Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Kingunge ....

NEC na Kamati Kuu lazima wapitishe mtu anayekubalika ndani na nje ya Chama...

Lazima wanaoteuliwa wawe wamepitia ngazi zote na mafunzo ya Chama kwani ndiye anaenda kuwa mwenyekiti...

Huwezi kumpitisha mtu ambaye ni mwanagenzi ndani ya Chama...

Lazima tuelewe kuwa atakayependekezwa ndiye anaenda kuwa amiri jeshi wa nchi lazima tujiulize je ana uzoefu gani na masuala ya ulinzi..

Je, amepita JKT...??

Je, Amewahi hata kuwa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama...?
 
Wajumbe Zaidi Ya 1200 Wameazimia Wakiingia Tu Mkutanoni Wapige Kura Ya Kutokuwa Na Imani Na Mwenyekiti Wa Taifa Wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete Kisha Mkutano Uvurugike Na Kuwe Na Timbwilitimbwili Na Jambo Hilo Limeratibiwa Sana Na Mtia Nia ALIYEDANGANYWA NA UTITIRI WA UMATI WA WATU Kupitia Kwa Wapambe Wake Waliopo Mkoani Dodoma. Na Duru Zinaendelea Kusema Kwamba Kuna Uwezekano Mkubwa Mno Pakatokea Na Fujo Na Itakayopelekea MACHAFUKO Makubwa UKUMBINI Kwani Watu Wamegadhabika Sana Na Maamuzi Ya Jana.

Kama Mtakumbuka Vyombo Vyote Vya Habari Hasa TBC1, STAR Tv Na Clouds Tv Walitakiwa Waanze Kurusha Matangazo Yao Ya Moja Kwa Moja Tokea Saa 3 Asubuhi Leo Lakini Mazingira Hayajaruhusu Bado Kutokana Na Kwamba Kuna MTAFARUKU Unaendelea Na JK Sasa Anahaha Kumtuliza Na Kumweka Sawa Lowassa Lakini Bado Mmasai AMEKATAA KATA KATA Hivyo Kupelekea Kuchelewa Kuanza Kwa MCHAKATO Kamili Wa Mkutano Mkuu Na Mpaka Hivi Ninavyandika Uzi Huu Huko Dodoma Hali Si Nzuri Na Ulinzi Umeimarishwa Vilivyo Mithili Rais Obama Anakuja Tanzania Leo.

NINI KINAFANYIKA SASA?

Marais Wastaafu Wote, Wa Sasa Na Mawaziri Wakuu Wastaafu Sasa Wanafanya Mazungumzo Na Mheshimiwa Lowassa Ili Kumshawishi Na Kumpoza Kwa Ahadi Kuwa Baadhi Ya Watu Wake Watapewa Nafasi Katika Serikali Ya Awamu Ijayo Ila Bado Lowassa AMEDINDA ( Amekataa ).

KOSA GANI LA KIUFUNDI AMELIFANYA JK?

Hakika Katika Hili Hata Mimi Naungana Na Wachambuzi Wenzangu Wengine Wa Kisiasa Kwa Kumlaumu Moja Kwa Moja Mwenyekiti Wa Taifa JK Kwa Makusudi Na Kwa Kutumia Ushawishi Wake Na Turufu Yake Kama Rais Kumpendelea Kwa Wazi Wazi Mtia Nia Bernard Membe Wakati Kiutaalam Ilitakiwa Kama Akimkata Lowassa Basi Membe Nae Pia Akatwe Na Kama Aliamua Kumbakisha Membe Basi Hata Lowassa Angebakishwa ILI Kutengeneza Uwiano Wao Kwani Hakuna Ambaye Hajui Kuwa CCM Ina Makundi Mawili Tu Ambayo Ni Kundi Kubwa La Lowassa Na Kundi Kubwa La Membe. Rais JK Hii Dhambi Itakutesa Milele Kwa Ulichokifanya Kwani Katika Hili Hakika Karata Zako Ulizicheza Vibaya.

