Yaliyojiri katika Uzinduzi wa Ukumbi mpya wa CCM Dodoma

Yaliyojiri katika Uzinduzi wa Ukumbi mpya wa CCM Dodoma

Fukara

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2013
Posts
1,625
Reaction score
928
Mgeni rasmi ni Rais Jakaya kikwete, namuona Ali shein, Kinana na Makamu wa rais Billal.

Rais kikwete anatoa hotuba fupi na kuwashukuru watanzania na wana CCM

Hitilafu inatokea mic zinagoma wanabaki kushangaa.

Bado anazungumzia jengo jipya na kuhusu pia niya ya kukodisha jengo hilo kwa shughuli mbalimbali.. anasema CCM inaviwanja vingi na vingine wakubwa wanagawana.

Anawasifia UVCCM, UWT,na Jumuiya ya Wazazi kwa kuonyesha mfano mzuri kutumia viwanja vyao vizuri, kuwekeza kwa tija

Namuona pia balozi wa China.

Anawashukuru wajenzi na kumshukuru Kinana na kumuita 'jembe' shukurani maalum anasema ukiona vya elea ujue vimeundwa.

Rais anazindua jengo rasmi wajumbe wa kamati kuu wanaitwa na ndugu Nape kupiga picha na rais.

Rais na balozi wa china wanafungua jengo kwa kufungua pazia, kwenye jiwe la msingi

====
Ukumbi huu una uwezo wa kubeba zaidi ya watu 3,000 na ulianza kujengwa na kampuni ya CRJE mwaka 2014. Jina rasmi la ukumbi ni CCM Convection Centre. Shughuli imeanza muda na anaeongea kwa sasa ni mwenyekiti wa chama.

Kikwete: Sera ya kujitegemea ndani ya chama sijui kama inasomwa, sera yetu sisi ni wafadhili. Kuna vitu tunavyoweza tukavifanya na tukapa pesa yetu clean kabisa, ni wakati sasa katibu mkuu tukaunda ofisi ya inspector kwenye chama chetu, tena sio auditor bali inspector kabisa.

Mikoa yenye viwanja waombeni Jitegemee waje, hiki chama hakina sababu ya kuwa kinaomba omba kwa rasilimali tulizanazo, tufungue jengo letu na tulitumie kwa tukio la kihistoria.

Nawashukuru wajenzi, namshukuru katibu mkuu 'jembe', usione vianaelea ujue vimeundwa. Ukitimiza wajibu wako umefanya jambo jema na sasa tufungue jengo letu. (King'ora kinabonyezwa na mwenyekiti kuashiria ufunguzi)

====
RAIS KIKWETE AFUNGUA UKUMBI MPYA WA MIKUTANO WA CCM, MJINI DODOMA JULAI 09, 2015

MMGL1152.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza wakati wa wakati wa hafla ya ufunguzi wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, uliopo njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, mjini Dodoma leo Julai 9, 2015.Kulia kwake ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal na kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Mzee Phillip Mangula.

MMGL1187.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akibonyeza kitufe cha kengere kuashiria ufunguzi rasmi wa Ukumbi mpya na wakisasa wa mikutano wa CCM unaofahamika kwa jina la Dodoma Convention Centre, uliopo njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, mjini Dodoma leo Julai 9, 2015.Kulia kwake ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM – Bara, Mzee Phillip Mangula (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.

MMGL1207.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing wakifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Ukumbi mpya na wakisasa wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, uliopo njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, mjini Dodoma leo Julai 9, 2015.

MMGL1261.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Kikwete, akimkabidhi mfano wa ufunguo wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana, baada ya kuufungua rasmi ukumbi huo leo Julai 9, 2015 mjini Dodoma.

MMGL1311.jpg

Picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali baada ya uzinduzi huo.

MMGL1328.jpg



MMGL1333.jpg


MMGL1334.jpg



MMGL1349.jpg


July 9, 2015 |
Chanzo: Ikulu
 
Jogoo awike asiwike lazima kutakucha tu.

Mtajizungusha sana lakini finally lazima mje na MAJINA MATANO ya wana-CCM!

Wanaotakiwa kufanya maamuzi WANAOGOPA.

Wanaosubiri kufanyiwa maamuzi nao WANAOGOPA!
 
Chadema bado wanapanga hili nalo watasema ulikuwa wa tanu ,ruzuku zote chagadema wanatumia kukodia chopa
 
CHADEMA maskini hebu na nyie tuonyesheni jengo lenu.Ruzuku sijui huwa mnapeleka wapi.Majengo hamjengi kutwa kuzurura mabarabarrani na magari ya kifahali
Kama si uzalendo wa waasisi wa CCM leo hii kila mali mlizochuma toka TANU wangekuwa nazo mafisadi wakubwa ndani ya lichama lenu.
 
MTEI SACCOS na nyie jipangeni angalau mjenge hata Room mbili kwa ajili ya chama chenu.

Toka mwaka 1977 mpaka leo mwaka 2015 takribani miaka 38 imepita ndio mmejenga hilo jengo, wakati mwingine huwa mnajitoa ufahamu?
 
Kwa kweli nimeona wivu chama changu kina nguvu ila hata ofisi ya chama tu tumeishia kukodi

Unajua chanzo cha hela ya kujengea hilo jengo? usichokijua ni kama usiku wa kiza.
 
Back
Top Bottom