Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe na wenzake: Kaaya amaliza kutoa ushahidi. Shauri kuendelea 29/10/2021

Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe na wenzake: Kaaya amaliza kutoa ushahidi. Shauri kuendelea 29/10/2021

Kwa cross-exam ya leo, case closed! Mbowe Januari 2020 alikwa gerezani Segerea lakini wakati huo huo alikutana na Shahidi Kaaya huko Longido! How possible was that?....
Mkuu dudus kwa ubora wa andishi hili naomba niweke Mahali pa msomaji wako kupata ukweli wa kile ulichoandika kwenye Biblia ktk kitabu cha
Kutoka 14: 15-25
 
Huyu shaidi kwa ufupi ilitakiwa kuwa mahabusu ili kupunguza mashaidi wanaojitokeza wa kusukwa sukwa kuwa fundisho.

Katika kesi inayoendelee inaonyesha maishaidi wengi ambao wakitoa ushaidi walitakiwa kuwa mahabusu ili kesi kuendelea vizuri. Ushaidi wanaoutoa kesho wakiulizwa wanajibu vingine !

Hili swala mnalionaje hapa JF
 
"Upande wa utetezi ameongezeka Wakili Niyikiza Seth Jacob, ametokea Bukoba mkoa wa Kagera Kuja kuongeza nguvu katika kesi ya Mbowe na wenzake."

Wapiga mayowe mitandaoni walikuwa wanasema hii kesi rahisi sana, sasa huu utitiri wa mawakili wa nini wakati kesi ni rahisi sana?
Akili ndogo, huwezi kujua mambo ya kisheria. Wewe kalinde kaburi.
 
Jichekee tu best angu maana mwaka huu tutaona na kusikia mengi, mtu anasema eti amebatizwa jina la Power khaaa nitafurahi nikilijua hilo Kanisa!!
Itakuwa AMEC. Wale wameru waliojitenga na KKKT baada ya yale mapigano ya miaka ya 90.
 
Huyu "shahidi" wa kuokoteza hana kabisa akili ndogo maana anatongoza likungu linalomzidi hata mama yake umri. Very useless boy.
kinachoendelea mahakamani ni Ze Comedy Hakimu ana maamzi yake mfukoni.
kwa mara ya kwanza nahisi giza kuishinda Nuru.
 
IGP hawa wanaondaa kesi hizi ama ziwe za kweli au za kubambikiziwa wanaku fedhehesha hawana weledi wowote
Waliomkoch Kaaya inakuwa kama konyagi ilikuwa inatembea vichwani vyao.
 
Cross examination ni sanaa kama zilivyo sanaa nyingine, ukisoma vitabu na kuwatazama mawakili nguli dunia namna wanavyofanya cross examination unaweza kusema kama wanafanya mzaha vile, ila kombora la mwisho watakalorusha uangamiza ushahidi wote, cross examination naweza kuifananisha na mchezo wa draft yaani unampa mpinzani wako kete moja ashangilie ila baada ya muda anajikuta amepoteza nusu ya kete zake zote.

Dhumuni kubwa na cross examination ni kuionyesha mahakama kuwa ushahidi unaotolewa na shahidi hauna mashiko, kwa hilo naona Kibatala amefanikiwa kumfanya shahidi kujikanyaga kanyanga na kuchanganya mambo, japokuwa mimi sio shabiki wa Kibatala ila kwa mtazamo wangu naona uharibifu wa ushahidi alioufanya kwa upande wa jamhuri ni mkubwa, mawakili wa serikali wamejitahidi kusawazisha ila naona kama hawajafanikiwa kwa kiasi kikubwa.​
 
Back
Top Bottom