Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Novemba 17, 2021: Kesi yaahirishwa mpaka tarehe 18/11/2021 saa tatu asubuhi

Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Novemba 17, 2021: Kesi yaahirishwa mpaka tarehe 18/11/2021 saa tatu asubuhi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Salaam Wakuu,


Leo tarehe 17/11/2021 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea baada ya kuahirishwa siku ya jana.

Kujua jana kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe: Jaji aahirisha kutoa uamuzi mpaka tarehe 17/11/2021 saa tatu asubuhi

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

UPDATES
- Jaji ameingia Mahakamani

- Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa


Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha
1. Pius Hilla
2. Abdallah Chavula
3. Nassoro Katuga
4. Jenitreza Kitali
5. Tulimanywa Majige
6. Esther Martin
7. Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi
1.Jeremiah Mtobesya
2. John Mallya
3. Dickson Matata
4. Idd Msawanga
5. Seleman Matauka
6. Khadija Aron
7. Evaresta Kisanga

- Jaji anaita Majina ya washtakiwa 1,2,3 na 4 na wote wanaitika kuashiria wapo...

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Uamuzi Mdogo, Tupo tayari

Wakili Peter Kibatala: Na sisi pia tupo Tayari Kuendelea kusikiliza Uamuzi na Kuendelea na Shauri

Jaji: Ni Kweli Kwamba Mahakama hii ilihairisha Shauri kwa ajili ya Kusoma Uamuzi na Uamuzi upo tayari na haya Ndiyo Maamuzi Yenyewe.

Jaji: Kwenye Shauri Maarufu Sana la Uingereza aliyekuwa Jaji Mkuu wa Uingereza Wakati huo alitoa Kauli ambayo inaisho Mpaka Leo, Kwamba Haki siyo tu Itendwe Bali ionekane Ikitendwa.. Na Kauli hiyo imekuwa Ikitumika Mpaka Leo pamoja na Shauri hili hili kuwa tofauti.

Kwa Mtu atakayesoma Uamuzi huu Hatoweza kuelea Kwanini Nimefika Uamuzi huu.. Historia inaonyesha Askari Polisi Mwenye Namba H4323 DC Msemwa alipokuwa anatoa Ushahidi Wake Mahakamani aliomba Kutoa Kielelezo Chake, Wakati anatoa Upande wa Utetezi walipinga.

Na wakati Pande zote Mbili Wakieendelea Kutoa Hoja, Basi Wakili Peter Kibatala Alisimama na Kusema Kwamba anaomba Kui' move Mahakama Kwamba Shahidi aliyepo Kizimbani ana Diary, pen na Simu...

Na Kwamba aliomba Mahakama Itamke Kwamba Siyo Shahidi Tena na Kwamba Ushahidi Wake ufutwe wote, Mahakama ili chukua Vitu Vile na Kwasababu Muda Ulikuwa Umekwenda sana Mahakama ilishindwa Kulishughulikia Jambo lile..

Na Mpaka Ilipofika 15 Mahakama Ilianza Kujiridhisha Kwamba Kama ingeweza Kujiridhisha kwa Kushughulika Simu. Hata hivyo Mahakama Ikaona hakuwa akitumia Simu Yake Basi Mahakama Ikaona arudishiwe Simu yake, Na Mahakama ikabakia na Diary na Pen

Hata hivyo Mahakama Ikawaelekeza Mawakili Kwamba wakafanye Utafiti, Itakapofika Tarehe 15 Waje na Utafiti, Ilipofika Siku ya Tarehe 15 Mahakama Ilishughulikia Suala Uamuzi Kwanza Kwamba Mahakama Ilielekeza Kielelezo Kipolewe na Kisomwe

Lakini Kabla ya Mahakama Haijasoma Kielelezo hicho basi Mtobesya Alisimama Kabla Shahidi hajasoma akaomba Mahakama Isikilize Jambo hilo kabla Shahidi hajasoma Kwa sababu akisoma Itaonekana aliendelea Kutoa Ushahidi, Upande Wa Mashtaka Wakasema hawana Pingamizi.

Jaji: Wakati Hoja inaletwa walisema waliona Jambo hilo wakati Mahakama Inaendelea, Wakasema Kwamba Shauri Linaundwa Juu Sheria ya Uhujumu Uchumi lakini Wakaona Sheria hiyo haisemi Moja kwa Moja.. Kifungu cha 28 cha Sheria hiyo kinaipa Mamlaka Mahakama Kutumia Sheria Nyingine.

Basi wakatumia Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai Kifungu cha 264, Basi Kwa Kutumia Kifungu hicho cha 28 na 264 ndiyo lilijenga Misingi Kwa wao Kuleta Jambo hilo. Wakasema Kwamba Shahidi anapokuwa Kizimbani hatakiwi Kuwa na Nyaraka Yoyote na Kwamba wakaomba Mahakama Itamke.

Kwamba Shahidi Hafai na Ushahidi Wake Ufutwe. Wakasema Kwamba Kuna Sheria Mbalimbali zinazoelekeza Jambo hilo Ka 168 ya Uhujumu Uchumi na PGO ya 282. Walitoa Hoja Mbalimbali kwa sababu ya Muda sito zitaja zote. Nitaje Kesi walizotumia wakati wa shauri hili Ka NANYARO Vs PENIEL

EDWARD ISACK SHAYO VS JAMHURI, OKUMU Vs UGANDA, GOODLUCK KYANDO Vs JAMHURI, Zote zimetumika katika kutoa Uamuzi huu. Msingi wa Hoja yao Kwamba Shahidi atakiwi Kuwa na Kitu chochote Wakati Mahakama Ikiendelea bila a Kibali Cha Mahakama.

Jaji: Ukweli ni kwamba Walimuona Shahidi Wakati Hoja zingine za Mawakili wa Serikali wakizitoa. Hakuna Ushahidi Kwamba alikuwa akirejea Jambo lolote. Kwa sababu hiyo waliiomba Mahakama i'presume Mambo yafuatayo kwamba wakati anaingia Kwenye Kizimba hicho aliingia nayo.

Kwamba Material ambayo aliingia nayo Wakati Mahakama aikiendele ionekane alitumia, Kwa sababu Aliingia na Nyaraka Bila Kibali cha Mahakama basi Shahidi aonekane ni Incompetent, Ushahidi ambao ameshautoa haufai, Na aondolewe Kutoa Ushahidi Mahakamani.

Na Kama itaonekana Suala la Kumuondoa Shahidi Ni Gumu basi Wakaomba Mahakama iruhusu Notebook Kukaguliwa na wao wapewe ili waweze Kutumia Notebook hiyo katika Maswali yao.. Kanuni inakataza Shahidi Kuingia na Nyaraka Kizimbani, Quran tukufu na Biblia Tukufu ndiyo Vitu Pekee.

