Kijiji cha Magufuli pale Chato kinawapa ushawishi baadhi ya watu kumuona Magufuli kama fisadi!
Hebu tujaribu kuiuliza historia na hisabati ili tuweze kumjadili vizuri. John Magufuli (JM) amekuwepo Bungeni na Serikalini tangu awamu ya 3 ya Mhe. Ben Mkapa hadi awamu hii ya 4 ya JK. Ni wazi kuwa JM amekuwepo kwenye taasisi hizo takribani tangu miaka 20 iliyopita. Nyumba 60 kila moja inaweza kuwa na construction value isiyozidi Tsh. 35,000,000/= ambapo jumla yake ni takribani 2.1 billion/-. Ukichukua 2.1billion ukawagawanya kwa miaka 20 utapata Tsh. 105,000,000/= kwa mwaka. Ukienda mbali kidogo ukagawa 105,000,000/= kwa miezi 12 utapata Tsh. 8,750,000/= kwa mwezi, kipato ambacho ni cha kawaida tu hata kwa mtu ambaye siyo mbunge wala waziri. Ikumbukwe pia kuwa Enzi za Mkapa kachukua Gratuity ya Bunge mara 2, kipindi cha Kikwete kachukua Gratuity ya Bunge mara 1 na sasa anachukua nyingine ya 2. Kiwango cha Gratuity ya Bunge unakijua vizuri. Aidha zipo fursa nyingi za mikopo kwa wale wanaoukwaa ubunge hivyo kwa mtu mwenye vision ya maisha haitamsumbua kujenga nyumba 60 kama za JM pale Chato.