ATHARI GANI INAELEKEA KUTOKEA KWA CCM NA KWA NCHI?

Hakika Katika Hili Hakuna Jinsi Na Wala Tusipepese Macho Wala Kutikisa Masikio Kwamba Ni Dhahiri CCM Wasipojipanga Na Kulimaliza Hili Chama Kinaweza Kupoteza Umaarufu, Wabunge Na Kikaathirika Na Kuna Hatari Pia Ya Kutokea MPASUKO Mkubwa Ambao Pia Utahatarisha Hali Ya AMANI Ya Nchi Na Kuelekea Hata Katika Machafuko Na Kuna Kila Dalili Kama Hali Hii Haitotatuliwa Serikali ITATIKISIKA Na Kuwapa Mwanya Jeshi Kuchukua USUKANI Kwa Muda.

NINI KIFANYIKE ILI KUOKOA HALI HII?

Kwakuwa CCM Sasa Kuna MPASUKO Mkubwa Baada Ya Lowassa Kukatwa Na Membe Kubakishwa Katika Kinyang'anyiro Kitu Ambacho Sasa Wanatakiwa Wakifanye Ni Ama Kumuengua Membe au Kumurudisha Lowassa Ili KUKINUSURU Chama Kisha CCM Kwa Nguvu Moja Impitishe Dr. John Pombe Magufuli Apeperushe Bendera Kwa MASHARTI Kwamba Akiwa Madarakani Basi Ahakikishe Vigogo Wawili Hao Anawapa Majukumu Kwa Maslahi Ya Chama.

Hayo Ndiyo Machache Niliyonayo, Niliyoyapata Kwa Muda Huu Na Mtazamo Wangu Pia ILA Dodoma Sasa KIMENUKA Na Kuna HALI Ya Wasiwasi Mno IMETAWALA Huku Watu Wakiogopa Nini KITATOKEA.

haya uliyoyaandika ya kweli au ni hadithi uliyojitungia? kama ni kweli toa chanzo cha hii hadithi yako.ninachokijua lowasa ameshakatwa na hawezi kufanya lolote la sivyo apelekwe segerea
 
Cha kufurahisha UKAWA ndiyo wanapambana kuwatafutia CCM mgombea safi.

Wao wanajua lazima rahisi atoke CCM na wengine wamekiri humu na kutaja safu ya viongozi wa CCM watakaounda serikali.

Dr.Slaa kama unafuatilia huu uzi nadhani unajionea mwenyewe utaendelea kuwa rais kivuli tu.

Nawapenda ccm maana wanagawa hela
Kuna mtu kakamatwa na hela sasa sijui leo posho tutapata wapi mkuu. Riz
 
Cha kufurahisha UKAWA ndiyo wanapambana kuwatafutia CCM mgombea safi.

Wao wanajua lazima rahisi atoke CCM na wengine wamekiri humu na kutaja safu ya viongozi wa CCM watakaounda serikali.

Dr.Slaa kama unafuatilia huu uzi nadhani unajionea mwenyewe utaendelea kuwa rais kivuli tu.

mkuu si umesema unataka Dr slaa awe rais?
 
mmasai wetu yu wapi...aseee kitanukaaaaa si punde....
 
Tuliliona hili mapema na kusema ukweli i was really dissapointed. Hivi tuseme chama cha mapinduzi na wazee wote hawa hawakuforesee hili eti unamtoa Lowassa alafu unamuacha Membe??????
Hivi walitegemea nini????
Kama umemtoa Lowassa lazima Membe nae atoke ili nchi itulie. Ila if it happens Membe anabaki basi its either of the two system i collapse au yatokee machafuko na basi nchi wapewe wapinzani.

Kikwete anatakiwa ajue kuwa muda wa kuweka mazingira mazuri na ya amani kwa kustaafu kwake ni huu. Yaani leo huku kila sehemu napita watu wanasema Lowassa kakatwa Membe kabakishwa na wanaamini ni influence ya Familia ya MKUU kwa sababu Membe na Migiro wote ni watu wa karibu na familia ya mkuu.