Vinavyo Ruhusiwa Kuingia nayo Mahakamani, Kwamba Kwa Shahidi Kuingia na Mambo Mengine yanafanya Shahidi asiaminike. Mahakama ikaombwa Imkoseshe Sifa Shahidi Kwa Kutumia Kifungu cha 127 Sheria Ya Ushahidi. Kuhusu hilo Upande wa Mashtaka Walipinga Kwamba Vifungu hivyo siyo wezeshi

Jaji: Ukisoma Kifungu hiki Kinaweka Vigezo ambavyo ni wazi Vinavyoweza Kufanya Shahidi asitoe Ushahidi Wake Mahakamani.. Kwa Sababu hiyo naona Kwa Kifungu hichi Upande Wa Utetezi wametaja Kifungu Sahihi bil kujali Kama Wapo Sahihi ndani yake kuhusu Shahidi huyu.

Kuhusu Sheria Kesi ya EDWARD ISACK SHAYO VS JAMHURI haina Uhusiano katika kesi hii. Kwa kuwa Mahakama Ime' solve issue ya Jurisdiction imelimaliza.. Imebakia Issue kama Shahidi Vitu alivyokuwa navyo vinaruhusiwana Mahakamani.

Jaji: Mtakumbuka Mshtakiwa anaruhusiwa Kuingia na Vielelezo Kwenye Kizimba, Kwa hiyo Shahidi ambaye anatoa Ushahidi Anaweza Kuingia na Kielelezo Mpaka Muda atakapo Omba kutumia, Hili linaungwa Mkono na Sheria ya Ushahidi katika Kifungu 168(1)(2) ya Sheria ya Ushahidi.

Kwamba Shahidi anapokuwa anaendelea Kutoa Ushahidi Mahakamani hataruhisiwa Kufanya Ukumbusho, Wakati anaandika hiyo Nyaraka alikuwa na Kumbukumbu wakati huo, Na aliposoma andiko hilo lilikuwa Sahihi. Basi ukisoma PGO 282(7) A & A na Sheria ya Ushahidi Kifungu cha 168, 1 na 2.

Shahidi hakatazwi Kuingia na Kitu chochote Kwenye Kizimba, Na Kwamba Kabla hajafanya Marejeo ataomba Ruhusa Ya Mahakama, Jambo linalofuatia katika Shauri hili, Ni Wazi Hakuna Kilicho onekana kama Shahidi akiwa anafanya Rejea.

Jaji: Nakubalina na Kibatala na Mtobesya Kwamba hayo Yalifanyika wakati Shahidi ana Kiapo chake, Sheria inasema Kwamba Wakati amefungua alikuwa anafanya nini, Mahakama Inaona ni Kweli kwa yeye Kufungua na Kuandika ilikuwa ni VIOLATION.

Jambo linalofuatia ni Je baada ya Violation Mahakama Ione nini Kitaifuata.. Upande wa Utetezi wakasema baada ya Violation Wa naomba atamkwe Hafai na Ushahidi Wake ufutwe.

Kuhusu Kumtoa Shahidi asiendelee Kuwa Shahidi Sheria Inasema Ni Shahidi ambaye hana Uwezo Wa Kujibu Maswali na Kwamba iwe imesababishwa na Umri Mkubwa au Mdogo.. Upande wa Utetezi weomba itumike hiyo ya Mwisho ya Any other Similar Cause.

Jaji: Mahakama imeombwa Kurejea Kwenye andiko. Ambalo Mr Kibatala alilirejea Hapa Mahakamani Akiwa ameichukua Kutoka North Carolina, Kwamba Moja ya a Jambo kwao ni Pale Shahidi ana Kosa Sifa ni Kwa Shahidi Kukosa Kuona Umuhumimu wa a kutoa Ushahidi wale.

Kwa sababu hiyo Sheria hiyo kwetu Tanzania hakuna, Mtobesya ameomba Mahakama ifanye kazi ya Bunge. Mahakama haiwezi Kuongezea Jambo hilo pamoja na Kuomba Mahakama inaweza Kuongezea Sheria hiyo.

Pale ambapo Inaona kwamba Kuna Ulazima wa Kufanya Jambo hilo, Hasa Ikiwa imethibishwa Kwamba Kweli limetokea.. Suala la Kwamba Shahidi hajaona Umuhimu Wa Kuzungumza Ukweli Kwa kuwa hakuna Sehemu imeelezwa Kwamba Shahidi hajui Umuhimu Wa Kuzungumza Ukweli.

Jaji: Kinachoonekana Ni kwamba Shahidi Kwa Kuonekana na Jambo hilo Mahakamani ni suala La Kutoaminika Ushahidi Wake.. Mahakama hii sasa Inashindwa Kumuodoa Shahidi Huyu.. Nafahamu katika PGO ya 292 (5&6) eeleza Sifa ya Notebook na Kwamba Details za namna gani.

Kwamba inatakiwa Kuwa na Taarifa za Utendaji kazi, Hapo Ndipo nakubalina na Suala la Utetezi kwamba Upo Umuhimu wa kukagua Notebook hiyo, Lakini Mr Chavula alisema Kw a siyo wote ambao wameruhusiwa kukagua Notebook hiyo.. Kwa PGO 282 (7)C kwamba Ndiyo Kuna watu waliotajwa Kuhusu.

Kukagua Notebook hiyo, Lakini kwa Jambo hilo Mahakama ina maamuzi Kwamba Nyaraka Yoyote inayojitokeza Kwenye Mwenendo Wa kesi Mahakamani basi Itakuwa ni Nyaraka ama Kielelezo Cha Mahakama. Na Kwa Sababu Notebook hiyo ilikutwa Kwenye Kizimba cha Mahakama hii basi Upande Wa Utetezi.

Jaji: Lakini Mahakama Ina maoni Kwamba Kuhusu Taarifa za Siri zilizokuwa katika Notebook hiyo zinaweza kuangukia katika Mikono ya watu Wasio husika, Kwa Namna hiyo basi Kwa sababu Jambo hilo linahusu Haki za Watu Mahakama inaweka Utaratibu Wa Wakili Mmoja Mmoja ataruhisiwa.

Kukagua na Kwa sehemu husika tu.. Na Wakili hatoruhusiwa Kupiga Picha Sehemu ya Notebook hiyo. Hiyo ndiyo Maana ya Kauli yangu kwamba HAKI ISITENDWE TUH BALI IONEKANE IKITENDWA.. Na huo ndiyo uamuzi wangu..

