Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Wakuu habari,

Ntakua nawaletea Update ya kile kinachojiri kwenye Vikao vya CCM vinavyoendelea Dodoma. Ntahakikisha kila kitu naweka hapa.

Karibuni sana.

===================

Updates;

1. Update;
Sasa mchakato unaanza rasmi, Wajumbe kamati ya Maadili wanaingia Ukumbini, CC itafuata, haijajulikana kama na NEC itafanyika leo, itategemea na muda utakao tumika na vikao viwili hivyo.

2.Update
Rais Kikwete ameingia Ukumbini muda huu

3. Update
Kikao cha Usalama na maadili kinaendelea. Hiki hata kikiisha hakina briefing. kama kawaida, Ulinzi umeimarishwa na state

4.Update
Wakuu Kuweka Updates sio lahisi kama mnavyodhani sababu ulinzi ni mkali na hakuna aliyeruhusiwa kuingia na simu. Kumbuka hii ni kamati ya maadili, hivyo kuweni wavumilivu. Kikao kinaendelea.

5.Update 14:46
Kamati ya maadili imemaliza kazi yake, sasa ni zamu ya CC kuingia, lakini Rais Kikwete katoka, Kikao kitaanza akirudi.


6. Update 16:00
Wajumbe wa CC ndo wameingia sasa hivi, watapewa majina matano
na kamati ya maadili ya Wagombea urais.

7.Update 16:55
Team inayomuunga mkono Edward Lowassa zaidi ya watu 200, wamekutana mchana huu Katika Ukumbi wa St. Gasper, kuweka msimamo iwapo huyo wanayemtaka hatakuwemo kwenye Top 5 ya Wagombea waliopitishwa na kamati ya maadili.

8.Update 18:50
CC imemaliza Kikao chake, Nape amesema majina matano yaliyopendekezwa yatatolewa baada ya Kufuturu.
mkuu hiyo futari bado tuu?
 
Jamani juice yangu inapata moto na pirton zangu zitaexpire. Si mtangaze tu nijue nakunywa juice au pirton?
 
Jamani na umeme nao wamekata sasa tutaangaliaje habari uuuwwwiiiiii.....
 
Nadhani na watanzani wanachukulia mgombea wa ccm kama vile ndio Rais, kwanini?? Kama ccm anang'oka October waacheni na mambo yao. Au watz bado tunataka mafisadi???

Mkuu hujaelewa picha kamili. Wengi wetu tunavutiwa na kitakachotokea baada ya majina makubwa kukatwa. Huenda CCM ikafa kibudu. Kuna ka tamthiliya kazuri mno hapo!
 
Makongoro is the 5th president of Tanzania.
 
Back
Top Bottom