Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

wakuu hapa dom tupo kwenye vikao vya ndani ndio tunakamilisha.
 
Chinja fisadi hilo, safi sana. At least CCM sasa wanaweza kusimama mbele yetu

Nani si Fisadi hapa Tanzania ? Ufisadi Upo kila kona kote watu ni mafisadi Hakuna Msafi ccm labda wazazi wako pekee.
 
Kamandaa na wewe unaamini kweli hiyo account ni ya Lowassa?

Usishangae akiamini kwani wengi tunapenda kusikia vile tunavyovipenda japo vinaweza kuwa ni dhihaka ya karne!!!
 
Ukawa wanaombea Goli la mkono la Nape ccm wampitishe Membe ambaye ni dhaifu sana ili Ukawa wapate kuingia ikulu kiulaini .

ccm wakimpitisha membe mbna ukawa watashinda bila kufanya kampeni
 
JINA la Edward Lowassa, mmoja wa wasaka urais kwa udi na uvumba, limeenguliwa katika hatua za awali za kinyang'anyiro hicho.
"Ni kweli jina la Lowassa limeondolewa katika kinyang'anyiro hiki. Baadhi ya wakubwa wamekuja na msimamo na wameapa kutosikia mtu anayeitwa Lowassa likikatiza na kuingia NEC," ameeleza mtoa taarifa wa gazeti hili.

Vikao vya uteuzi vya CCM – Kamati ya Maadili, Kamati Kuu (CC) na Halamashauri Kuu – tayari vimeanza mjini Dodoma mchana huu. Kikao cha NEC kinatarajiwa kuanza saa mbili usiku.
Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema, ikiwa Lowassa ataondolewa katika kainyang'anyiro hicho katika hatua za awali, basi ndoto za mwanasiasa huyo kushika madaraka ya juu katika nchi, zitakuwa zimezimwa.

Lowassa amekuwa akihaha kutaka kuwa Rais wa Jamhuri tangu mwaka 1995, ambako alijitosa kugombea nafasi hiyo.
Hata hivyo, jina lake liliondolewa katika hatua ya awali baada ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere "kumng'ang'ania" na kushinikiza kuobdolewa kwa jina lake.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Lowassa hakujitosa katika kinyang'anyiro hicho; badala yake alimuunga mkono Kikwete kwa makubaliano ya kufanywa kuwa waziri mkuu na baadaye kuwa rais.

Habari zinasema, kuzimwa kwa ndoto za Lowassa, kunafuatia taarifa kuwa mchakato wa uchujaji majina ya wasaka urais kupitia CCM, kuendeshwa na baadhi ya vigogo kutoka idara ya usalama ambayo imesheheni "wabaya" wake.
Lowassa, mwanasiasa machachari katika siasa za CCM, ni miongoni mwa makada 38 wa chama hicho waliochukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa na chama chao kugombea wa urais wa Jamhuri.

Inaelezwa kuwa vita ya kisiasa anayopigana Lowassa kwa sasa, siyo tena kati yake na chama chake, bali ni kati yake na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).
Mgogoro wa Lowassa na TISS unatokana na ukaribu wa mwanasiasa huyo na aliyewahi kupata kuwa Mkurugenzi mkuu wa idara hiyo, Apson Mwang'onda.

"Lowassa akiteuliwa kugombea nafasi hiyo, atakuwa amewashinda watu wa usalama waliopo sasa; jambo ambalo haliwezi kukubarika," kimeeleza chanzo kimoja cha taarifa mjini Dodoma.
Anaongeza, "…ikiwa hivyo, maana yake ni kuwa TISS iliyoko kwenye uongozi wa sasa itakuwa imeonyesha udhaifu mkubwa mbele ya Apson anayeratibu mbinu na mikakati ya Lowassa."

Mkurugenzi wa usalama wa sasa, Othuman Rashid anadaiwa kumuunga mkono Bernard Membe, mmoja wa wasaka urais anayetajwa kuwa chaguo la Kikwete.
Katika hatua nyingine, taarifa zinamnukuu mmoja wa viongozi wa kamati kuu akisema, chombo hicho muhimu katika uteuzi wa wagombea urais, imegawanyika.
"Mgawanyiko unatokana na baadhi ya watu kutaka Lowassa asikatwe, huku wengine wakisema, sharti aondolewe," anasema mmoja wa watoa taarifa wa gazeti hili.
 
Kwani Wewe Mkoroshokigoli Sifa Za Mnafiki Huzijui? Yeye Si Ameshatoa Hadi Uzi Wake Kuwa Lowassa Kakatwa Sasa Ananiuliza Nini Tena?

acha hizo ww mnyarwanda yaan unazira kisa mmoja kakuudhi?
Tupe taarifa bhana kama hutaki hata kesho tutaipata
 
Last edited by a moderator:


Akili Zetu Laiti Zingekuwa Zinafanana Na AVATARS Zetu Sijui Ingekuwaje!
 
Ametumia fedha nyingi sana katika kampeni.
Pengine ndio mtangaza nia aliyeanza kukampeni mapema kuliko mtu yeyote kati ya wagombea kuteuliwa kuwania kiti cha urais na chama chake.

Amesubiri nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka kumi.
Alikuwa mtandao, alikuwa na bado ana marafiki wengi.
Anazo pesa za kumwaga.

Mikajati mixito sana anayo.
Lakini masikini wale wampendao ni karibusawa na wale wamchukiao.Jina lake likitajwa kuna wanafyonza na kutema mate, wengine wanamuimbia sifa na kupiga vigelegele.

Mwisho wa siku ni jopo la wazee wenye mvi nyingi na wajuao kuonyesha njia.

Masikini Lowassa atalalaje leo?
 


Sawa, asante sana!..kama ni kujua tutajua muda ukifika; sio lazima tujue kutoka kwako. Endelea na matusi yako. Pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…