Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Lowasa anajichekesha hapo ili awe salama na asisomeke maazimio yatapangwa kwenye kamati kuu ya kundi lake nini cha kufanya saizi anajua taasisi zote zinamtolea macho lazima ajifanya mnyonge hata kwa nape kweli mzee ni mafios
 
wakuu kwa mujibu wa mjumbe ndani ya kikao cha Nec amesema January magufuli na migiro ndio waliopenya tatu bora

Kwa hiyo kwa mujibu wa huyo mjumbe ndani ya NEC tayari Membe naye wameshamkata?
 
Yule bingwa wakukariri km za barabara na mtendaji bora ktk baraza la mawaziri kipenz cha wa Tz ndie atakayekuwa rais wa Jamuhuri ya muungano. Tumuombe nakumwambia Mungu ampe nguvu na ustadi mkubwa kulitumikia taifa la Tz. Thank you God
ccm ni watoto wa baba mmoja hawana tofauti ni walewale tu.refer Bunge la katiba
 
Yule bingwa wakukariri km za barabara na mtendaji bora ktk baraza la mawaziri kipenz cha wa Tz ndie atakayekuwa rais wa Jamuhuri ya muungano. Tumuombe nakumwambia Mungu ampe nguvu na ustadi mkubwa kulitumikia taifa la Tz. Thank you God
Dont tell me all four options of WAMA PROJECT have failed to convince members. Basi thanks to God
 
Dr John Pombe Magufuli ndie atakaye peperusha bendera ya Tz na ccm. Mungu akampe afya na nguvu kuwatumikia wa Tz. Kusema kweli haki imetendeka na tunasababu kumuunga mkono Dkt Magufuli, he do a very gud job in ths nation.
 
Kwenye ubunge utaona chama kinatoa rushwa hadharani kweupe hata kwenye urais saizi wanajifanya clean watanzania tunakosa mbongo tunahadaika , ni kama tuna madafu badala ya mbongo
 
Kweli mafuliko hayazuiwi na mikono,haya ni matokeo ya kuzuia mafuriko kwa mikono,Haya ni Maamuzi ya Lowasa na kura zake anadumbukiza kwa January,JK hakujipanga vizuri kumtosa Lowasa
 
Wanajamvi,lazima tukubali kwamba,tangu nchi hii ipate uhuru,kama CCM watampitisha Magufuli ktk nafasi yaUrais na hatimaye kushinda,ndiye atakuwa Rais Bora kuliko wote baada ya Nyerere.Hana Makundi,ana uwezo wa kusimamia nidhamu ya watumishi wa umma na ni mtu pekee anayeingia kwenye kinyang'anyiro bila kutumia nguvu kubwa,utendaji wake unambeba.Historia mbaya aliyonayo ni ya kuuza Nyumba za serikali.Hata hivyo alikuwa anatekeleza amri ya bosi wake;Hon Ben.Tumpe support,ila Ukawa tuwape wabuge wa kutosha ili bunge liwe uwezo wa kuiadabisha serikali.Utaratbu wa yes--ndiyoooooo!!!!!bungeni uishe kabisa.
 
  1. Dr. John Pombe Magufuli
  2. Bernard Camillius Membe
  3. Dr. Asha Rose Migiro

Baadae Atakayepita Mwishoni Atakuwa Ni Dr. John Pombe Magufuli Kwasababu Wajumbe Wote Wa Mkutano Mkuu Na Waliokuwa Wakimuunga Mkono TEAM NIMEKATWA NALIA Wataamua Kumuunga Mkono Magufuli Kwani TEAM NIMEKATWA NALIA Hawawezi Kuthubutu Kuwapitisha Membe Na Migiro Kwakuwa Wanajua Kuwa Wote Hao Ni Pro JK Hivyo Wataamua KUKINUKISHA Ili Kuwakomoa. Magufuli Ndiyo CCM Flag Bearer Na Possible Next President IWE ISIWE Na Mazingira Yote Yanambeba Na Kama Ni Mtanzania Unayejitambua Basi Ni Lazima Tu UTAPENDA Magufuli Awe Kiongozi ( Siyo Mtawala ) Ajaye. Kiongozi Ni Mtu Anayekubalika Na Mtendaji Wakati Mtawala Yeye Ni Mpenda Utukufu, Kutembea Na Kusimamiwa. Tanzania Ya Sasa INAMTAKA Kiongozi Na Siyo Mtawala Na Magufuli Naturally Ni Kiongozi Japo Kama Binadamu Ni Lazima Tu Atakuwa Na Mapungufu Yake ILA Mema Yake Na Utendaji Kazi Wake Ni Wa KUTUKUKA. Binafsi Namtakia Kila La Kheri Na Inshaallah Dr. John Pombe Magufuli Atapita....Amen!

Huenda akapita lakini swali linabaki kuwa ni nani ataweza kurudisha uzalendo uliopotea ndani ya chama hicho? Mtu mmoja huwezi, iwapo watendaji wako hawako na wewe hii imemshinda mkwere na hakuna atakaeiweza tena, watatupotezea miaka kumi kumi ya maisha yetu mpaka tuzeeke ndani ya umasikini, bora watoe kijiti kwa wengine kwani wao walizaliwa ikulu?! Nani amewaambia hii ni dynasty ya ccm? Wapishe kwa muda nao wakae nje wajipime makosa yao, kama watarudi watakuwa wamejirekebisha.
Maana kutupa rais msafi ni kutupa ahadi zijazo wakati maswali yaliyopita bado hujayajibu! Wajibu ufisadi wao kwanza ndipo watoe mtu, vinginevyo huyo msaffi, anaeonekana kuwa msafi njanja tu ya wao kuendelea kuwepo ili asiweze mtu kuwahoji kwa mabaya yao yaliyopita!
 
Back
Top Bottom