- Mawakili wa pande zote mbili Wanasimama Kukubaliana na Uamuzi wa Jaji

Jaji: Sasa Kuhusu Utaratibu wa Nani ataruhisiwa Kukagua, Mtachaguana Mmoja Mmoja.. Na Kwamba Notebook hii ilikuwa Chini ya Mikono ya Mahakama, basi nawakabidhi hapa. Je, Mniambie Maoni yenu Mkafanyie zoezi hili katika Usiri (Privacy) au hata hapahapa.. Nahitaji Maoni yenu..

- Mawakili wa pande zote mbili Wanashauriana

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Kama Ukiridhia naomba Uhairishe Shauri kwa Muda kwa Sababu hatuwezi Kujua Ukaguzi Utachukua Muda gani.

Jaji: Utetezi ni sawa?

Wakili Peter Kibatala: Sawa haina Shida, Kwa Dakika 20 inatosha

Jaji: Kwa sababu nimesema Taarifa yoyote isichukuliwe Kwa picha au Vinginevyo basi namuweka na Afisa wangu Mmoja kwa ajili ya Kusimamia hilo Zoezi

Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na hilo.. Jaji anaandika Kidogo..

Jaji: Dakika 20 pamoja na Maandalizi ya Kurudi tufanye Saa 5 kamili Basi nahairisha kwa nusu saa, Tukutane Saa 5 Kamili.

- Jaji anatoka!

- Jaji ameingia Mahakamani..

- Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena


Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji quorum ipo Vilevile tupo tayari Kuendelea.

Kibatala: Mh Jaji, Wote tupo vilevile na Tunaomba Kumuongezea Nashon Nkungu alikuwa Mahakama ya Rufaa..

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Muda Mfupi uliopita tumetoka kwenye zoezi la Kukagua Diary

Wakili wa Serikali: OBJECTION Mheshimiwa hilo haliruhusiwi hata kidogo na hatuko tayari kuona anaendelea

Jaji: nini hasa ulitaka?

Mtobesya: Nilikuwa nataka Kui' move Mahakama chini ya Kifungu cha 176 (1) Chini ya Sheria ya Ushahidi Mahakama Ukiona inafaa Imtake Atoe Nakala ya Nyaraka Yake...

Jaji: Sasa Mimi sijajua nyie Mmeona nini? Labda tuingie Ofisini Tukaone Mmeona nini unasemaje Mr Robert Kidando?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Sawa Mheshimiwa Jaji

Jaji: nahairisha Kwa Muda,

- Jaji anatoka

- Jaji amerudi Mahakamani

- Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Quorum ipo Vilevile na tupo tayari Wakili

Peter Kibatala: Quorum ipo Vilevile haijabadirika, Na tupo Kuendelea

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Wakati umetupatia nafasi ya Kwenda Kukagua Diary Tumekuta Kuna Mambo yapo Relevant na Kesi yetu.. Kwa sababu hiyo kupitia Kifungu 176(1) ya Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 Ilivyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2019 tunaomba Mahakama Tupatiwe Kama Kielelezo..

Jaji: Upande wa Mashtaka

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi

Jaji: basi hiyo Relevant part Mahakama inaelekeza ichukuliwe na iingie Kama Sehemu ya Kielelezo. Mawakili wote wa Pande zote mbili wanakubaliana.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kuna shahidi alikuwa anaendelea na Ushahidi Wake, Tupo tayari Kuendelea

Kibatala: Tupo tayari Kwa Ruhusa yako

Jaji: Shahidi Karibu Shahidi

- kashapanda Kizimbani tayari.

Jaji: Shahidi nakukumbusha Kuwa Ulishakula Kiapo na Kwamba Chini ya Kiapo hicho Utaendelea Kutoa Ushahidi wako. Kwa Mujibu wa Taratibu zetu Shahidi anatakiwa asome Kielelezo, au Kuna Jambo Lingine

Wakili wa Serikali: Hapana Mheshimiwa

Jaji: Soma Kwa Sauti

- Shahidi anasoma Kielelezo..

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Shahidi Barua Uliyosoma ni ya Tarehe ngapi?

Shahidi: 12 November 2021

Wakili wa Serikali: Imeandikwa Kutoka wapi Kwenda wapi?

Shahidi: Kutoka Kwa Deputy Register wa Po Box 35067 Dsm, Kwenda NPS Dodoma, Po Box 1733 DODOMA

Wakili wa Serikali: Kwa Barua hiyo walikuwa wa namaanisha nini?

Shahidi: Kwa Barua hii namkabidhi Detention Register DC Msemwa Kama Ilivyoombwa

Wakili wa Serikali: Detention Register ipi Shahidi: Exhibit TP 1

Wakili wa Serikali: Ukiondoa DC Msemwa wengine ni akina nani.

Shahidi: Ni Jaji Inchaji wa Mahakama hii

Wakili wa Serikali: Barua ulipokea Lini?

Shahidi: Tarehe 12 November 2021

Wakili wa Serikali: Tofauti na Barua hii,sajili alikukabidhi Kitu gani Kingine

Shahidi: Detention Register

Wakili wa Serikali: Detention Register ya namna gani?

Shahidi: Nilitoa Mwanzo Kielelezo na ni ya Kituo cha Central Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Ulitoa Ka Kielelezo, Kielelezo Wapi

Shahidi: Kwenye Mahakama hii hii

Wakili wa Serikali: Unakumbuka ni Shauri Gani

Shahidi: Shauri hili hili la 16 /2021

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Kwamba ni Vigezo gani Vinatambulisha hiyo Detention Register

Shahidi: Kwamba Kuna Initial ambayo ni CD kwamba ni Central Dar es Salaam ambayo uwezi Kuipata Sehemu yoyote pale

Wakili wa Serikali: Inaelezea nini?

Shahidi: Mtuhumiwa aletwe pale Central Dar es Salaam lazima awe na REF namba ya Kesi iliyofunguliwa na Kwa pale Central ni CD kwa Maana Central Dar es Salaam. Na Kama Kesi haijaanza Kupelelezwa (RB) KWA HIYO inaanza CD/RB namba ya Kesi / Tunamalizia na Mwaka na Kama Kesi haijaanza Kupelelezwa(RB) KWA HIYO inaanza CD/RB namba ya Kesi / Tunamalizia na Mwaka. Unaweza Kupewa Reference kwa Kesi iliyo Anza Kupelelezwa Itaanza CD/ Badala ya RB Itaingia IR/Namba ya Kesi na Utamaliza na Mwaka.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kwamba Tarehe 12, Detention Register Iliyokabidhiwa Kwa Msajili Utatambuaje

Shahidi: Pale Juu Kuna PF namba 20, Ili Detention niweze Kuitambua lazima iwe na PF namba 20.. Na Pale Juu lazima Pawe na Ministry of Home affair.

