Wakuu habari,
Ntakua nawaletea Update ya kile kinachojiri kwenye Vikao vya CCM vinavyoendelea Dodoma. Ntahakikisha kila kitu naweka hapa.
Karibuni sana.
====================
Updates;
1. Update;
Sasa mchakato unaanza rasmi, Wajumbe kamati ya Maadili wanaingia Ukumbini, CC itafuata, haijajulikana kama na NEC itafanyika leo, itategemea na muda utakao tumika na vikao viwili hivyo.
2.Update
Rais Kikwete ameingia Ukumbini muda huu
3. Update
Kikao cha Usalama na maadili kinaendelea. Hiki hata kikiisha hakina briefing. kama kawaida, Ulinzi umeimarishwa na state
4.Update
Wakuu Kuweka Updates sio lahisi kama mnavyodhani sababu ulinzi ni mkali na hakuna aliyeruhusiwa kuingia na simu. Kumbuka hii ni kamati ya maadili, hivyo kuweni wavumilivu. Kikao kinaendelea.
5.Update 14:46
Kamati ya maadili imemaliza kazi yake, sasa ni zamu ya CC kuingia, lakini Rais Kikwete katoka, Kikao kitaanza akirudi.