuma, sijasikia upande wowote ukinukuu 'public mood'
 
YAANI huo ujinga wenu wa kufurahia ugaidi unaingia nchini na watu wenye tamaa kina mbowe haukubaliki mbowe lazima alle miaka mingi sana na akiachiwa tunakuja kumpiga hata na mawe huku mtaani MBOWE GAIDI
Shahidi kakutwa na diary na pen akinukuu majibu, kesi ya kubumba ni fedheha.
 
Kuna jamaa hapo pichani tumesoma naye chuo na alikuwa Ana feli Sana Ni mbishi Sana na kweli alikuwa mwanasiasa kutwa kuiponda ccm..kweli asee mpk kwenye kesi ameenda Basi anaipenda cdm toka moyoni nimeamini Leo
Bashite wewe kiazi ulifeli darasa la nne mara 4 la saba mara 2 chuo.Moshi walikudisco ukarudi umeapa kubaki jina ukamaliza kwa nguvu za sita kwa sababu alikuondoa marinda habari yako Tanzania nzima tunaijuwa so usijitoe ufahamu
 
Justice must not only be done but seem to be done... anzia hapo huku ukijikumbusha kuwa hiyo ni open court, ingia hata google.

Pia mapingamizi hayo ni ya kisheria ndio maana wananukuu vifungu vya sheria na maamuzi ya kesi za nyuma, sijasikia upande wowote ukinukuu 'public mood'
Mkuu sijasema popote kuwa wananukuu public mood, nilichosema ukiwasikiliza na ukochora body language yao kifasihi utagundua kuwa kuna mahari Ni Kama wanakwenda na public mood, japo hawawez wakasema, ili ujastfy heb Angalia kile kibatara alichokise wakati anatoa zuio la kukataa kielelezo, mpka akasema hyo mtu ana diary cjui sim[emoji15][emoji15] cjui kama unanielewa, Sasa Angalia chanzo Cha alikotoa hyo taarifa, unaweza kuona how public mood inavyo waendesha wanasheria wetu, na ujue hata ile kesi ya yule mkuu wa wilaya ingekuwa inarepotiwa hivi Bila shaka isingekuwa imeisha...
 
Hii kesi inavutia sana jinsi mawakili wanavyochuana, najilaumu babangu kunipeleka sayansi..nafikiri ningefiti sana hapa kwa sheria maana mimi ni king of logic.

If..then.. end if...zimelala.
 
Back
Top Bottom