Wakili wa Serikali: Vitu gani Vingine Vinaweza Kuku fanya Utambue ndiyo DR uliyoleta Mahakamani

Shahidi: Ndani lazima itakuwa na Mwandiko Wangu, Niliandika Kibatala wakati tofauti tofauti wakati Nilipangiwa zamu

Wakili wa Serikali: Kitu Kingine

Shahidi: Lazima itakuwa Mwezi wa Nane

Wakili wa Serikali: Jambo lingine Shahidi Tarehe 07 August 2020 lazima itakuwa na Mwandiko Wangu sababu Ilipolewa Watuhumiwa

Wakili wa Serikali: Wangapi?

Shahidi: Wawili Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali: ambao ni akina nani.

Shahidi: Mohamed Abdilah Ling'wenya na Adam Hassan Kasekwa

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukabidhiwa Detention Register Ikawaje?

Shahidi: Nafanya Kazi Oysterbay Polisi na Kwa sababu ni Mpelelezi Nina Sehemu ya kutunza Nyaraka zangu niliiitunza.

Wakili wa Serikali: Unayo kwa ajili gani

Shahidi: Kutoa Ushahidi Mahakama Kuu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi ameonyesha Uwezo, kwa Ridhaa ya Mahakama tunaomba akabidhiwe

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Nyaraka hiyo ni Kitu gani?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji Nyaraka hii ni Detention Register, a Kitabu Kinachotunza Kumbukumbu Kwa Mahabusu waliofikishwa Central Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Inahusiano gani na wewe

Shahidi: Ina Uhusiano na Mimi kwa Sababu ndiyo Nyaraka Niliyoitumia tarehe 07.8.2020.

Wakili wa Serikali: Ina vitu gani inayo Utambulisho ni ya Central Dar es Salaam

Shahidi: Kama nilivyosema Mwanzoni Kwamba Detention Itakuwa ya 12/2020, Nikasema itakuwa na PF namba 20, Nikasema lazima iwe na Maneno ya Ministry of Home affair. Ndani Kuna Mwandiko wangu Kwamba Tarehe 07.8.2020 Nilipokea watuhumiwa..

Wakili wa Serikali: Unaiomba nini Mahakama Kwa Nyaraka hiyo

Shahidi: Naomba Ipokee Ka Kielelezo Kwamba 07 August 2020 nilikuwepo Central na Nilipokea Mahabusu Wawili.

- Mawakili wa Utetezi Wanaikagua ile Nyaraka, Wanaigeuza nyuma na mbele, Wanafungua Kurasa zake kwa Haraka kidogo, Wanasikitika Kwa Kutingisha vichwa vyao..

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji, sisi kama Jopo la Utetezi tunapingamizi Kwenye Kielelezo hiki. Kwa sasa tunaomba tukutane na wewe pamoja na wenzetu, lakini tunategemea kuweka mapingamizi matatu katika suala la kupokea Detention Register ikishindikana basi tutafanya mawasilisho..

Wakili wa Serikali: Ni sawa mheshimiwa

- Jaji anaandika kidogo

Jaji: basi tukutane kwenye Ofisi yangu, karani naomba hivyo Detention Register..

- Jaji anatoka!

- Jaji ameingia

- Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena


Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kesi Imekuja kwa ajili ya Kuendelea na Tupo tayari

Wakili Peter Kibatala: Na Sisi tupo tayari Mheshimiwa Jaji

Mtobesya: Naomba kuongelea Mapingamizi Mawili then Kaka yangu Kibatala ataongeza katika pingamizi la tatu Pingamizi letu la tatu lipo kwenye Kifungu cha 353(3) cha Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai Sura ya 20 Kama ilivyofanyiwa mabadiliko Mwaka 2019.

Mtobesya: Kimsingi tunasema kwamba nyaraka Hii kwa sababu imeshatumika katika Shauri Dogo kuhusu kesi ndogo ya mshtakiwa Namba mbili, Ili Kutumika Mahakamani, Basi mahakama Ilitakiwa itoe kitu kinaitwa DISPOSAL ORDER Amri Ya Kukitoa Kielelezo hicho..

Mtobesya: Na Pingamizi letu la Pili ni Kwamba Kielelezo hiki kilishatolewa Maamuzi katika Mahakama hii, Hivyo Mahakama hii inazuia Kuiongelea tena, Na Pingamizi la Tatu kwakuwa Hoja ya The issue of Admisibility (THE ISSUE Estoppel) inazuia Mahakama hii Kutumia Kielelezo hicho. Kwa hiyo naongelea kwanza hizi tatu, Naanza Pingamizi la Kwanza.

Mtobesya: Kuwa na DISPOSAL ORDER, Kifungu cha 353 ndiyo kinaongelea Masuala ya DISPOSAL ORDER na ukisoma HEADING kabla ya kifungu hicho haijaanza Kinaonyesha (sehemu C) kinaongelea (DISPOSAL EXHIBIT) Ndiyo Title ya Juu.. Ukisoma Kifungu cha Kwanza na Cha Pili Kinaongelea kwa Ujumla ila Hoja yetu inaongelea Kifungu cha 3..


- Mtobesya Anasoma Kifungu cha 1 & 2 Naomba Sasa Umakini wa Mahakama Uelekee Kifungu Kidogo cha 3.. Na Vifungu Vingine Vyote vinavyoendelea

Mtobesya: NI Mawasilisho Yetu Kwamba Kielelezo chochote ambacho Kilishawahi Kuingia Mahakamani, Tunaomba Kurejea Kifungu Kidogo Cha 3 ndiyo tunaona Kinahusika hapa.. Kwa hiyo tunasema Kwamba Ni AMRI pekee ya Mahakama hii Ilitakiwa Kutolewa Kwa ajili ya Kielelezo. Kilichotakiwa Kuingia wakati wa Kesi Ndogo Ya Mshitakiwa Wa Pili Wakati Ule, Kuinyima. Na hayo basi Kielelezo Kitakuwa Hakija Mfikia Shahidi Kwa Utaratibu sahihi.. Kwa Maana hiyo haiwezi Sasa Kuingia Kwenye Proceedings Kama ambavyo anaomba Shahidi huyu.

Mtobesya: Kwa sababu Palipaswa Pawe na AMRI ya Mahakama Kabla ya Msajili hajatoa Kielelezo Hicho.. Kwa Maana hiyo ni Ombi Letu Kuwa Kisipokelewe Kwa Utaratibu huo Wa Kukiuka Utaratibu Wa Kisheria.

Mtobesya: Hoja yetu ya pili Tunawasilisha Kuwa ni Inakataza Kujadili Kielelezo hicho Katika Kesi Ndogo Ya Kesi Kubwa.. PW1 Aalishaomba Kuingiza Kielelezo hicho lakini ilishindikana na Mahakama ilikataa Isiwe sehemu ya Ushahidi Wake.

