Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Hapa kwenye huu uzi umevamiwa.. Ndio maana utaona kuna comments nyingi zinajirudia.. ..
Nchi yetu ina inteligensia kali sana lakini isiingizwe siasa tuu...ikiingia kila kitu kinaharibika..
ANGALIA OFISI YA CID
Yaani ofisi inapokea taarifa ya mipango ya ugaidi kisha mtoa taarifa anaambiwa we endelea tuu kuwatafuta vijana wa hiyo kazi kisha utakuwa unatutaarifu (hapa wakina Adamoo hawana hatia)
MFUMO WA INTELIGENSI
hapa ilitakiwa Boaz kama kweli kapewa taarifa ni kutafuta askari kanzu (undercover) kisha Urio anapiga simu wameshapatikana.. Then tuma nauli askari kanzu wanaenda Moshi.. Wanakuwa wanampa ulinzi Mbowe pamoja na mipango hiyo ya ugaidi ambayo Urio anasema..
CID kwakweli amekosea sana.. Maana kama kulikuwa na njama za ugaidi hawa askari kanzu wangesoma mchezo wote.. Wangekuwa wanajua nani na nani wapo wapi... Plan iweje... Mikoani sijui Moro.. Iringa.. Kukata miti barabarani nk
MATOKEO YAKE
Hakuna maelezo ya kutosha ya watu hao wanne wangefanyaje huo ugaidi kwa maeneo mbalimbali..
Tutabaki tunabishana humu ndani mpaka kesho kutwa.. Lakini Polisi... Urio wote hawakujipanga na hii issue kama kweli Mbowe alipanga ugaidi..
Extraction za simu zao ni hela kwenda huku na kupokelewa.. Hakuna voice record call kujua kilichozungumzwa
Zaidi ya SMS za happy new year.. Wasalimie nk
HII KESI ITAENDA KUAMULIWA VIZURI COURT OF APPEAL
Sure, ila sting operation sio lazima ihusishe askari kanzu. Kosa walifanya hapa kina kingai ni kuwahisha ukamataji. Kama walitaka kumsave sabaya, wangemchepusha tu, ili hao macomandoo wakamatwe red handed. ,
 
Hivi hawa watu wako serious na mambo ya ugaidi kweli? Kama huyu Luteni alitoa taarifa kwa DCI na wakakubaliana aendelee na utaratibu kama walivyokubaliana na Mbowe basi kazi tunayo.
Hao makomando Mbowe alikuwa anawafahamu? Kwa nn wasipeleke polisi wapelelezi wakawa undercover kama ndiyo makomando ili kupata ushahidi mzuri?
Unajua hao kina adamoo sio undercover?
 
Sure, ila sting operation sio lazima ihusishe askari kanzu. Kosa walifanya hapa kina kingai ni kuwahisha ukamataji. Kama walitaka kumsave sabaya, wangemchepusha tu, ili hao macomandoo wakamatwe red handed. ,
Mkuu nimekuelewa sawa wangechepusha... Lakini hivi kweli umepewa taarifa na Mbowe nitafutie watu nahitaji kulipua vituo vya mafuta.. Kudhuru viongozi.. Kukata miti nk..
Halafu wewe kama Luteni wa Jeshi unatafuta wanafunzi uliowafundisha wapo mtaani... Unawapigia simu... Banaeeee njoooniiii...
Kuna kazi ya ulinzi Moshi kwa Mbowe..
Hawajui wanaenda kwakuwa ni VIP Protection... Kisha unawaunganisha kwa Kingai ili wadakwe kabla ya mission kufanyika.....
Huoni hao makomandoo wameonewa?
Huoni kuna kitu katikati? Huoni kuna shida sehemu?
 
