Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Shahidi alinichanganya aliposema alitumiwa kwenye cm tshs 500,000/= alipoenda kuitoa akapewa cash tshs 499,000/=.
Kuwa makato yalikuwa tshs buku pekee. Hayo makato siyo hapa bongo,au labda kwa vile ni cm ya luten komandoo
Mkuu labda Urio alikuwa na salio zaidi ndo maana ikatoka hiyo figure .
 
Hapa kwenye huu uzi umevamiwa.. Ndio maana utaona kuna comments nyingi zinajirudia.. ..
Nchi yetu ina inteligensia kali sana lakini isiingizwe siasa tuu...ikiingia kila kitu kinaharibika..
ANGALIA OFISI YA CID
Yaani ofisi inapokea taarifa ya mipango ya ugaidi kisha mtoa taarifa anaambiwa we endelea tuu kuwatafuta vijana wa hiyo kazi kisha utakuwa unatutaarifu (hapa wakina Adamoo hawana hatia)
MFUMO WA INTELIGENSI
hapa ilitakiwa Boaz kama kweli kapewa taarifa ni kutafuta askari kanzu (undercover) kisha Urio anapiga simu wameshapatikana.. Then tuma nauli askari kanzu wanaenda Moshi.. Wanakuwa wanampa ulinzi Mbowe pamoja na mipango hiyo ya ugaidi ambayo Urio anasema..
CID kwakweli amekosea sana.. Maana kama kulikuwa na njama za ugaidi hawa askari kanzu wangesoma mchezo wote.. Wangekuwa wanajua nani na nani wapo wapi... Plan iweje... Mikoani sijui Moro.. Iringa.. Kukata miti barabarani nk
MATOKEO YAKE
Hakuna maelezo ya kutosha ya watu hao wanne wangefanyaje huo ugaidi kwa maeneo mbalimbali..
Tutabaki tunabishana humu ndani mpaka kesho kutwa.. Lakini Polisi... Urio wote hawakujipanga na hii issue kama kweli Mbowe alipanga ugaidi..
Extraction za simu zao ni hela kwenda huku na kupokelewa.. Hakuna voice record call kujua kilichozungumzwa
Zaidi ya SMS za happy new year.. Wasalimie nk
HII KESI ITAENDA KUAMULIWA VIZURI COURT OF APPEAL
 
Hicho kinachoendelea hapo mahakamani ni kesi iliyotengenezwa vizuri, au mimi ndio sijui kutengeneza vizuri nini? Kweli wazungu wakiendelea kutuita manyani hawakosei, huo utoto hapo mahakamani ndio uwezo wa vyombo vyetu vya usalama kifanya fabrication, duuu basi kazi ipo.
aa baki hivyo hivyo.
Wenzenu wanatumia huu upumbavu wenu kuwakandamiza.
Kesi imetengenezwa vizuri na stering ndo huyo kamanda urio.
Alimpigia DCI boaz simu .
Kazi NI kwako
 
Una nafasi mbili- ama uwe shahidi au uwe wakili badala ya Kibatala ila hutaweza muokoa Mbowe
 
ndo maana nasema mbowe alijichanganya kufanya kazi na hao wanajeshi.
Mpaka akawa anamtumia hela.
Katika akili hata za kawaida hauwezi kufanya mipango ya ulinzi na wanajeshi wakati wewe ni kiongozi wa upinzani.
 
Muambie jaji sasa amfunge Mbowe kwa hayo maneno ya Urio ili wewe na Kinuju mkale kitimoto huku mnakenua meno yote 32 nje
Sasa mnachobisha nini?
wakati mbowe na ulikuwa walikuwa wanapanga kutafuta vijana kwa ajili ya kufanya matukio ya ugaidi .kulipua vituo vya mafuta,kuchoma masoko,kufanya nchi isitawalike n.k
Anatoka vipi hapo?
 
Sauti alizorekodiwa wakati wanakutana zitawasilishwa.
Maana FM alikataa mazungumzo ya kwenye simu akasahau Kuna voice recorder.
Yajayo yanahuzunisha.
Hawo mashahdi waliopita akiwemo huyo IT wenu wa mchongo ambaye alikuwa na simu nane hakuonesha na alisema hajaona hayo sasa huyo ataeleta ni mamayo hizo sauti?
 
hakuna voice rekodi wakati mfumo unaweza na ulirekodi?
 
Kwahiyo commando anaenda kuwasagia kunguni makomandoo wenzake
Ajabu sana awatafutie msala huku akijua watakamatwa sio fair kabisa.
Kingine eti kukata miti wangetumia shoka au chain saw hadi wasionekane.
Nani angeandamana sasa
Kama kweli Mbowe alikuwa na aina hii ya plot basi huo ni ukichaa.
Kwa nini polisi wasingetafuta watu wengi zaidi kumnasa mbowe.
Kama kama kina Bwire walitumiwa kama chambo tangu awali huku Urio akiwa masterplan kwa nini wateswe na washakiwe.
 
Ndivyo alivyofundishwa ni mawakili wake na vitisho juu ili aongee hayo anayoongea yaliyoyakweli hajayagusa kuyaongea kama ushaihidi.
 
HII KESI ...WASHITAKIWA WOTE ....WANASHINDA.
 
Hawa akina adamoo na wenzake kimsingi hawana kesi kama hata baada ya kuajiriwa na mbowe waliendelea kuripoti kwa luteni urio
 
Ww nakufananisha na shabaki wa mpira ambaye akiingia uwanjani na timu yake kupata goli la mapema anaanza kushangilia kuwa ameshinda, kumbe mechi ni dakika 90. Hapo ametoa maelezo yake, atapaswa kutoa ushahidi usioachashaka juu ya hicho anachokisema. Subiri aulizwe maswali na mawakili wa utetezi, hapo ndio utajua huko kwenye vyombo vya dola kumejaa vilaza wanaondekeza siasa chafu.
Stering wa mchezo huu NI kamanda urio.huyo adamoo sio kitu chochote.
Urio ndo atakeyewatia hatiani.
 
kipi kilichoanza kutokea kuteswa kwa urio.
Au urio kumpigia Simu DCI boaz kumwambia mipango ya mbowe?
Urio na DCI Boaz wote ni wa upande wa mashtaka,kama wameamua kubambika kesi basi wanaweza kusema hata uongo!
Huenda hata hiyo simu haikuwahi kupigwa!Utajuaje?
 
Hamna kitu umejibu ati!!!
 
ndo maana nasema mbowe alijichanganya kufanya kazi na hao wanajeshi.
Mpaka akawa anamtumia hela.
Katika akili hata za kawaida hauwezi kufanya mipango ya ulinzi na wanajeshi wakati wewe ni kiongozi wa upinzani.
Kwahiyo majeshi ni maadui wa wapinzani?
 
Mawakili wa utetezi waende mitandao husika waulize gharama ya kutoa Tsh 500,000/ ilikuwa sh ngapi wakati huo,,maana haiwezekani 500,000 itolewe kwa makato ya buku
Hii haiwezekani,kabda kama wakala alikuwa hawara wa Urio
Basi hii kesi Mbowe ashashinda shahidi muongo hata kama alikuwa na mahusiano na Mbowe
 
Aliyetengeneza hyo kesi ni mbowe mwenyewe.
Anapiga simu kwa namba binafsi,akipigiwa apokei,anatuma hela kwa njia ya wakala.
Kwanini alikuwa anajificha ficha mawasiliano yake na urio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…