Mtobesya: Hata kwenye Ruling za Mahakama Wakati Inapokea hili suala tulikubaliana Kimsingi Kwamba Taratibu za Upokeaji ni Uleule iwe ID au Exhibit.. Tunaomba tu tusisitize Kwamba Suala hili ni Jurisdictional Issue tunaomba ichukuliwe Kwa Uzito huo.

Mtobesya: Kwa sababu inaathiri Uzito wa Mahakama Kwa Kutoa Maamuzi kwenye Jambo hilo, Tuna kazi kwa Kurejea Kesi Tatu, BIBI KISOKO MEDARD Vs MINISTER FOR LAND, HOUSING AND URBAN DEVELOPMENT PLANNING ANTA ANOTHER..

- Mtobesya ANASOMA

Na pia ipo kwenye Ukurasa Wa 251 aya ya Pili Kutoka mwisho, Inaelezea hicho Kitu.. Kesi ya pili ni Kesi ya THERESIA ZACHARIA Vs OCSAR RWECHENGULA.. Mahakama Kuu ya Tanzania Iliyoketi Dar es Salaam Mtobesya anasoma yote.

Mtobesya: Ya tatu ni NBC AND ANOTHER Vs BRUNO VITUS SWALO Maamuzi ya Mahakama Ya Rufaa Iliyoketi MBEYA (Civil Appeal).. Kwa Maana hiyo Jambo hili lilihitimishwa Kwamba ni FUNTUS OFICIO. Kwenye Maamuzi ilionekana Kwamba Siyo Sahihi Kwa Kuleta Jambo ambalo limeshatolewa Uamuzi. Kwamba Kwa Kielelezo ambacho Shahidi Wa Pili anaomba Mahakama kukipokea, Mahakama ikatae hicho Kielelezo.. Na Kwa Sababu hiyo Naomba Kimkaribisha Kaka Yangu Peter Kibatala.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Naomba Kuunga Mkono Hoja zilizotolewa na Kaka Yangu Mtobesya.. Ni suala la Utaratibu kwamba Kielelezo kinachokuwa Chini ya Mahakama Kufika KWA Shahidi au Kwa Mtu Mwingine Baada ya Mahakama Kutoa Malekezo kwa Kutumia DISPOSAL ORDER.

Kibatala: Na DISPOSAL ORDER zipo za namna Mbili.. 1. Ile inayotolewa baada ya shauri Kumalizika 2. na ile ambayo Kesi inaendelea.. Moja ya Sifa ya DISPOSAL ORDER ni kwamba inatakiwa Ifanyike Kwa uwazi.. Pia Itoke Kwa Namna ile ile.

Kibatala: Kwa Kesi yetu Kwa kuwa Kielelezo Kilipokelewa Kwa Jaji basi ni Kwa namna ileile Walipaswa wamuombe Jaji yule yule au Jaji aliyerithi.. Tunatambua kwamba Wenzetu Kupitia Shahidi Wa pili wamejitahidi Ku' lay Foundation Kwamba Kielelezo hicho Kimetoka Kwenye Mahakama.

Hata Kama Tukisema Barua Iliyotoka ni Authentic, Basi Naibu Msajili Hakuwa na Mamlaka hiyo With Due respect.. Tulitakiwa kabla ya Shahidi huyu Kutoa Exhibit Register walitakiwa Kutoa hapa Mahakamani Kupitia Kwa Exhibit Register.

Kibatala: Hiyo ni suala la Kisera la Mahakama kuu. Naomba Kukurejesha Kwenye Nyaraka ya EXHIBIT GUIDE LINES SEPTEMBER 2020 Iliyotolewa na Jaji Juma Katika Ukurasa Wa 19 sehemu 4:3 Heading Disposal Exhibit.. Kibatala ANASOMA SASA KWA KINGEREZA.

Kibatala: Hili ni Hitaji la Nyaraka ya Kisera, na Maelezo haya ya Jaji Mkuu hayahitaji Nyongeza. Ilikuwa ni Sharti la lazima la Sera la Nyaraka yafuatwe kabla haijafika kwa Shahidi Na kabla haijafika Kwa Shahidi. Kuhusu Pingamizi hili tunaomba tuishie Hapa Kwamba Mahakama Ikatae.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji hii Nyaraka Ipo inapatikana ila kwa Uhusiano wa Kaka na Dada Nawaazima ya kwangu.. Mheshimiwa Jaji Sasa niende Kwenye dhana ya Estoppel.. Naialika Mahakama Katika kesi ya ISSA ATHUMAN Vs JAMHURI Ukusara wa 25 na 26 Paragraph ya pili.

Ilikuwa ni Kesi ya Madai lakini Mahakama ya Rufaa ikasema inafaa Kutumika Kwa Kesi ya Jinai.. Naomba Pia Nikupeleke kwenye Kesi namba 264 Mwaka 2004 Chini ya aliyekuwa Jaji Mkuu wakati huo Jaji Othuman JULIUS MICHAEL AND FOUR OTHERS Vs REPUBLIC katika Ukusara wa SitaUkurasa wa 6,7,8 na 9.

- Kibatala Anasoma...

Kibatala: Kwamba Jambo lililokuwa limesha amriwa Katika Kesi hiyo Kurudishwa tena Mahakamani.. Imekataza. Page ya 8 ya Kesi ya Julius Michael ilisema Kwamba Issue ya Estoppel ina maana Kwamba, Siyo Sahihi Kwa Jambo lililokuwa limeamriwa a Kurudishwa Mahakamani.

Kibatala: Kwa Sababu ya Criminal Fairness, Value za Taasisi Zinazofanya Maamuzi Kulinda Hadhi yake, kutolutumia Muda na Fedha Kuamua Jambo hilohilo, Kwa kuwa Jambo lilisha amriwa basi haliwezi Kurudiwa tena.. Ni hayo tu. Kibatala anaketi..

Jaji: Serikali!!?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji ataanza Mr Chavula..

Wakili wa Serikali Chavula: Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima zote baada ya Kusikiliza Hoja za Wenzetu ambazo zimejielekeza Maeneo Matatu, Hoja ya Kwanza Ikijieleleza Kwenye Kifungu cha 353(3) cha Sura ya 20 na Kwamba Swala Zima Lililopo ni Dhana ya Utunzaji wa Kielelezo yani Chain Of Custody. Na Eneo la Pili lilijielekeza kwenye Kanuni inayoifunga Mikono Mahakama Kufanya Maamuzi, Juu ya Kile Kilochokiamua hapo awali.

Na Eneo hili Linaenda Mamlaka ya Mahakama Kuhusu Kukisikiliza au Kukitolea Maamuzi Kwa lugha Nyingine Wenzetu kwenye Kanuni ya Issue Estoppel kwamba Kanuni hii inakubana Siyo Upande wa Mashtaka, Kwa Heshima zote Mheshimiwa Jaji Hoja zote zilizotolewa na Wenzetu Kwenye hoja hizo tatu hatukubaliani nazo.

