Reallocation is equivalent to poor planning! Hivi viraka viraka katika hii case japo mi si mwanasheria, naona kabisa ina viashiria vingi vya uongo! Haikupangwa vizuri, na inaanika uonevu wa Serikali dhidi ya watu wake. Njia inayotumika ni ya kuzimu, kufanikisha ukweli usiyokuwa wa kweli.
Eee Mungu simama na waja wako. Haiwezekani hata mara moja Mwanajeshi akashirikiana na Askari Polisi kutafuta watu wa kufanikisha Ugaidi na kuifanya nchi isitawalike. Alafu akawaacha hao watu wa kufanya Ugaidi bila uangalizi wowote, na kumonitor kwa kutumia simu tu. Haiji akilini! Kwamba Serikali iliamua kutengeneza watu wa kufanya Ugaidi na Gaidi Mkuu kwa Maslahi ya nani Sasa!!!!
Sterling kauawa Kabla ya Pigo la Mwisho! Shida ni kwamba hata Trailer tu iliharibu mambo tangu kwa Mama wa Glocery na Mlima mbogamboga na wale wa PGO! Nia ya Serikali ingeishia hapo hapo, lkn kama ni kumtia mtu hatiani kwa kesi hiyo, itakuwa ni nguvu tu ya Serikali na siyo utekelezaji wa Sheria.
Mtunzi kafeli kuimalizia vizuri, japo naamini Moses Lijenje nae atakuja kutoa ushahidi namna alivyoamua kujiondoa kwenye mpango wa Ugaidi baada ya kugundua nia ovu ya Mbowe! Maana hisia zinaniambia kuwa mko nae anafundishwa Cha kuja kusema. Ni suala la muda tu, Mungu atasimama na mwenye haki.