Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Atakapoteua Cabinet yake ajiepushe sana na hawa wanamtandao. Wataanza kuusaka urais naye akiwa madarakani.
 
Kweli chama cha mapinduzi mnatisha sana, yaani mlichofanya ni sawa na kukaba mwili wa messi wakati ana mpira obviously utaaibika tu, ndugu zangu UKAWA wameshindwa hata pa kuanzia na wasiwasi wangu mechi itaisha 6-0 labda mechi iahirishwe.
 

Mkuu, ni bora ukapunguza miemko ili uweze kuwasilisha hoja.

Ninacho jaribu kuonyesha hapa ni kwamba, ccm hamjui nani anayeitajika kwenye Taifa hili ninyi mnachoangalia ni nani atakayewabeba wafalme wenu na kuficha siri zao.

Ni lazima nimjadili yoyote yule atakayepitishwa na chamama chochote kile ili agombanie uraisi wa nchi yangu.

Kwani atakayepita ni9 lazima atakuwa Raisi wangu ata kama sikumchagua.

Hivyo ninaposema Magufulli ni mkabila/mshamba/anadharahu/kiburi namaanisha kweli kwasababu nataka watanzania wapime na kuiakikisha hatuongozwi na watu wa aina hiyo.
ulitaka achaguliwe nani kama wewe huna mihemko hadi unasema eti mkabila kana kwamba wizara alizowahi kuziongoza alijaza wasukuma thibitusha ukabila wake ,na ushamba wake ili nione kama kweli unahoja by the way kura tayar magufur ndo kapeta na lowasa hahami
 
ukijumlisha hizo kura zote unapata karibia 2600 na tumeambiwa wajumbe wapo 2400 na kidogo swali je mpk wenyewe wanajiibia kura?
 
Atakapoteua Cabinet yake ajiepushe sana na hawa wanamtandao. Wataanza kuusaka urais naye akiwa madarakani.
WildCard,

Naona umeishampitisha kabisa Dr.Magufuli, vipi UKAWA hawawezi kuchukuwa dola na kuunda cabinet.
 
Hahaha Michepuko ooyeeee! Wasichana wa UDSM mtafaidi mpaka kufa maana Shemegi atakua Raisi wa nchi, endapo UKAWA watachemka. Wale wa mabibo alikua anakuja usiku sasa atakuja mchana kweupe. Ulipokua waziri watoto walikiona cha mtema kuni, sasa unataka kua raisi.. Tanzania nzima yako dah
 
Jamii forums limekuwa jukwaa la umbea km Facebook. Badala ya kuweka feedbacks, wanaongelea mambo mengi ambayo hayapo.Wakati mwingine badala ya kuandika bora uwe unasubiri mpaka upate uhakika wa hiyo habari kwanza.

You are right mkuu
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimempitisha Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kupitia chama hicho. Anandika Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

❝
Katika Mkutano Mkuu uliofanyika usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma, Dk. Magufuli amechaguliwa kwa kura 1560 akifuatiwa na Asha-Rose Migiro aliyepata kura 702 huku Balozi Amina Salum Ali akipata kura 349.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, Dk. Magufuli amepita kwa kura hizo kutokana na nguvu yake dhidi ya wagombea wengine.

“Hakukuwa na namna hapa kwa kuwa, wajumbe wanaamini katika mazingira haya magumu ya upinzani Dk. Magufuli anaaminika na kukubalika nje kuliko hawa wengine,” anasema mtoa taarifa na kuongeza;

“Baada ya kutemwa Membe (Bernard Membe) kwenye NEC kila mjumbe ambaye alikuwa upande wa Lowassa (Edward Lowassa) alipumua jambo lililomrahisishia Magufuli.”

Mkutano huo umehairishwa mpaka saa nne asubuhi, ambapo ndiyo muda ambao Dk. Magufuli ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki na Waziri wa Ujenzi atatangazwa rasmi kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho.

Awali ndani ya ukumbi wa mkutano, kulidawa kuwepo kwa mpango wa wafuasi wa Lowassa kutaka kumpitisha Balozi Amina ili chama hicho kipate changamoto katika ‘kumuuza’ kwa wananchi ikiwa ni kulipiza kisasi kwa kukatwa mtu wao (Lowassa).

Katika Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho, majina yaliyopitishwa yalikiwa ni Migiro, Magufuli, Balozi Amina, Membe na January Makamba.

Katika Halmashauri Kuu ya CCM yalipita majina matatu ya Dk. Magufuli, Dk. Migiro na Balozi Amina.

Magufuli mgombea Urais CCM | MwanaHALISI Online
 
Back
Top Bottom