Wakili wa Serikali: Na Ni Maoni hatukubaliani nazo zote. Zinakosa Miguu ya kusimama. Mheshimiwa Jaji katika Kujibu nitaomba nianze na Utangulizi ufuatao. Siye hatuelewi ilikuwa kwa Bahati Mbaya au Kwa Makusudi, Wanaipotosha Mahakama. Lini Mahakama hii ilifanya Maamuzi Kuhusu Detention Register ambayo inaombwa na Shahidi?

Sisi kwa Pamoja tunasema Hapana. Hakuna Wakati Wenzetu waliweka Pingamizi dhidi ya Hii Nyaraka tunayotaka Kuitoa na Hakuna Uamuzi Ulifanywa Na Mahakama Dhidi Ya Hii Nyaraka tunayotaka Kuitoa.

Wakili wa Serikali: Kilichoamriwa ni Shahidi Yule wa Kwanza alishindwa kuweka Misingi Juu Kielelezo Kilikuwa wapi na Kilifika Vipi Mahakamani na Hizo Ndiyo zilikuwa Hoja zilizotolewa na Kubishaniwa. Hapakukuwa na Shaka hiyo Kwamba hicho siyo Siyo Chenyewe kimechezewa

Na hata Leo hii hakuna Hoja hata Moja Kwamba Kielelezo hichi Sicho alichokotoa Mahakamani, Mheshimiwa Jaji siyo Katika Shauri la awali wala Sasa Palipo tolewa Hoja Kwamba Kielelezo hicho ni irrelevant na Siyo Material.

Mheshimiwa Jaji Ulichokifanya Uamuzi Mara ya Kwanza Ulikuwa dhidi Shahidi Mwenyewe Na siyo hiki Kielelezo, Mheshimiwa Jaji kwenye Maamuzi yako tunaomba Tukurejeshe, Kwamba Shahidi amekidhi Vigezo Vya relevance... Na Suala Lenyewe alishindwa Kuestablish Chain Of Custody.

Hakuna Mahala ulisema Kielelezo hiki kadha wa kadhaa, Mheshimiwa Jaji wanalolisema Halipo wala Mahakama haijawahi kulifanya, Mheshimiwa Jaji tunakubaliana na wenzetu kwamba ni Kweli Vigezo Vya Upokelewaji wa Vielelezo ni Vile Vitatu, Relevance, Competence na Materiality.

Wakili wa Serikali: Na Kweli Wakati PW1 anatoa Ushahidi Wake na sisi tunatoa Hoja zetu, Tulisema, Sisi Mheshimiwa Jaji tu atofautiama na Wenzetu Kwa namna Wanavyotaka Mahakama Iamini kwenye hilo Eneo, Kilichopo Mheshimiwa Jaji Siyo Vigezo, kinacho angaliwa ni Dhumuni, Kwamba Kielelezo kile kilipaswa Kutolewa.

Siye Haturuhusiwi Kupeleka Mahakama huko na Mahakama atakiwi Kufanya Maamuzi hayo, Mahakama Ilitakiwa Kwaajili ya Utambuzi, KATIKA Mahakama zetu Exhibit zilizokuwa zimetolewa kwa Exhibit Purpose Mahakama haiwezi Kuchukua na Kufanya Maamuzi yake.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kwa mantiki hiyo Utaona hata Mazingira ya PW1 na PW2. Hata Kama Mahakama ingefanya Maamuzi sisi hatufungwi, Mheshimiwa Jaji Nielekeze kwenye Sheria Case za wenzetu walisoma, Siye tunaomba tuipeleke Mahakama Mbali zaidi.

Ni Mazingira yapi Mahakama Inaweza Kukumbwa na Hali hiyo ni Kwenye Shauri la NIBUO COSMAS Vs JAMHURI, Shauri la Jinai na 519 ya Mwaka 2016 Mhakama ya Rufaa, Naomba Kusoma Ukurasa wa Saba Mpaka Kurasa ya Nane aya ya Mwisho.. Samahani Mheshimiwa kuanzia Msati wa Pili aya ya Mwisho.

Wakili wa Serikali: Katika kesi yetu hakuna Vedict Mpaka Sasa, Je Kuna Amri ya Mahakama Imeshaitoa Katika Madhila haya? Kwa sasa Kesi hii na Kesi ambazo wemeilekeza Mahakama haina Msaada Kwao

Jaji: Ukisema Mamlaka Unamanisha nini?

Wakili wa Serikali: Hizo Authority, Wameilekeza Mahakama Katika kesi ya NBC Ltd.

Wakili wa Serikali: Wakasema ni Paragraph ya mwisho aya ya Saba..

- ANASOMA

Jaji: Ukurasaa wangapi

Wakili wa Serikali: Ukurasa wa 10 Anasoma Mheshimiwa Jaji kilichopo hapa Awali iliikuwa Hoja Kilichopo kinafungwa Muda

- ANASOMA tena Ukurasa wa Saba

Wakili wa Serikali: Tofauti na hapa Mheshimiwa Jaji, Kilichokwepo ni Kutoa Utambuzi, Na Mahakama haikulikwa Kufanya Maamuzi dhidi ya Kielelezo Chenyewe, Hivi sasa Mahakama Inaalikwa Kwa Kutolewa kwa Kielelezo, Vitu Viwili tofauti kabisa, Kwa hiyo Mahakama mikono yake Haifungwi.

Mheshimiwa Jaji Vilevile Wenzetu walialika Mahakama hii Kwenye Mashauri Mawili, ISSA ATHUMAN Vs JAMHURI Wakaielekeza UKURASA wa 25 Mpaka 26.. Ukurasa wa 25 na Ukurasa wa 26 Mahakama Ilikuwa ikijadili Uwezo wa Matumizi Ya Kanuni hii.

Wakili wa Serikali: Hivyo Mheshimiwa Jaji ukienda kwenye huo Ukurasa, mimi naona, Sasa Mheshimiwa Jaji kuisaidia Mahakama Yako na wengine Kuelewa haya Masuala naomba nielekeze kuanzia Ukurasa wa Saba..

- ANASOMA...

Kwanza LAZIMA Pawe na lesi Mbili, Na Moja lazima liwe limetangulia

- Anasoma.

Sasa Mheshimiwa Jaji mie na Mwenzangu tunajiuliza hivi haya Masuala ni Mawili Tofauti, Kwenye hicho Kitendawili Jibu ni Hapana.. Mheshimiwa Jaji pia walielekeza Mahakama Kwemye Shauri la JULIUS MICHAEL AND FOUR OTHERS Vs REPUBLIC wakasema Ukurasa 6, 7, 8, na 9.

