Mtobesya : Kama Walikuwa na Order Ya Kuomba Kielelezo, hawakupaswa Kuomba Kwenye Proceedings hizi, Ni Ukiukwaji Mkubwa wa Taratibu na Mahakama Isingeweza Kuombwa Kitu ambacho Kimechukuliwa Kwenye Proceedings zingine na Kama Kweli walifanya hivyo basi Taratibu zingefuatwa kwa Mujibu wa 353 na Muongozo wa Mahakama. Na Kaka zangu hawa ni Mawakili Wasomi siwezi Kuwafundisha, Lakini Hilo halikufanyika na Kama Kilifanyika Basi Kimekiuka Utaratibu ninaousema.
Mheshimiwa Jaji Kama Kweli Proceedings hizi ni sawa Kwanini wanaomba Mahakama Ipokee tena Kwa mara ya pili Kwenye Shauri hili Kama Proceedings zote ni sawa na Kesi ni ileile? Kitendo cha Kuomba Ipokelewe tena na Mahakama ni Ushahidi Tosha Kwamba hili ni Shauri tofauti