Honeslty hali sio nzuri ndugu yangu, hawa jamaa maamuzi yao yanaliangusha taifa rasmi. Tuombeni.
 
tena wakileta kelele ndani ya NEC watatolewa nje haraka sana....

sio kutolewa nje tu...na kuwekwa Lupango

Unajua uzuri wa haya mambo Ushahidi wa Rushwa zote unaweza kupatikana

Nchi hii ukiamuliwa kushughulikiwa unashughulikiwa vizuri sana

Huwezi kuleta Masharubu mbele ya Rais wa Nchi
 
Kwa msisitizo, rais bado ni Lowassa ila kupitia nje ya CCM, infact nashauri ndie awe mgombea wa UKAWA!.

Pasco
Pole sana ndugu Pasco mlimwamini sana Mkwere,naamini katika watu walioumia kwa maamuzi haya ni wewe hata Lowasa mwenyewe hajaumia kama wewe ulivyoumia na tatizo lako kubwa unaamini sana katika siasa za Mtu kuliko Chama kama Taasisi. Ulianza kwa Zitto sasa kwa Lowasa. Na kaa ufahamu kuwa Lowasa hana nafasi Ukawa,panapomfaa ni ACT tuu sababu ndege wanaofanana uruka pamoja.
 
Edward Lowassa kukatwa sawa sawa kabisa ila pia Membe nae alitakiwa akatwe kwa sababu matendo mengi aliofanya EL na Membe kayafanya hivyo membe nae alishapoteza sifa(ninajiuliza kwa nini membe kapitshwa
 
nakumbuka yupo mchungaji mkubwa siwezi mtaja kwa jina akiwa katika kipindi cha mfungo wa miezi miwili alioteshwa UKAWA kuchukua nchi mwaka-2015.

Pia TB Joshua na wachungaji fulani walioteshwa eti ENL ndiye raisi wa JMT awamu ya 5!
 
Yeye ni nani mpaka wambembeleze namna hii, aliingia ubia na nani kuwa lazima awe rais
 
haya uliyoyaandika ya kweli au ni hadithi uliyojitungia? kama ni kweli toa chanzo cha hii hadithi yako.ninachokijua lowasa ameshakatwa na hawezi kufanya lolote la sivyo apelekwe segerea

Siku Hizi Najiepusha Mno Na Sana Kubishana au Kujibizana Na MAPOPOMA. Huna Unachokijua Na Tulia Tu Tulio Jikoni Tuwe Tunakupakulia!
 
Cha kufurahisha UKAWA ndiyo wanapambana kuwatafutia CCM mgombea safi.

Wao wanajua lazima rahisi atoke CCM na wengine wamekiri humu na kutaja safu ya viongozi wa CCM watakaounda serikali.

Dr.Slaa kama unafuatilia huu uzi nadhani unajionea mwenyewe utaendelea kuwa rais kivuli tu.

Hvi Asha rose migiro anasali jumapili au yeye ni wale walioko kwenye mwezi mtukufu wa ramadhan namanisha muislam?
 
Lazima sauti za wananchi zisikilizwe....

Anaulizwa kwa nini majina yamechelewa sana kutangazwa tofauti na miaka ya nyuma??

Kingunge anasema...

Inatia shaka katibu wa itikadi wa NEC alisema hakuna mtu ambaye ataruhusiwa kukata rufaa...

hii ni mbinu ili masuala yasijadiliwe kwa kina na watu kukata rufaa...

Kingunge anasema utaratibu wa mwaka huu ni wa hovyo tofauti na miaka ya nyuma...

Kuhusu kauli ya kina Nchimbi & Co...

Anasema utaratibu wa kamati kuu ni kujadili na kupata concensus, lakina misingi ikikiukwa wajumbe wana haki ya kikatiba kuonesha hisia zao...

Lakini wengine wanatumia demokrasia hiyo hata kutoka nje ya kikao...
 
Back
Top Bottom