Wakili wa Serikali: Miye naomba nielekeze Mahakama Kwenye Ukurasa Wa 9.. Walichozungumza Ukirasa wa 6 Mpaka Nane Wanauunga Mkono niliyoyatoa..

- Anasoma...

Wakili wa Serikali: Hata hizi Mamlaka za Sheria walizoleta ilikuongeza Nguvu Kwenye hoja zao Bado nazo haziwakubali, Kwa sababu hizo Mamlaka Mbili zimewakataa.

Na siyo Sahihi Kwamba Kanuni ya ISSUE Estoppel inaifunga Mahakama, Hapana Inatufunga sisi Watu wa PROSECUTION. Siye tunasema Katika Mazingira yote hakuna Mahala wala mazigira yoyote Mahakama ilishafanyia Kazi, Na Tunaomba Mahakama Watupiloe Mbali Mapingamizi yao Kwa sababu Yamekosa Nguvu Kisheria, Mheshimiwa Jaji Nielekeze Katika Hoja ya Kwanza.. Katika Kuzungumza Hoja yao Waka zungumzia Exhibit Guidelines.

Wakili wa Serikali: Katika Kuzungumza Hoja yao Wakazungumzia Exhibit Guidelines, Anyway nisizungumze Sana Kuhusu hizo Guidelines, Wanataka Kutenganisha Trial Within a Trial iliyofanyika Kwa Mshtakiwa wa Pili na Shauri hili Kubwa la Kesi namba 16 ya Mwaka 2021.

Kwamba ni Vitu Viwili tofauti na Kwamba havitegemeani, Na hata Kinachofanyika Sasa ni Ku' separate Trial Within Trial, Hatuwezi Kuvitenganisha hivi, Vinaenda Sambamba Mpaka Mahakama Siku inatoa Hukumu ya Kuwaachia washtakiwa au Kuwatia Hatiani.

Wakili wa Serikali: Ya leo ni procedure tu ya ku' Admit tu Kielelezo.. Na effect yake haiendi Ku' dispose Kesi ya uhujumu uchumi. Mheshimiwa Jaji Utaratibu huu kwa sababu ni Utaratibu wa Kipekee ndiyo kunahitajika kuwe na Ushahidi Ndiyo Kielelezo Kiingizwe.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Utaratibu huu kwa sababu ni Utaratibu wa Kipekee ndiyo kunahitajika kuwe na Ushahidi Ndiyo Kielelezo Kiingizwe, Trial Within a Trial ni Process tuh ya Adminisbility, Sasa Mheshimiwa Jaji sote tunafahamu Kwamba Mahakama ili itoe Amri Lazima Kuwe na Maombi.

Na Hayo Maombi yote yanaongozwa na Kifungu Namba 394 (a) Sura ya 20 ya Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai, Na Kwamba Maombi yanaweza Kufanywa kwa Maandishi au Kwa Mdomo. Subsection inasema Kwa Wito au Kiapo cha Mahakama.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Wenzetu Wanataka Kuleta Chamber Summons au Lah tulete Maombi Yetu kwa Njia ya Mdomo, Haiwezekani kwa Sababu Asilia ya Maombi yako yataonyesha Umeyaleta Kwa ombi Gani.

Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Namna pekee Iliyo Bakia tukienda na Hiyo Leading Ilikuwa ni Kuomba Kwa Njia ya Mdomo. Mheshimiwa Jaji Wakati PW1 anatoa Ushahidi Wake Tulitoa Hoja na Hoja hiyo Ilitolewa, Na baada ya Maombi hayo Mahakama ikatoa Maelekezo Kielelezo hicho Kitolewe nasi tukakabidhiwa.

Wakili wa Serikali: Wakati tunakabidhiwa Wenzetu hawakupinga Kwamba haya Maombi Siyo badala yake walikaa Kimya, Wakati tunakitoa ndiyo wakaanza Kuweka Mapingamizi. Wenzetu Wakasema hawa mabwana Kuna Kitu walitakiwa wafanye.. Mheshimiwa Jaji Utaratibu uke tulioufanya Wenzetu waliupinga.

Kwamba tulitakiwa Tupate Order Kwa sababu ile kabrasha lilishafungwa na Likawekwa Store, Sasa wanatuchanganya Wenzetu.. Tumefuata Maelekezo Ya Mahakama Wenzetu Wanasema Hakuwa Sahihi Lazima ipatikane Amri.. Mheshimiwa Jaji hapa sasa lazima Ieleweke na lazima tuelewane.

Wenzetu Watuelewe nini tunachokitaka sisi. Sisi tunatambua hiki Kifungu cha 353 ambacho kinapatikana SEHEMU E ya Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai, Ambapo pale Kuna Kichwa Cha Habari Kinasomeka DISPOSAL of Exhibits.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji na sisi tunatambua Kweli Kwamba lazima Mahakama Itoe Amri yake, Lazima. KUWE NA AMRI YA MAHAKAMA. Kwa minajiri ya Kifungu cha 353(1) Kifungu Kinatoa Muongozo Kwa Mahakama. Je ni wakati wa Kufanya Amri ya Kufanya Disposal ya Kielelezo.

Kifungu hiki Mahakama itakitumia pale tu ambapo Kielelezo Kilitolewa Mahakamani na Mahakama Ikakipokea Kama Ushahidi, Na baada ya Kukipokea Shauri hilo limeenda Hadi Mwisho Mahakama Ikalikamilisha.

Mheshimiwa Jaji Shauri limesha, Hakuna Mtu anaye Mmiliki Kielelezo Kile na Hakuna mtu anayekuja Kudai Kielelezo Kile Mahakamani na Hakuna Rufaa iliyokatwa hapo Ndipo Mahakama itatoa Amri ya Kufanya Disposal.

Wakili wa Serikali: Mahakama lazima Iangalie namna ya Kuki' Dispose hicho Kielelezo.... Mheshimiwa Jaji Kwenye Shauri letu hali ni Tofauti. Sisi Hatujaomba Kielelezo hiko kiende Kukaa Kwa Mmiliki wa Kielelezo.. Hapana Hatujaomba hivyo, Exhibit P1 kwenda kwa Msajili Wa Mahakama, Yaani BARUA.

- Wakili wa serikali merejea kusoma Barua yote..

Wakili wa Serikali: Shahidi ameonyesha Lengo lake ni Kutolea Ushahidi, Hoja ya kwamba Sisi hatujapaswa Kukidhi Vigezo Kwa Mujibu wa Kifungu cha 353 sisi tunasema Hapana, Ingekuwa Shauri hili ni Tofauti Ingekuwa Sawa Lakini Sasa Shauri ni Moja na Tunachokitumia Kipo Ndani ya Kesi Moja hiyo hiyo, Na Hata Ukiangalia Muongozo Wa Wenzetu Kipengele Cha Nne na Cha Tatu Disposal of Exhibit is Done at the End, WS Ana Soma YOTE.

