Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Tujipange tuwe na mshikamano wakati huu shetani akipita. Ccm tuwe makini Sasa ni Makofuli kanda ya ziwa ni mtaji
 
kumbe watu ndio wanatongozaga hivi mie sikujua bwana. tunasubiria hiyo saa 3 tumpate Membe au magufuli bwana. sasa tufanyeje tena?

Inaonekana wewe ni mdau wa rangi ya kijani, mgombea unayemkubali ni yupi kati ya hao
 
Mawe yote, miti mikubw, mibuyu, makalavert na madaraja kwenye bara bara kuu nchi nzima yameandikwa Mwigulu raisi 2015 ..... sasa anayo kazi ya kufuta hayo maandishi yote
 

Ni kweli Osangobantu.
Tuache makundi sasa tuungane na kujenga chama. Mungu humuinua mtu kutoka mavumbini na kumketisha na wafalme. Nimeamini mpango wa Mungu ktk maisha ya mtu hauzuiliwi na wanadamu.
Queen Esther
 
Ukawa ndio mkombozi wa watanzania .

Tanzania ni nchi nzuri sana. Watu wake hawaeleweki na ndiyo maana watabiri na masangoma hupata shida sana. Leo hii wanaodaiwa kuwa ni mafisadi utashangaa wakihamia ukawa wakachaguliwa kuwa rais. Sasa utajiuliza watanzania tunapenda chama au tunapenda watu.Kama ni chama hakuna chama chenye watu wasafi tu. Na kama ni mtu vyama vyote vina watu wasafi. Elimu ya uraia inahitajika sana. Ushabiki ndio umeteka nafasi ya uelewa. MUNGU TUNUSURU WANAO.
 
Hii tabia ya kuweka Foreign Affairs Ministers kuwa marais inatugharimu sana, wote waliopita huko ni wezi. Wamekuwa wakiishi maisha yao yote kwa ujanja ujanja tu na kutafuna pesa za walipa kodi bila kufahamu zinapatikana vipi? Hawafahamu matatizo ya nchi yetu.
 
Safari yetu ya matumaini imeishia njiani baada ya kumkata lowassa na kumwacha membe, kwa taarifa tu lowassa mlimkata kitambo kabla ya kutangaza safari ya matumaini. Mkateni na magufuli asiingie 3 bora ili mfunike kombe huyo mwanaharamu apite!
 
Mawe yote, miti mikubw, mibuyu, makalavert na madaraja kwenye bara bara kuu nchi nzima yameandikwa Mwigulu raisi 2015 ..... sasa anayo kazi ya kufuta hayo maandishi yote


njia yote huko singida mpaka manyara yameandikwa hivyo kuanzia jumatatua akafute maandishi yake
 
watu wa Lowasa watapiga kura za kutoa adhabu watampitisha Amina kuwa mgombea wa kupambana na UKAWA ,magufli hayumo kwenye tatu bora watu wa Lowasa wamefanya hivyo kkiweka chama halijojo mbarikiwe sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…