Nkurukumbi
Senior Member
- Sep 6, 2013
- 196
- 77
habari wanajanvi, mda huu dodoma hali si ya kawaida kama ilivyozoeleka , wapambe watia nia mbali mbali wameonekana kusononeka sana na wengine kutoweka kabisa karibia na eneo la tukio la mchakato mzima wa kumpata mtia nia, wameanza kuwapunguza wengi hasa ambao hawana vigezo kamili na mlolongo wa ukataji ulikuwa hivi
1. ametolewa ambaye elimu yake si sawa na anayetakiwa, yule mtia nia wa kigoma mr mahale,
2.wakatolewa wenye kashfa nzito sana na ni vigumu kuwasafisha hapa tuna, edward lowassa..richmond, . sospeter muhongo ,, tegeta escrow, sumaye.. uuzwaji wa nyumba zza serikali na uuzaji wa mashirika ya umma ovyo, membe kaponea chupuchupu kukatwa ana makundi ya kukigawa chama, wasira ana kashfa ya rushwa mwaka 1995,
3.uzoefu na umri, japo wote wametimiza umri lakini bado hawajawa na uzoefu wa kutosha, hapa ni kigwangala, na mwigulu nchemba.
waliotangulia kuingizwa kwenye list ni
1.asha rose migiro gender factor , uwajibikaji wake na usafi wake
2.augustino ramadhan zanzibar factor na kutokuwa na makundi na uwajibikaji wake,
3.makongoro nyerere, uwajibikaji na kuchukia rushwa kukemea hadharani wala rushwa na hali ya juu ya uthubutu kwenye maslahi ya wengi hana woga, pia nyerere factor usafi na kumuenzi mwalimu nyerere,
4.pombe magufuri, uwajibikaji wake na hasa kutekeleza sheria bila kupindishwa, na muwajibikaji wa hali ya juu
5. mizengo pinda , ni kiongozi mkuu wa serikali imekuwa vigumu serikali yenyewe kushindwa kutompitisha mtekelezaji mkuu wa ilan ya chama hicho bungeni na pia akikatwa itaonekana serikali nzima ilikuwa haifai, pia ni mtu msafi mwenye busara
6. samwel sitta, kwakuwa anasimamia sana matakwa ya chama na ameweza kutoyumbishwa wakati wa katiba mpya, amepitisha mapendekezo asilimia kubwa yaliyokuwa yanapendelewa na chama chake,mbali ya hapo ana uthubutu na ni mwajibikaji,
7.mark mwandosya
8.bernad membe
hapo ndo itatoka tano bora ,tatu mpaka moja bora,
Hivi mnajisikiaje mkitumia muda mwingi kuandika habari za uongo mtupu wakati hamna kitu kama hicho. Tulia Nape ataleta habari rasmi. watu tunaingia jf ili tuone Nape kaongea nini baada ya vikao make hizo ndizo habari sahii na rasmi kama huna habari tulia kama sisi usubiri jibu utalipata leo hii.