Wakili wa Serikali: Under Special Circumstances Disposal cab be Dane Before or During the Trial, Sasa Mheshimiwa Jaji Wenzetu Walitakiwa Waeleze Sasa hizo Special Circumstances Zilizotakiwa zifuatwe, Sisi tuna Kazia Kwamba huwezi Kutengenisha Trial Within a Trial na Shauri namba 16 ya Mwaka 2021.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Hoja yetu siye Tumekiomba Kielelezo Ili tukitumie kwenye Proceedings hizi hizi na Tumekileta tukitumie kwenye Proceedings hizi hizi, Sisi tunasema Siyo Kifungu cha 353 wala Muongozo wa Mahakama Ukurasa wa 19.4:3 unaweza Kutumika, Kwa sababu Mazingira Tofauti.

Wakili wa Serikali: Na hoja ya wenzetu ni kwamba kielelezo kimepatikana ILLEGALLY.

Jaji: Mmmmmmmmmhhhhhhhhhhhhh

Mtobesya: HAPANA HAPANA HAPANA

Wakili wa Serikali Chavula: Basi niweke hivi Kimekiuka Kifungu cha 353, Naomba Niwakaribishe Wenzangu

- Wakili wa Serikali Pius Hilla anasimama..

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Kwanza Naunga Mkono aliyo ya ongea Wakili Msomi Chavula, Lakini Submission yangu Itaendana na Kesi ya ABASI KONDO vs JAMHURI Criminal appeal namba 472 ya Mwaka 2017. Mahakama Kuu ya Dar es Salaam.. Mheshimiwa Jaji katika Shauri hili Mahakama Ya Rufani ilisema.

Kwamba Oral Evidence Is Sufficient without, Kwamba Where a Fact is Submitted Orally, Ita Does not need Documents To prove that Facts.. Mheshimiwa Jaji Submission Za Utetezi Ukiangalia Kwa Maana Yake Sababu Kubwa zimejikita kwenye Chain Of Custody.. Mheshimiwa Jaji, tayari ipo.

Kwenye Rekodi za Mahakama Kupitia Ushahidi Namna gani Kielelezo KILIVYOFIKA Mahakamani, Kilivyo Ombwa na hadi Kinaletwa Mahakamani. Hakuna Mahala Mahakama Yako Imeelezwa Kwamba Ushahidi huo hauna Maana Na haijafika Mahala Kusema kwamba Shahidi ambaye ameeleza hayo Is Relevant.

Wakili wa Serikali: Hakuna Kifungu Kinasema Kwamba Disposal ya Kielelezo ni Kwa Amri ya Mahakama, Sisi ni Wasilisho letu kwamba Administration ni Njia Moja wapo ambayo Shughuli Inaweza.

Jaji: hujamalizia..

Wakili wa Serikali: Kwamba Shughuli Inaweza Kupatikana hata Kwenye Utawala, Kwamba ni Wasilisho letu kwamba Kielelezo Kimetoka Kwenye Mikono ya Mahakama, Mheshimiwa Kwamba Ilitakiwa Exhibit Register Ilitakiwa Ionyeshe kwamba la la la.. hatuoni Umuhimu wa Hilo. Walikuwa Wanazungumzia Kuhusu Mwongozo wa Mheshimiwa Jaji Mkuu, Hatupo nao Mbali sana lakini page one ya Muongozo Paragraph ya Kwanza Mstari wa kwanza unasema,

- ANASOMA...

Wakili wa Serikali: Zinatakiwa Kusomwa na Sheria zinginezo, Sheria Kesi na Nyaraka zingine za Mahakama. Mheshimiwa Jaji Imekuwa submitted pia kwamba Detention Register Ina mapungufu ya Kisheria ndiyo Maana ilikataliwa hivyo haiwezi Kuletwa tena. Na Kwamba Litigation Must come to the end, Bila Kutumia Maneno Mengi Mheshimiwa Jaji ambayo ni Subject Matter ya submissions Yetu, Hakuna Mahala Imekuwa Declared Kwamba Siyo Competent Kwenye Procedure, Zaidi Ya kwamba ilikuwa ni swala la Shahidi.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Hoja ya kwamba Mahakama ipo Funtus officio kwa kutumia Kielelezo hiki, SIO sahihi. Hakuna Element ya Re-litigation Kwa Kuwa Kielelezo hicho Kilikuwa Competence na Pia Purpose haikuwa hiyo, Ni Submission Yetu Mheshimiwa Kwamba Hakuna Decision ambayo Ime' decide Detention Register Isipolelewe..

Jaji: nakukumbusha Ulisema Utazungumza kwa Kifupi sana, Sasa ushatumia Nusu Saa,

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa naomba Nimalizie tu Kesho.

Jaji: Naomba kuhairisha shauri hili mpaka kesho Saa 3 asubuhi Shahidi Utarudi tena kizimbani kesho regardless ya kitakachotokea, washtakiwa wataendelea Kuwa rumande chini ya magerezapaka kesho Asubuhi saa 3 Asubuhi.

Mwisho
 
Kwa kawaida mahakama hufanya kazi kwa siku 5 yaani Jumatatu to Ijumaa.

Kesi ndogo ya Msemwa kupanda kiximbani na notebook pamoja na simu iliibuliwa Ijumaa iliyopita na leo ni siku ya nne ndio tunategemea kupata maamuzi.

Mahakama za Tanzania zinajiendesha kwa gharama kubwa sana.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote!
 
Another day in court. Tunamsubiria Jaji.
JPEG_20211117_084815_7791875033840601815.jpg
 
Liko wapi lile jitu na wafuasi wake walizushaga, eti kina Mbowe wanatangulizaga wanyonge kwenye hizi vita za ukombozi wao na familia zao, waakula bata?! Eti “Mwambie aandamane yeye na mama ake!!” Mbowe ameubeba mzigo wa upinzani mwenyewe, na status ya ushujaa na u-Mwamba wa siasa za Tanzania ni haki yake! Mbowe ni mfano bora kujitolea maisha kwa kile unacho amini!
 
Tusubiri tuone pingamizi litatupwa au litakubaliwa?
 
Huyo gaidi anatupotezea muda watanzania ale mvua 30.

Mtandao wake wamelipua Uganda.
Hiyo ni statement Kutoka Lumumba! Islamic State wamejitangaza wamehusika, wewe kwa kuwa umezoea kubumba k esi inasema mtandao wavMbowe!
 
Mpaka hapa naona jaji kamhalalisha shahidi
 
Back
Top Bottom