Wakuu salaam,
Leo Julai, 7 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwasili mkoani Morogoro kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili katika maeneo ya Msamvu manispaa ya Morogoro, Dumila wilayani Kilosa na wilaya ya Gairo.
Aidha Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw. Martin Shighela alisema ziara hiyo ya Samia Suluhu Hassan atakutana na Wananchi na hivyo akatoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais wao.
Pia Rais Samia anatarajiwa kushiriki mkutano mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania utakao fanyika Julai 8 katika manispaa ya Morogoro.
Tutakuwa hapa sote kuwaeleza yanayojiri.