Angekuwa undercover Adamoo asingeweza kusema tulimsikia Urio akilia kwa uchungu Tazara katika case ndani ya kesi... Anyway watu hawaifuatilii hii kesi..
Huyo Urio kala kibano cha kimataifa.. kuna kitu hapo
Uko sahihi kabisa kwa wanafuatilia wanafahamu adamoo aliwahi kusema walisikia luteni Urio analia walivyokuwa tazara
 
Hili hoja ungemtumia Kibatala amulize Shahidi....

Hoja mzuri sana
Naamini akina Kibatala na team yake wanapita huku kuona matobo ambayo pengine wameyasahau!Kesho kitaeleweka!Shahidi huyu ataugua ghafla!
 
Hizo namba alizokua anapigia na mbowe amvazo sio zake shahidi alimpa Kingai?

Kumbuka aliambiwa awe anaripoti kwa Kingaki matukio yote...

Kwakua mbowe alikua anatumia namba za watu, hao watu walimamwatwa kutoa ushahidi kwa simu zao kutumiwa mbowe?
Kumbuka enzi hizo palikua na mtambo wa israel,,, kama hii ishu ni kweli lazima kuna audio evidence
 
Naamini akina Kibatala na team yake wanapita huku kuona matobo ambayo pengine wameyasahau!Kesho kitaeleweka!Shahidi huyu ataugua ghafla!
Huyu urio na kingai hakuna walichokifanya. Wanapotezea raia muda wao na kutumia pesa za walipa Kodi bila sababu. Ikiwezekana wafunguliwe mashitaka kwa usumbufu.
 
Mkuu nimekuelewa sawa wangechepusha... Lakini hivi kweli umepewa taarifa na Mbowe nitafutie watu nahitaji kulipua vituo vya mafuta.. Kudhuru viongozi.. Kukata miti nk....
Bwire ndo alumwambia urio kuwa madogo wameenda moshi kum Term sabaya,

Urio akatoa ripoti faster kwa kingai kwamba kuna wet mission iko on progress, nadhani kina kingai wakampanick na kupelekea kukamatwa kwa madogo kabla hajatekeleza mission(if true)
 
Bwire ndo alumwambia urio kuwa madogo wameenda moshi kum Term sabaya,
Urio akatoa ripoti faster kwa kingai kwamba kuna wet mission iko on progress, nadhani kina kingai wakampanick na kupelekea kukamatwa kwa madogo kabla hajatekeleza mission(if true)
Sawa mkuu basi tuendelee kusubiri..
itabidi extraction ya simu ya Bwire kwa Urio (voice call) kwa tarehe husika..
Tusubiri...
 
Logically:

Urio ni muongo wa kutengenezwa.

Hivi watu unawaambia Kuna kazi ya ulinzi kwa mh.Mbowe,halafu unawaambia wakiona vitendo vya uvunjifu wa amani wakutaarifu?
Haya ni matukio mawili ambayo yamelazimishwa yatokee kwa wakati mmoja.
BUT
God is the rightiest.
 
Kwamba urio alikutana na mbowe,

Mbowe kamuomba urio amtafutie wanajesh wastaafu wa kufanya vurugu inchi isitawalike,

Urio kaenda kuwadanganya makomandoo kwamba kuna kesi ya ulinzi akishirikiana na Boaz na Kingai,

Makomandoo wanaingia kwenye mtego wakijua wanaenda kufanya kazi ya ulinzi,

Then wanakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kukusudia.kufanya ugaidi?

Hii inchi wote tunafanywa mazuzu
 
Unajua hao kina adamoo sio undercover?
Undercover halafu wahenyeshwe mahabusu mwaka mzima huku Mbowe akiwa uraiani!
Undercover wangesemaje chini ya kiapo kuwa waliteswa Ili wasaini maelezo yaliyoandikwa na Polisi?Think deep,Urio mwenyewe kasema kuwa akina Adamoo aliwaambia kuwa wanahitajika Kwa kazi ya ulinzi!
Sasa hapa unajaribu kusemaje?
 
Back
Top Bottom